Mfalme Kibaka

Mfalme Kibaka

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,536
Reaction score
3,883
WIMBO unaitwa Juicy. Mali ya Notorious BIG. Ni release ya kwanza, albamu ya kwanza, Ready to Die.
Intro; Biggie anasema:

"Albamu hii ni salamu kwa walimu wote waliosema sitofanikiwa.
Ni kwa wote walioishi juu kwenye mijengo niliyo-hustle mbele yake.
Waliniitia polisi nilipokuwa natafuta pesa ya kumlisha mtoto wangu.
Ni kwa niggas wote katika mapambano.
Unajua nasemaje?
Kila kitu kipo vema."
Baby, Baby, Baby
!

Anamaliza.

Verse ya kwanza; Biggie anarap ilikuwa ndoto kuwa staa wa Hip Hop. Aliwaona Salt-n-Pepa na Heavy D kwenye jarida la Word Up wakiendesha magari ya kifahari. Akachukua picha na kubandika ukutani.

Anaeleza alipokuwa akipigika, hakuna aliyewaza kama Hip Hop ingempa vyeo, heshima na utajiri. Anasema kama hujui jua. Kila kitu kipo vema. Verse ya pili; Biggie anarap kuwa amebadili mchezo kutoka kibaka mpaka mtu mwenye ukaribu na wanahabari mashuhuri. Anamtaja mwandishi, Robin Leach.

Biggie anasema yeye sio mtu cheap tena, anakula raha na kusambaza upendo na wanaye wa Brooklyn. Anasema hakujua kama rap ingempa yote, maana alikuwa akiuza unga atengeneze pesa. Anatamba maisha ni poa japo alionekana mpuuzi alipoacha shule, kama uhujui ujue.

Verse ya tatu; Biggie anarap kuwa alipokuwa anapigika hakuwaza maisha ya kifahari ambayo alianza kuishi baada ya ustaa. Nyumba nzuri, magari, bili za simu hazimsumbui maana mhasibu wake alirekebisha. Kila siku ni raha. Kiu inapozwa na shampeni. Ni kwa sababu alibadili mchezo kutoka hasi hadi chanya. Kama hujui jua. Mambo yapo safi.

Chorus; wapo Total, wanaimba "Unajua vizuri wewe ni nani. Usiwaache wakudidimize. Fikia nyota. Unalo lengo. Lakini yasiwe mengi. Maana wewe ni mmoja." P Diddy anachomekea maneno. Ni wimbo ambao Biggie alitulingishia maisha ya ukwasi na ustaa, baada ya zama za kuuza unga na wizi. Unahamasisha kukomalia ndoto.

Jana ilivuma kuwa wimbo huu, Juicy, uliimbwa na wakazi wa Brooklyn wakiwa karantini. Reuters wamesema ni uzushi.
Audio inayosikika ni ya mwaka 2010, shoo ya Jay Z, akimuenzi Biggie. Majengo kwenye video ni Upper West Side, Manhatan, sio Brooklyn, NY.

Pamoja na hivyo, haiondoi ukweli, Biggie ni Mfalme wa Brooklyn. Kutoka Kibaka hadi Mfalme.

Credit: Luqman MALOTO
 
Aisee baharia unatuangusha...pamoja na kucopy na kupaste bila kuichosha akili yako ukashindwa hata kuichosha akili yako utengeneze tittle yenye mashiko na inayoeleweka dah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom