Mfanyabiashara Maarufu Arusha Samiri Patel Mbaroni

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
634
1,000
Mfanyabiashara Maarufu wa madini,Mwenye asili ya kiasia ,Samiri Patel anayemiliki kampuni ya Madini ya Gyan gems jewellers ltd jijini Arusha, amekamatwa na Polisi mkoani Manyara kwa kosa la kukutwa na Madini akitorosha kinyume na utaratibu.

Patel ambaye ni mtunza hazina wa chama cha wafanyabiashara wa Madini TAMIDA ,anadaiwa kukamatwa na polisi katika bar ya Songambele ,Mererani wilayani Simanjiro wiki iliyopita akiwa na shehena hiyo ya Madini aina ya Tanzanite akidai kupatiwa na mfanyabiashara mwenzake wakati akijua hana leseni ya biashara hiyo.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Madini mkoani humon(Majina yamehifadhiwa)wamedai kuwa Mfanyabiashara huyo amekuwa akitumiwa na wafanyabiashara wenye asili hiyo kutorosha Madini kinyume cha sheria huku akitumia kivuli cha kufahamiana na baadhi ya viongozi wa serikali.

Hata hivyo Polisi Mkoani humo imemwachia kwa dhamana mtuhumiwa huyo kwa Madai kwamba shtaka linalomkabili lina dhamana na wakati huo jalada la shtaka lipo kwa mwanasheria wa serikali likisubiri kurejea ili kuweza kufikishwa mahakamani .

Akiongelea tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoani humo,Agustino Senga amethibitisha kushikiliwa kwa mfanyabiashara huyo na kwamba yupo nje kwa dhamana hadi upelelezi utakapokamilika kuweza kumfikisha mahakamani.

" Ni kweli amekamatwa ila tunasubili taarifa ya mwanasheria wa serikali tuweze kumfikisha mahakamani mtuhumiwa "Amesema kamanda Senga.

Hata hivyo taarifa zinadai kwamba mfanyabiashara huyo ni moja ya wanamtandao wa utoroshwaji wa madini ambao kwa sasa mianya yao imedhibitiwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo ujenzi wa ukuta wa Mererani.

Katika hatua nyingine Afisa Madini Mkazi Mkoani Manyara ,RMO Daud Ngalula alipotakiwa kuzungumzia madai hayo alishindwa kutoa ufafanuzi badala yake alikata simu ,baada ya kuwepo madai ya kuwabeba baadhi ya wafanyabiashara wa madini wanaoenda kinyume na utaratibu .
images%20(4).jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom