Mfalme wetu ropokizi

Mfalme wetu ropokizi

Kweli huyu ni mfalme ropokizi, amelewa pombe ya madaraka ndiyo maana anapenda sifa na hajaribiwi
 
Ngoja namimi niharibu kama ifuatavyo...

Unajua tunakopelekwa na tulipo fikia nizaidi ya .......ohoooo ninamke nawatoto bado wananitegemea jamani sorry.
 
style wanayoishi ccm siku hizi inaitwa "kujikaza kisabuni".
Yaani wanavumilia tu hata km chama chao kinahatibiwa na Faru....
Nlitegemea wawe wa kwanza kupeleka hoja ya kutokuwa na imani kwa kukiuka katiba na sheria za nchi. Kujipa utukufu binafsi. Kujenga airport binafsi huku wanafunzi wakikosa mikopo na hakuna dawa hospitalini na hakuna chakula kwenye maghala ya serikali. Kutumia ubabe na kutisha wananchi kwa kisingizio cha hapa kazi tu....na upumbavu mwingine mwingi unaofanywa na huyu mpayukaji, mropokaji na mkurupukaji
 
  • Thanks
Reactions: bne
MFALME WETU ROPOKIZI.

View attachment 461755

Eeh Mfalme Juwa,
Mfalme wetu wa ajabu, watawala huongozi,
Sote twapata adhabu, mashavu tele matozi,
Umetutia ububu, kuamba hatukuwezi.

Eeh Mfalme Enze enze,
Hivi sasa aghalabu, kufungwa kwa uchochezi,
Mahakama zetu tabu, zapangiwa maamuzi,
Haikupona maktabu, nayo yatia jelezi.

Eeh Mfalme Jeuri,
Bunge lakula kababu, zilizoungwa na rozi,
Mpishi ni weye babu, mwenye fikira tatizi,
Hii ndio asbabu, kupitishwa upuuzi.

Eeh Mfalme Ropokizi,
Watisha kwa lako gubu, kutwa domo liko wazi,
Waropoka kwa ghadhabu, mfiwa hubembelezi,
Hakika huna adabu, wewe bwana ropokizi.

Eeh Mfalme Katili,
Muda wenda taratibu, ka jua halichomozi,
Ela twafanya hesabu, saa siku na miezi,
Yaja siku ya dhahabu, jua utasema mwezi.

Eeh Mfalme Rahimu,
Mwisho nafunga kitabu, huu sio uchochezi,
Mesema yanotusibu, na kututoa machozi,
Ewe bwana tahdabu, koma wako ubazazi.

19 January 2017.
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whats app 0622845394 Morogoro
Naota kui miss JF in advance.
 
Nimecheka sana hapo eti acha "UBAZAZI"

Na nimeshtushwa na hilo "Mfalme Katili"

Kisha nikashangazwa na hilo la "Mfalme Juha".
 
Dotto C. Rangimoto sikuiona hii mkuu uwe unanitag kaka Nakumbuka miaka ya 80 ilikuwa mchana nakumbuka ilikuwa ikitoka mchana mwema inakuja kipindi cha Malenga wetu.ila Morogoro imetoa washairi wazuri sana
 
Daaah ngoja waje wataalamu wa lugha za mashairi useme dhima yako nini?!! Haya mkuu mi nakunywa chai chapati hapa kwa raha tu
 
Ubunifu tunao...shida ni kuugeuza huu ubunifu uweze kutuletea mafanikio,kitu cha ajabu kwa wabongo ni uwezo wetu wa kuwakashifu wale walioweza kupigana na kufanikiwa katika vile walivyovitamani maishani mwao,kwa mfano leo kuna watu wanaomkashifu rais wa WCB kuwa sio kitu ilhali mafanikio aliyopata yanazidi jumla ya mafanikio ya koo zote zinazompondea,sasa turudi kwa mfalme tajwa hapo juu,mbali na madhaifu yake lakini aliweza kupambana na kufanikiwa kufikia nafasi ambayo wengi wetu hatufikirii kama hata wajukuu zetu wanaweza kuwa,badala la kukesha kumkejeli na kumsimanga ni wakati sasa wa kutafakari kuwa hivi vipaji vyetu tunavyovitumia vibaya tunawezaje kuchannel hiyo energy ilete mafanikio kwetu binafsi na kwa taifa letu. Asubuhi njema amigos
NB;baba tiffah kapost Rolls Royce,msaga sumu hebu tutafutie kadi ya gari!
 
Hilo shairi limejaa uchochezi, dharau, udhalilishaji kwa kupitia lugha ya kishairi
 
Back
Top Bottom