godson Lomayani
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 538
- 711
Wakuu nakuja mbele zenu muweze kunisaidia hata kwa ushauri tu kwa sababu naamini hapa JF kuna vichwa vya kila aina vilivyobobea katika fani mbalimbali.Wakuu kama title inavyojieleza nimeamua kujitokeza mbele yenu ili muweze kunisaidia.Mwaka 2009 niliondoka Kibaha kuelekea Segera nikiwa naendesha pikipiki aina ya Honda Freeway Cc 250,baada ya kulivuka daraja lililokuwa likinijulisha sasa naingia mkoa wa Tanga takriban M.200 baada ya kulivuka lile daraja mbele yangu kulikuwa Semi trailer inakuja kwa speed na mimi pikipiki ilikuwa imekubali mwendo,dereva wa Semi alikuwa akija huku amebana zaidi upande wangu kwa sababu kulikuwa na kona lakini haikuwa sharp,basi mimi kuona vile ikabidi nitoke nje ya site yangu na kutembea kwenye ule mstari wa njano ulioko pembezoni mwa barabara,sasa ile semi iliponipita ule upepo wake uliniyumbisha na kunitoa kabisa barabarani,kosa nililolifanya nilitanguliza chini mguu wa kushoto pikipiki kwenye kasi hali iliyopelekea mimi kuanguka na kutupwa umbali kiasi,nilikuwa siamini kama nimepata ajali,lakini nilikuja kurealize baada ya kujikagua na kukuta ankle ya kushoto ikiwa imehama sehemu yake na mguu kuwa kama namba 7 ilikuwa serious complicated dislocation,wasamaria wema walinibeba kwenye kitanda kilichosukwa kwa makuti hadi kituo kidogo cha afya pale Manga wengine walikokota pkpk hadi kwa mwenyekiti wa eneo lile la Manga na kutoa taarifa kwake kuhusu ajali niliyopata,naye bila kuchelewa aliwataarifu Polisi wa kituo cha Kabuku.Baada ya kufikishwa kwenye kituo cha afya niliona manesi wakiziba midomo hali iliyonifanya nihisi nimeumia sana kwa sababu nilipata open wound kwa hiyo wale manesi walishtuka ndipo mama mmoja wa makamu akaamuru niingizwe kwenye moja ya vyumba yeye mwenyewe alinivua raba niliyokuwa nimevaa,sio siri wakuu baada ya kuona mguu ulivyokuwa nililia na kujua naenda kukatwa mguu.Yule mama alinifariji na kuniambia ntapona,alinichoma diclofenac injection kunipunguzia maumivu,na baada ya muda mwenyekiti kijiji cha Manga alifika akiwa kwenye L/rover ya askari Polisi,wakaanza kunihoji jinsi ajali ilivyotokea baada ya kuwaeleza wakataka kunipeleka hospitali ya Handeni,niliwaomba wanipeleke Kibaha kilipo kituo changu cha kazi,na ilipo pia Hospitali ya Tumbi.Wakuu nimetibiwa MOI na Lugalo lakini bado mguu haujakaa sawa,nikitembea mguu unaonekana umepinda kwenye ankle ya kushoto na pia maumivu ni makali nnapotembea umbali mrefu.Msaada wenu tafadhali.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app