Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,351
- 9,846
Wazito wa JF nawasalimia,
Carlos The Jackal, kwa jina la kuzaliwa anaitwa Ilich Ramirez Sanchez,alizaliwa mwaka 1949 huko Venezuela.
Carlos alizaliwa katika familia inayojiweza kiuchumi,ambapo baba yake alikuwa ni mwanasheria mahiri mwenye itikadi za kikomunist,hata jina la Ilich alilompatia Carlos lilikuwa kwaajili ya kumuenzi mwanamapinduzi wa kikomusti wa Urusi aitwae Lenin,ambae Ilich lilikuwa ni jina lake la kati.
Duniani kuna magaidi wakubwa maarufu wawili ambao karibu kila mtu amepata kuwasikia,Carlos the Jackal na Osama bin Laden.
Tofauti kubwa ya Carlos na Osama ni kwamba Carlos yeye alikuwa gaidi wa kisiasa wa itikadi za kikomunist wakati Osama bin Laden yeye ni gaidi wa itikadi za kidini.
Pia tofauti kubwa zingine ni kuwa Carlos yeye alikuwa ni gaidi ambae anapanga mikakati na kwenda front mwenyewe kwenda kuitekeleza wakati Osama alikuwa yeye ni mpanga mikakati na mfadhili wa matukio ya kigaidi.
Kwa mukhtadha huo utaona kuwa Carlos the Jackal ndo gaidi mkubwa aliyepata kutokea duniani.
Carlos alianza kujiunga na movement za kisiasa za kikomunist tangu bado akiwa mdogo kutokana na msukumo wa baba yake, ambae alikuwa mkomunist muaminifu.
Alijiunga na chama cha National Communist Party cha nchini Venezuela mwaka 1959 kabla ya kwenda kujiunga na camp ya Matanzas huko Havana Cuba.
Mwaka 1968 alijiunga na chuo kikuu cha Patrice Lumumba cha huko Urusi ambacho kilikuwa maarufu kwa kuzalisha wanamapinduzi hodari duniani.
Lakini hakukaa sana akawa amefukuzwa hapo chuoni kwasababu mbalimbali ikiwemo kutokufaulu vizuri masomo yake na matatizo mengine na uongozi wa chuo hicho.
Baada ya kufukuzwa chuo alienda moja kwa moja mpaka Beirut Lebanon ambako alijiunga na kundi la PLPF na kujitolea kuwa mpiganaji kwa ajili ya kuwatetea wapalestina pamoja na kupinga uzayuni.
Mwaka huo wa 1970 ndo mwaka ambao Carlos alianza rasmi kuwa mpiganaji wa kigaidi,alipofika Beirut alipelekwa huko nje ya mji wa Amman- Jordan kwaajili ya mafunzo ya upiganaji kwa kutumia silaha.
Alipokamilisha mafunzo hayo alienda kujifua zaidi kwenye chuo cha mambo ya kijeshi kinachoitwa H4 ambacho walikuwa wanafundishwa na maafisa wa kijeshi wa Iraq mpakani mwa Iraq na Syria.
Baada ya kukamilisha mafunzo hayo,alienda kujiunga na wapiganaji wa Black September huko Jordan,ambao ni kundi la wapalestina waliokuwa wa PLPF na PLO chini ya Yasser Arafat ambao walikuwa wakipigana na serikali ya Jordan.
Akiwa na Black September ni huko ambako alijizolea umaarufu wa kuwa mpiganaji hodari na jasiri.
Baada ya vita ya Jordan kuisha Carlos alipelekwa jijini London ili aweze kuwa anakusanya taarifa za watu muhimu wenye itikadi kali ya kizayuni ambao wanatakiwa watekwe au wauawe.
Baada ya kukamilisha hii kazi alienda Ufaransa ambako alikutana na Mohamed Boudia ambae ni gaidi habari ingine wa kizazi chake.
Mohammed Boudia alikuwa na sifa ya kipekee ya kujibadili muonekano na hata kutokea kama mwanamke,mzee nk pale anapotaka kuwakwepa majasusi wa Mossad wa Israel.
