Meya wa Ilala aunda kikosi kazi cha kukusanya kodi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa sasa inafanyakazi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Halmashauri hiyo wakati wa kukusanya mapato. Ili kufanikiwa zoezi hili Kamati ya kudumu ya fedha na utawala ya Madiwani chini ya Mwenyekiti wake mhe.

Kuyeko ambaye ndiye Meya wa Manispaa ya Ilala imeunda kamati nane zitakazo fuatilia na kusimamia ukusanyaji mapato kwa lengo la kufikia makadrio ya bajeti ya mwaka 2015/2016 ambayo ni Tshs. 55,839,000,000.00/ fedha za mapato ya ndani. Ukusanyaji wa mapato kwa Manispaa ya Ilala umekuwa ukisuasua kutokana na ufuatiliaji na usimamizi mbovu wa maafisa wanao kusanya kodi.

Kutokana na ukusanyaji wa kodi kusuasua Mstahiki Meya ya Ilala, mhe. Charles Kuyeko ameunda kikosi kazi kitakachoingia mtaani kufuatilia na kusimamia ukusanyaji wa kodi. Kikosi kazi hicho kimegawanyika katika kamati 8 ambapo wenyeviti wa kamati hizo ni Madiwani na makatibu watakuwa wakuu wa Idara/ vitengo vya Halmashauri yetu.

Kamati hizo za kikosi kazi ni kamati ya majengo, kamati ya lesseni za biashara, kamati ya service levy, kamati ya makontena, kamati ya achinjio, kamati vibali ya ujenzi na kamati ya sheria na Mawasiliano. Kamati hizo zote zitasimamiwa na Naibu Meya wa Ilala mhe. Omary Kumbilamoto.

Uamuzi huo wa Manispaa ya Ilala umetangazwa Leo na mhe. Kuyeko katika mkutano wake na waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Arnautoglo jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mhe. Kuyeko amesema makadrio ya makusanyo ya mapato ya ndani kwa bajeti ya mwaka 2015/2016 ni Tshs.55,839,000,000/ lakini mpaka sasa tumekusanya bilioni 35 tu na tumebakiza mwezi mmoja tu kumali mwaka wa fedha wa bajeti tuliyoikuta. Hii haiwezi kukubalika. