Michael Chairman
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 922
- 583
Moise katumbi aliyekuwa mwanachama wa chama tawala nchini congo alipokuwa akishililia wadhifa wa gavana wa jimbo la Katanga , baadaye akajiengua kutoka chama tawala na kujiunga na upinzani September mwaka jana, ambapo upinzani ulimtaka awe mgombea wa Urais kupitia mwanvuli wa vyama saba yaani G seven, katumbi alindika Tangazo lake la kugombea Urais kupitia ukurasa wake wa twitter.
Lakini serikali kupitia waziri wa sheria mpaka sasa imetangaza mashitaka juu ya Moise katumbi kuwa amejiri mamluki kwenye shughuli zake na sasa Moise katumbi ameitwa na mwendesha mashitaka wa serikali kujibu shutma hizo ambapo Moise yeye kasema kuwa hizo ni njama za kutaka kukwamisha harakati zake na kumchafulia jina Moise katumbi.
my take , wakati wa demokrasia kukua afrika ndiyo wakati wa wakuza demokrasia kuwa makini zaidi
updates...Baada ya maelezo kuhusu historia ya kina ya Moise katumbi ,,,,jina kamili lake anajulikana kama MOISE KATUMBI CHAPWE aliyezaliwa mwaka 1964 /12/28 na mama mkongo na baba yake muitaliano Mzee Nissim Soriano ambaye alikimbia italia kutokana na unyanyasaji mpaka congo akiwa na Dada zake wawili mwaka 1938 , mwaka huo wakaanza kuishi kwenye jimbo la Katanga ambapo mzee huyu walipendana na mwanamama wa kikongo aliyetoka kwenye kabila la kazambe ambao huu ulikuwa ukoo kifalme ,walianza maisha na mtaliano huyu. Mwaka 1964 wakamzaa Moise katumbi ambaye alianza shule kwenye shule ya kiwele iliyokuwepo Lubumbashi. Moise katumbi alimuoa bi Carine katumbi binti aliyetoka kwenye familia ya kitajiri. kwa maelezo ya jumla Moise katumbi alianza kufanya biashara akiwa na umri wa miaka 13 ambapo alikuwa akiuza samaki baadaye alikuza biashara zake na kuanza kumiliki mgodi (Mining Company Katanga) in 1997, kisha alianza biashara ya usafirishaji , na uuzaji wa vyakula. Biashara hizi zilimpa utajiri mkubwa sana na umarufu uliopelekea kujitosa kwenye mambo ya siasa mwaka 2007 ambapo alichaguliwa kuwa gavana wa jimbo la Katanga na vilevile toka mwaka 1997 amekuwa kiongozi wa timu ya TP mazembe timu yenye umarufu mkubwa barani afrika.