Mfumo wa Elimu Vyuo Vikuu umeexpire

Mfumo wa Elimu Vyuo Vikuu umeexpire

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,096
Reaction score
22,826
Habarini wanadau!

Rejea kichwa cha habari hapo ndipo ujumbe wa leo unahusika.
Katika jamii yeyote ya viumbe uijuayo hapa duniani iwe ni mwanadamu, wanyama hata wadudu, elimu ni swala nyeti sana katika kuisaidia hiyo jamii ya viumbe kusurvive kizazi kimoja hadi kingine.

Elimu si tu swala nyeti bali ni swala tete ambalo hutakiwa kufanyiwa utafiti na marekebisho ya kina kila sekunde iendayo na pumzi. Nasikitika kusema kuwa kwenye mataifa ya Afrika, tanzania tukiwamo tumefeli kwa dhati katika swala la elimu kwa maana ya mfumo rasmi wa elimu.

Kwann ukienda vyuo vingi tanzania iwe ni masters au degree bado tunaendeleza ule utaratibu wa sekondari wa kusoma ili umeze badala ya kusoma kwa namna ya kutafakari na kuja na majibu binafsi kwa kutumia ufahamu wa kuzaliwa nao. Kwa mfano leo hii, ukienda kwa mwanafunzi anayesomea banking au microfinance utakuta wanajifunza kuna aina ngapi za taasisi za kifedha, banki zipo za aina ngapi basi....halafu mwisho wa siku hayo ndio majibu ya maswali atakayoulizwa katika mitihani yake. Na siku akihitimu huyu mtu ataitwa msomi........na kiuhalisia ni msomi kwa maana amesoma notes nyingi sana huko darasani. Ila uwezo wa ubongo kutoa majibu ya hali ya uhalisia ni sifuri au kiwango cha chini. Cha ajabu watu ambao hawana elimu ya chuo au wenye ufaulu mdogo vyuoni ndio huja na udadisi mzito sana wenye kutoa majibu yenye kuleta mabadiliko, hawa wenye ufaulu wa juu ambao kiuhalisia si productive, hukalia kuvimbisha vichwa kama sijui kitu gani na jeuri za kujiona wajuaji kumbe si lolote.

Kwann hivi hatufikirii kubadili mfumo wa elimu ili tuanze kupata watu vichwa.....?!

SONY Xperia Z5 Premium
 
Hii kituu hata mimi ilinipa tabu sna wakati naanza kusoma masomo ya uhandisi ilaa nilivyovikuta ni tofauti na matarajio yangu

Nokia ya Torch
 
Back
Top Bottom