Mfahamu mbu mdudu hatari kwa mauaji

Thewildlife_tz

Senior Member
Joined
Apr 23, 2019
Posts
127
Reaction score
85
MBU/MOSQUITO

Kwa mwaka mmoja mbu anauwa watu zaidi ya 430,000
kitaalam Mbu anaitwa "CULICIDAE" ni moja ya wadudu hatari warukao anapatikana sehemu zote katika dunia na wako katika species 3500

Mbu ana miguu sita na mwili wake umegawanyika katika sehemu tatu, na macho mawili, antenna mbili za hisia pamoja na mbawa mbili ambazo hutumia kuruka
Mbu anapiga mabawa mara 580 kwa sekunde 1.
na anauwezo wa kupaa kwa spiidi ya 2.6 km/h ( yaani hapo ndio katembea spidi ya falcon)

Na kawaida mbu hawezi kupaa juu ya futi 23 lakini kuna baadhi ya mbu wa Amerca sehemu za barafu huweza kuruka mpaka futi 8.000

Anapokuwa kwenye kutafuta chakula dume ndio huongoza safari kwa kupiga mabawa na kutoa sauti na wakifika eneo la tukio dume hukaa pembeni na jike kusaka chakula

mbu jike ndio anaeng'ata na ni kwasababu Anahitaji protein nyingi kwa matumizi ya mwili wake kama kurutubisha mayai
Ila mbu dume yeye hushindia maji tu

Mbu anafahamu kabisa tabia za binadamu kabla ya kumfanya kitoweo anasenser ambazo hugundua joto la mwili pamoja na kufahamu upumuaji wa mwili yaani kuvuta hewa na kutoa anajua huyu mzima au mgonjwa ( mgonjwa hana tabu nae)

Mbu yuko active sana wakati wote mchana na usiku wao "kazi tu"
Kawaida mbu hategemei sana damu kuishii ila anategemea sana maji, na hana meno ila jike huwa anakunywa damu mara tatu ya uzito wake

Mbu haambukizi ukimwi kwasababu hana receptors za kubeba vile virusi hivyo huishia kubeba damu tu
na sababu kubwa ya kuambukiza malaria ni kwakua kwenye mwili wake huwa anakua na parasite ambae huishi kwenye mate na humuacha anapong'ata

Kwa maramoja mbu anataga mayai 200 na huanguliwa baada ya siku 10 ambapo hukaa pembezoni mwa maji wa siku kumi ndio huenda kusaka chakula
mbu dume anaishi siku kumi tu
na jike anaweza kuishi mpaka siku 60 kama asipo kutana na isreal binadamu

VIDEO
Hapo ndio anopheles yuko kazini lakini huwa analindwa na dume na kupewa

NINI UNATAKIWA KUFANYA KUZUIA MBU
1. hakikisha hakuna majan na majimajii yanayokuzunguka kwnye nyumba yako
2.hakikisha unapulizia dawa au kutumia vyandalua
3. ukisikia dalili za kuumwa nenda kamuone daktari mara moja

tupige vita maralia inauwa

instagram Thewildlife_tz
 

Attachments

  • thewildlife_tz-20190425-0002.mp4
    1.7 MB
hapo mbu anapohitaji protein kwaajili ya kurutubisha mayai bado sijaelewa, protein hii hii au?
naomba elaborations zaidi chief...

asante kwa uzi mzuri.
 
hapo mbu anapohitaji protein kwaajili ya kurutubisha mayai bado sijaelewa, protein hii hii au?
naomba elaborations zaidi chief...

asante kwa uzi mzuri.
shukrani kwenye damu kuna protein ambayo humsaidia mbu jike kurutubisha mayai yake
 
''Ila mbu dume yeye hushindia maji tu"

Ina maana hanywi damu kabisa hata akimfuma mtu?
 
''mgonjwa ( mgonjwa hana tabu nae)''

Unamaanisha nini hapa kwamba mbu hamuumi mgonjwa kabisa?na ni mgonjwa gani was malaria?

Vipi kuhusu wanyama,Je mbu hanywi damu ya mnyama(kuuma mnyama)?
 
''mgonjwa ( mgonjwa hana tabu nae)''

Unamaanisha nini hapa kwamba mbu hamuumi mgonjwa kabisa?na ni mgonjwa gani was malaria?

Vipi kuhusu wanyama,Je mbu hanywi damu ya mnyama(kuuma mnyama)?
mbu wengi huwa hawanywi damu ya mgonjwa wa malaria tayari na mbu hushindwa kung`ata mnyama kwasababu ya nywele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…