Mfahamu samaki ambaye dume ndio huzaa

Thewildlife_tz

Senior Member
Joined
Apr 23, 2019
Posts
127
Reaction score
85
Wanaitwa SEAHORSE Hawa ni wanyama wasio na uti wamgongo wanaopatikana katika bahari ya pasific Kitaalam anaitwa "Hippokompus"

Jina hili ni la kigiriki likimaanisha "hippo" horse na "kompus" likimaanisha sea monster (ila huyu kweli kama monster )

Ni moja ya jamii ya wanyama na wanapumua kwa kutumia giills na wanauwezo wa kuogelea wana shingo na wanamkia mrefu kama wa nyoka.

Wana urefu kufikia cm 35 na speed yao ni mita 2 kwa saa moja (mdogo mdogo) .

Wana macho makali sana na yenye uwezo wa kuona sehemu mbili tofauti bila kutegemea jicho moja linaweza angalia nyuma na lingine mbele hii ni kwaajili ya mawindo ya prey

Wanakula wadudu wadogo dogo waitwao "Mysis Shrimp" na anakula mara 50-60 kwa siku moja

Jike anaumiliki wa eneo (100sqm), dume anamiliki 0.5q kama kawaida hapa dume anakimbizwa mchaka mchaka kila kitu ndio bebe

SASA HAWA WANYAMA DUME NDIO ANABEBA MIMBA NA KUTOA WATOTO (daah dume anazaa mwe! Mwe! Mwee! (Kwa sauti ya senga )

Maisha yao yote wanakuwa na jike na dume mmoja tu hamna kucheat.Jike anamfuata dume anaenda kuishi nae kwake na ndio anafanya kila kitu
ishara ya kukubaliana wote hubadilika rangi hapo mambo mukidee na huishi sehemu moja

Sasa muda wa kuzaa dume huwa na pochi kwenye tumbo na jike huhamishia mayai kwa dume yakiwa bado kabisaa na yakishaingia kwa dume huboreshwa na hukaa kwa siku 14 mpaka wiki 4 ambapo hutoa watoto mpaka 150

Kitendo cha kuzaa hutumia masaa 8 hadi masaa 12.. ndio shuhuri huishaa ( kama ni mimi ningekufa bachela)

Watoto wanaitwa fry na huishi kivyao tangu kuzaliwa

DOWNLOAD VIDEO
Sasa hicho kitendo ndio dume anazaa hapo anakaa mpaka masaa kumi na mbili huku jike anamchora tuu

Naamiini kabisa wangekuwa watu kuna wengine wangebaki na kufa bachelor hapo ndio anatoa watoto mpaka 150 hadi 200 akimaliza vyombo vinamsubiri kuoshaa, na kusafisha nyumbaa bila kusahau kuwinda.[emoji2532][emoji2532]..

follow us on instagram Thewildlife_tz
 

Attachments

  • thewildlife_tz-20190425-0003.mp4
    1.9 MB
Huyo jamaa nae bwege tu, atakubali vipi kupelekeshwa kijingajinga ivo si kuna samaki wengi tu akachague jamii nyingine
 
safiiii naku fatilia sana instagram kamanda
sasa unge kua na acc youtube ili unapo upload video kule ukishare link apa inakua rahis sie wenye storage ndogo tunakua tuna stream badala ya kuzi download kama ilivo sasa
 
safiiii naku fatilia sana instagram kamanda
sasa unge kua na acc youtube ili unapo upload video kule ukishare link apa inakua rahis sie wenye storage ndogo tunakua tuna stream badala ya kuzi download kama ilivo sasa
sawa sawa mkuu nitafanya hvyo mkuu wangu
 
Mtoa post unajua maana ya dume lakini??

Sifa za dume;-
Dume halizai.
Halina muda wa kutoa malezi.
Dume linazalisha.

Kwa ujumla hicho kiumbe kimepoteza sifa ya kuwa dume.

kumbuka
Sio kila uambiwacho na mzungu ukubali. Mambo mengine tumia akili mwenyewe
 
ha ha sawa mkuu ila nature ya binadamu sio nature ya wanyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…