EXTERMINATOR
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 343
- 90
Kutokana na athari za itikadi za vyama katika kuongoza nchi, napendekeza kufuta mfumo uliopo wa vyama kuongoza dola na badala yake ziundwe taasisi za kutunga sera na mipango ya serikali ambayo wananchi watapewa kuchagua ni ipi inafaa kama ilivyo katika uchaguzi mkuu na taasisi itakayoshinda sera na mipango yake ndiyo itakayotekelezwa na serikali kwa kipindi kitakachopendekezwa katika sera husika. Kuhusu upatikanaji wa uongozi wa juu nchini katiba ielekeze sifa za wagombea huru ambao wataelezea utekelezaji wa sera za taasisi zinazoshindanishwa na kuchaguliwa sambamba na sera. Mwisho wa siku hakutakuwa na ushabiki wa vyama kwani taasisi hizi ni za kitaalam na ni za serikali na hazitafanya harakati za kisiasa. Wadau naomba maoni niwasilishe kwenye ngazi husika