Mpunilevel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2015
- 3,140
- 1,871
Toka Rais Magufuli aanze kusafisha uozo na kuleta nidhamu kwa watumishi wa umma, neno mfumo limetawala miongoni mwa wadau mbali mbali.
Kwamba kazi aifanyayo ni bure bila kuweka mfumo thabiti kwa watumishi wa umma. Sipingani na mawazo hayo ya kuweka mfumo thabiti ndani ya serikali yake ili haya ayafanyayo yawe endelevu.
Lakini tujiulize hapo nyuma wakati wa utawala wa awamu ya kwanza ya Hayati mwalimu julius kambarage nyerere kulikua na mfumo gani? Nasema hivyo kwa sababu hatukushuhudia haya ya uhalifu wa namna hii unaotokea sasa.
Nauliza wadau tatizo ni watu kukosa uzalendo na nchi yao au ni mfumo?
Naamini team ya watu ambao hawako tayari kuitumikia nchi yao kwa weledi hata uweke mfumo upi, watajipanga kuhakikisha mfumo huo haufanyi kazi, kwani watakua wametanguliza ubinafsi kwenye huo mfumo.
Anayoyafanya Rais Magufuli ya kusafisha serikali na kuamsha hali ya watumishi kufanya kazi kwa weledi ni la kuungwa mkono na kila raia mwema wa nchi hii.
Tumwache asafishe uozo , kisha abaki na cream ya watumishi ambao mfumo ukiwekwa utafanya kazi.
Naamini pia hawezi kuwafuta kazi watumishi wote wazembe, na wabadhirifu lakini Kuna percent kubwa flani ya maeneo flani ndani ya serikali yatakaa sawa na mambo yatakwenda vizuri.
Mwisho namaliza kwa kusema kiongozi wa nchi ni kioo cha watumishi wa serikali na jamii kwa ujumla. Kama mzembe, na watumishi watakua wazembe. Kama si mfuatiliaji vivo hivyo kwa walio chini yake na kama ni mbadhirifu vivo hivyo na.....
Ni mtizamo tu!