Waziri mkuu wa Israel kipindi hicho mama Golda Meir alimuweka Boudia katika list ya watu 11 ambao lazima wauwe kwa sababu ya kushiriki kupanga na kutekeleza mauaji ya wana michezo wa Israel kwenye Olimpic ya Munich mwaka 1979 (Tafuta movie inayoitwa Munich).
Akiwa na Mohamed Boudia walifanya matukio mengi ya kigaidi kwa kushirikiana.
Walitumia advantage moja kubwa ya kufanana,Carlos na Boudia walikuwa wanafanana wajihi hata kimo,na kwasababu Mohamed Boudia kipindi hicho tayari alikuwa ni gaidi anayewindwa na shirika la kijasusi la Mossad na lile la Ufaransa la DST,walikuwa wanahakikisha wanakuwa katika muonekano mmoja wa kufanana muda wote ambao ulikuwa unatumika kuwaingiza maboya majasusi waliokuwa wanawafatilia.
Kwa mfano kama Mohammed Boudia alikuwa anataka kwenda kufanya tukio,Carlos alikuwa ndio anaanza kutoka kwenye nyumba na kuondoka na gari..
hii ilikuwa inapelekea wale waliokuwa wanamfatilia wamfuate kwa nyuma kujua anaenda wapi,kuonana na nani na kufanya nini.
Kwa kutumia mwanya huo Carlos alikuwa anawazungusha mji mzima kupoteza muda na huko nyuma Muhammed Boudia alikuwa akitoka na kwenda kufanya matukio.
Hii haikuchukua muda sana kabla mamlaka za usalama za Mossad hazijashtukia mchezo na kumuua kwa bomu la kutega kwenye gari Mohammed Boudia mwaka 1973.(Tafuta kitabu cha Maisha ya Mohammed Boudia).
Baada ya kifo cha rafiki yake Mohammed Boudia,Carlos alifanya tukio la kulipa kisasi la kutaka kumuua Joseph Sieff alikuwa ni mfanyabiashara tajiri na kiongozi wa movement za kizayuni aliyekuwa anaishi ufaransa, ambapo alimpiga risasi ya chini ya pua,na alipotaka kummalizia bastola aliyokuwa anaitumia ilijam hivyo akakimbia.
Mwaka 1975, aliekuwa mtu wa kati wa mawasiliano (contact person) kati ya PLPF na Carlos,Michel Mourkharbal alikamatwa na shirika la kijasusi la DST la ufaransa na kubanwa ili akawaonyeshe Carlos (mpaka kipindi hicho hakuna shirika la kijasusi lilikuwa linamjua Carlos kwa sura), Michel pamoja na spy agents hao wa DST walimkuta Carlos katika house party na marafiki zake wakinywa.
Baada ya kutakiwa awaonyeshe Carlos ni nani,alipowaonyesha tu Carlos aliwashuti wote watatu na kuwauwa.Baada ya tukio hilo alitoroka ufaransa na kwenda Beirut.
Mwaka 1975 Carlos alitikisa dunia kwa kuongoza kundi la Black September na kuwateka mawaziri na maafisa wa ngazi za juu 60 wa nchi zinazoongoza kwa kutoa mafuta duniani OPEC, huko Vienna Austria.
Katika tukio hilo watu watatu waliuwa, Carlos alitoa sharti kwa serikali ya Austria kusoma kwenye TV na radio kila baada ya masaa mawili juu ya mateso ya watu wa Palestina ama sivyo ataendelea kuua mateka.
Kitu ambacho kilitekelezwa na serikali ya Austria. Baada ya siku mbili walipatiwa ndege ambayo iliwapeleka mpaka Libya ambako Ghadafi alikataa kuwapokea kwasababu kati ya hao watu watatu waliouawa alikuwemo afisa wa Libya.
