Meya wa Kinondoni aungana na Meya wa Jiji kumpinga Makonda

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
WAKAZI WA KINONDONI,MUWE NA AMANI NA UTULIVU,HUU NDIYO MSIMO WA VIONGOZI WENU MLIOWAPA DHAMANA YA KUONGOZA JIJI LA DAR ES SALAAM,
NAUNGA MKONO TAMKO HILI HALALI LA MEYA WA JIJI
*TAARIFA KWA UMMA*
Leo Tar 15/07/2016

YAH: KUTAARIFU WANANCHI WA DAR ES SALAAM YA KWAMBA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NI *BATILI* NA HALIWEZI KUTEKELEZEKA.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mstahiki Meya Isaya Mwita Charles anapenda kutoa ufafanuzi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam Juu ya agizo ka Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda aliyeagiza kuwe na msako wa nyumba kwa nyumba kutambua wasio na kazi maalum.

Yafuatayo ni muhimu sana kutambuliwa na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kama *haki* yao ya msingi kabla ya utekelezwaji wa Amri hii ya Mkuu wa Mkoa.

Kwanza zoezi hili ni BATILI na haliwezi kutekelezeka kwenye Halmashauri zetu za Jiji la Dar es Salaam kwa sababu za msingi zifuatazo:

*i)* Sheria ya makosa ya Jinai Inaelezea utaratibu wa kukaguliwa nyumbani kama search warrant ambayo inatolewa Na Mahakama au polisi, Na ambayo Inaelezea wanatafuta nini.

*ii)* Sheria hiyo pia inamtaka mwananchi kuwakagua maafisa wa Mahakama Na Polisi watakaofika Nyumbani kwake ili wasiweze kumpandikishia ushahidi wa uongo.

*iii)* Kamwe popote duniani Kibali cha wananchi kukaguliwa majumbani hakiwezi kutolewa Na Viongozi wa kisiasa.

*iv)* Kwa maagizo hayo inasemekana wananchi watawekwa ndani Kwa kukataa kutii agizo hilo, hakuna sheria Tanzania inayoruhusu Mwananchi kuwekwa ndani kwasababu za hovyo Kama hizo.

Naomba nimalizie Kwa kusema wananchi wote wa Jiji la Dar wawe na Amani kabisa na wajue haki zao na wajue kuzitetea, sisi viongozi wao tupo imara kusimamia haki zao na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Asanteni sana na Mungu awabariki.

Imetolewa na,
Isaya Mwita Charles,
Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
 
Asiye na kazi maalum ni nani? Na kazi maalum ni IPI?

Waliomaliza vyuo kwa level mbalimbali km degree, diploma, na certificate na hawajapata kazi zinazohusiana na taaluma yao lakini wanasongesha maisha kwa namna nyingine kama udereva wa private cars eg kupeleka watoto wa jirani shule au housegirl sokoni wanatakiwa waadhibiwe au haiwahusu?

Kwa wale hawana kazi kama mwenye nyumba wangu kila siku ananisubiri nimlipe kodi ndo aishi, vipi makonda nani anastahili kuwa mkazi wa Jiji hili. Kodi ya serikali nalipa na mwenye nyumba namlipa lakini kodi yake mwenye nyumba wangu we huipati kodi yake

Naungana na meya wanaostahili kuishi jijini ni wale wenye utashi wa kuishi jijini ili mradi wawe na mchango kwa maendeleo ya jiji.

Meya chunga ....Mayor beware
 
Unasaka wasio na kazi huku umesitisha ajira zinachaji kweli? watu tuna vyeti vyetu makabatini tena vizuri tu kuliko chake sasa anataka tulazimishe kuajiriwa?

yeye kama amebahatika kupata kazi na gentleman yake basi asinyanyase wengine, ajue hata Sitta alikuwa na kazi leo ni jobless.
 
Asiye na kazi maalum ni nani? Na kazi maalum ni IPI?

Waliomaliza vyuo kwa level mbalimbali km degree, diploma, na certificate na hawajapata kazi zinazohusiana na taaluma yao lakini wanasongesha maisha kwa namna nyingine kama udereva wa private cars eg kupeleka watoto wa jirani shule au housegirl sokoni wanatakiwa waadhibiwe au haiwahusu?

Kwa wale hawana kazi kama mwenye nyumba wangu kila siku ananisubiri nimlipe kodi ndo aishi, vipi makonda nani anastahili kuwa mkazi wa Jiji hili. Kodi ya serikali nalipa na mwenye nyumba namlipa lakini kodi yake mwenye nyumba wangu we huipati kodi yake

Naungana na meya wanaostahili kuishi jijini ni wale wenye utashi wa kuishi jijini ili mradi wawe na mchango kwa maendeleo ya jiji.

Meya chunga ....Mayor beware
Ha ha haaaaa umenifurahisha sana basi aje amkamate mwenye nyumba wangu hana kazi maalum kutwa anashinda kibarazani.

Huyu jamaa sijui ame define vipi mtu asiye na kazi maalum au anadhani kazi hadi uingie ofisini.
 
Mkuu wa mkoa yupo sahihi kazi za wana dar wengi ni unjustified, hongera kwa kijana mwenzangu, vijana siku zote tunawaza kwa speed, itawezekana tu taratibu.
 
ndio matokeo ya kusifiwa na mkuu, hadi mtu anapitiliza, anajisahau na kutoa maagizo yasiyotekelezeka.amalize kwanza la ombaomba na walimu kupanda daladala bure.
 
Tatizo mh. Makonda haja-define maana ya neno ajira kwa muktadha huu.
Lakini sababu za mamea zinapanguliwa ndani ya dakika moja tu. Makonda Kupata search warrant pamoja na kukabidhi hilo jukumu kwa jeshi LA polisi hashindwi.
 
Kuna kazi Makonda angetakiwa awe ameshaimaliza then tungemuelewa!

1: kuwahamisha Mashoga wote hapo Dar!
2: kuwarejesha omba omba wote makwao!
3: waalimu kupanda daladala bure Dar!

Kwa madawati nakupa %100 big up!
 
"Mkiweka picha zenu kwenye pesa muweke na zet ili pale mnapotumia mtutumie na sisi"
cc mjomba
 
Back
Top Bottom