Mpauko
R.I.P
- Jan 19, 2019
- 2,323
- 3,451
Anaitwa Secretary bird,kwa kiswahili ni Karani Tamba.
Karani tamba ni miongoni mwa ndege ambao wanapatikana kwa wingi hapa nchini Tanzania hasa huonekana kiurahgisi katika maeneo tengefu ya hifadhi za wanyamapori.
Ndege huyu mwenye umbo kubwa ambae ni mla nyama kama jamii ya ndege kipanga na mwewe anapatikana barani Afrika tu.
Kutokana na uzuri wa ndege huyu imepelekea baadhi ya mataifa barani Afrika kumuweka ndege huyu katika nembo zao za taifa na mataifa hayo ni Sudani na Afrika ya Kusini.
Ndege huyu ameitwa karani kutokana na manyoya yaliyo simama sehemu ya nyuma ya kichwa chake mfano wa karabi ya karne ya 18 na alama ya kalamu katika kona ya mbawa zake na hatimae jina karani likatokea kwa ndege huyu.
SIFA NA TABIA ZA KARANI TAMBA
Karani tamba wana muonekano wa kufanana zaidi na ndege kama kongoti au korongo tofauti na ndege wenzie jamii ya walao nyama.
Ana kichwa kidogo na mwili mkubwa kama tai huku mdomo wake hasa mdomo wa juu ukiwa umejikunja kuelekea chini.
Karani tamba ndio ndege mwenye miguu mirefu kuliko ndege wote katika jamii ya ndege walao nyama. Wana magamba magumu sana kwenye miguu yao na hii huwasaidia wasi dhurike hasa pale wanapo pambana na mawindo yako kama panya na nyoka.
Dume na jike wana fanana sana ni ni vigumu kuwatofautisha japo jike huwa na mwili mdogo kidogo kuliko dume.
Ndege hawa ni wakimya sana na mara nyingi wanapotoa sauti basi huwa ni ya chini na husikika marachache sana watoapo sauti.(sijui ndo nae introvent?)
Kimo- hufikia kimo cha mita 1.3-1.4 wastani wa futi 4.5.
Upana wa mabawa hufikia mita mbili ambao ni sawa na futi 6.6.
Uzito-ndege hawa hufikia uziti wa kilogramu 2.3-5
Wanapendelea sana maeneo ya wazi yenye majani mafupi na savana japo wana uwezo wa kuishi maeneo ya nusu jangwa na sehemu zenye miti na vichaka
Karini tamba ni miongoni mwa ndege walao nyama na hupendelea sana kula nyoka, mijusi, vyura, wanyama jamii ya panya, ndege wadogo na mayai ya ndege wengine. Muda mzuri wa mawindo kwa ndege hawa huwa ni mchana kwani wana uwezo wa kuona mchana zaidi kuliko usiku.
Japo wakati mwingine hula mizoga ya wanyama ambao wameuwawa katika mazingira yao.
Karani tamba huishi wawili katika maisha yao, hii ina maana kwamba dume mmoja huishi na jike wake mpaka nwisho wa maisha yao. Dume hawezi kuwa na jike zaidi ya mmoja hali kadhalika jike hawezi kuwa na dume zaidi ya mmoja.
Jike hutaga kuamzia yai 1 – 3 na kila yai moja hutagwa kwa tofauti ya siklu 2- 3. Mayai hutamiwa kwa muda wa siku 42-50 na jukumu la kutamia huwa wana shirikiana wote dume na jike japo jike ndio hutumia muda mwingi kutamia mayai kuliko dume. Katika kipindi chote cha kutamia mayai kazi ya kutafuta chakula huwa ni ya dume. Hivyo dume hulazimika kutafuta chakula na kumletea jike katika kiota.
Karani tamba ana uwezo wa kuishi wastani wa miaka 10 – 15 awapo katika mazingira yake asili japo kama anafugwa kwenye bustani za wanyamapori basi huweza kufikisha hadi miaka 19.