hhhhj
Member
- Oct 5, 2016
- 41
- 68
Nianze na hili la mfumo wetu wa elimu maana kama tukiliacha liendelee hivi ni matarajio yangu hakuna kipya tutakacho kitarajia katika elimu.....
Mfumo wetu wa elimu upoje?
Kwanza mfumo wa elimu ni utaratibu unaowekwa ili kufikia malengo na dira ya elimu katika eneohusika....
Mfumo wetu wa elimu unajumuisha elimu ya awali(1),elimu ya msingi(7),elimu ya sekondari(4) +(2),elimu ya juu (3+)....Lengo hasa la mfumo huu nikupitia michakato tofauti katika kuondoa ujinga Tanzania.lakini ifahamike mifumo hii inatofautiana kila nchi kulingana na malengo na dira......
TATIZO LA MFUMO WETU...
Elimu ya awali
Nielimu ambayo kwanza kama imesahaulika kwani haupo mpango maalumu wa kuiboresha elimu hii.kwani kwa kipindi kirefu sasa serikali haidahili walimu wa awali baadala yake vyuo binafsi ndiyo vimekuwa vikifanya hivyo....
Hii imepelekea kumekuwa na uholela wa waalimu wa awali kwani hata yule asiye na vigezo nao husomea.....
Elimu msingi
Hapa ndipo matatizo yote huanzia kwani kitu chochote kizuri lazima kiwe na msingi mzuri....
Hatutaweza kuwaandaa wataalam wa hesabu wakati mtihani wake majibu achague....Hatutaweza kuongeza ushindani wa kujifunza kama mtoto hatuta mchuja darasa mpaka darasa....
Hatutaweza kufika popote kama upimaji kwa mwanafunzi utafanyika mara mbili(kwa mujibu wa pesa ya captation)....Hatuwezi kufika popote bila ya kufuta sheria inayoruhusu utoro ambayo inasema ili mtoto afukuzwe kwa utoro sharti akae siku tisini yaani akikaa 80 bado unamuhesabu mwanafunzi na hapa unazalisha wasiojua kusoma hatimae usumbufu sekondari.....
Elimu sekondari
Kama hatutakuwa mpango madhubuti hapa tukiendelea kuuamini mtihani wa darasa la saba kuwa ni kipimo tunajidanganya.....
Huwezi kuingia sekondari kwa kushedi baada ya kuchagua utakachofanya utabahatisha naunaweza kufaulu.....
Nangoja niwaambie kitu mitihani hii ya darasa la saba ya kushedi majibu kama swali zima a-d utashedi majibu basi utapata kwakuwa mashine ya kusahihisha mtihani hii huwa inasahihisha jibu sahihi tu yaani huwa imesetiwa isahihishe jibu la kweli tu itakalo kutana nalo kwa kila swali ikikosa inaruka swali lingine.....
Kwa mfumo huo matokeo wanafaulu hata wasio na sifa mpaka wavuta bangi mwisho wa siku mwalimu anapiga anapata kesi...
MWISHO
Mie nafikiri ipo haja ya kuupitia upya mfumo wetu wa elimu la sivyo tutatoa matamko kila siku na kufukuzisha watu kazi huku mzizi wa tatizo upo palepale...