Waliachia baadhi ya mateka na kuelekea Algeria ambako aliachia mateka waliobaki.Baada ya tukio hili Carlos alifukuzwa kutoka katika kundi la PLPF kwasababu ya kukiuka maelekezo ya mkuu wake Waddie Haddad kwa kutokuwaua mawaziri wa OPEC pale alipoona kuwa masharti waliyotoa hayakutekelezwa.
Katika tukio hili inasemekana Carlos alipokea mshiko wa nguvu kutoka serikali ya Saudia ili asiwadhuru mawaziri na maafisa wake, kati ya dola million 20-50,ambazo wenzake wanasema alizichikichia kwa matumizi yake binafsi na sio kwaajili ya mapambano ya kuikomboa Palestina.
Baada ya kufukuzwa ndani ya PLPF Carlos alielekea Ujerumani mashariki ambako walikuwa wanafata itikadi ya kikomunist,ambako alipewa support ya wafanyakazi 75 na aliweza kuunda kundi lake mwenyewe linaloitwa Organization of Armed Struggle,ambalo lilikuwa na wapiganaji wa kilebanon,Syria na waasi wa kijerumani.
Ambapo aliendesha harakati zake za kigaidi kwa kulipua sehemu mbalimbali za ujerumani magharibi.Inasemekana kipindi chote hiki Carlos alikuwa agent wa shirika la kijasusi la KGB la Urusi lililokuwa likimuunga mkono na kumtumia kwa siri.
Mwaka 1982, aliekuwa mke wa Carlos-Magdalena Kopp,alikamatwa nchini ufaransa akiwa na gaidi mwingine wa kikundi cha Carlos wakiwa wamebeba milipuko kwenye gari,baada ya kukamatwa Carlos alitoa sharti waachiwe ama atalipua sehemu mbalimbali za Ufaransa.
Serikali ya nchi hiyo ilikataa,kitu kilichosababisha kutokee balaa la milipuko ya mfululizo iliyojeruhi watu mamia na kuua zaidi ya watu kumi.
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha,miaka ya mwisho wa vita baridi kati ya marekani na Urusi,Carlos alikuwa hapati support tena aliyokuwa ameizoea kutoka kwenye nchi zinazofata mrengo wa kikomunist.
Mataifa mengi yaliyokuwa yanamtumia yaliona hayana kazi nae tena na kuanza kumfukuza katika nchi zao.Mpaka kufikia mwaka 1985 Hungary walimfukuza ambapo alijaribu kwenda Iraq,Libya na Cuba ambako nako walimkataa.
Mwishoni alipokelewa na Syria ambao walimpa sharti la kutojihusisha na mambo ya kigaidi.
Ambapo alikaa bila kufanya matukio yoyote mpaka mwaka 1991 ambapo serikali ya Saddam Hussein walimfuata baada ya kuisha vita vya ghuba, ili akawafanyie kazi za kigaidi dhidi ya nchi za magharibi, jambo ambalo lilipelekea Syria kumtimua na akaelekea Jordan ambako aliishi kwa muda mfupi kabla ya kupewa hifadhi Sudan (Tafuta movie inayoitwa Carlos).
Mwaka 1994 mashirika ya kijasusi ya Marekani na Ufaransa yalipata fununu juu ya uwepo wa Carlos nchini Sudan na kuanza kumfuatilia.
Baada ya makubaliano na nchi ya Sudan ilitakiwa akabidhiwe kwa Ufaransa.Jambo ambalo lilitekelezwa kipindi ambacho Carlos alikuwa amefaniwa operesheni ya tezi dume.
Mlinzi wake alimsubiri akiwa amelala usiku akampa dawa ya kumlevya na kumfunga miguu na mikono kisha walimuhamisha hapo hospitali na kwenda kumficha mahali pengine.
baadae walimkabidhi kwa shirika la kijasusi la Ufaransa lililomsafirisha mpaka Paris kwaajili ya kwenda kujibu mashtaka ya kuwaua majasusi wawili wa ufaransa pamoja na informer wao.
Mwaka 1997 alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Huyo ndo Carlos the Jackal, gaidi aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kujibadili ili asiweze kukamatwa na ambae aliisumbua sana dunia zaidi ya miaka 20.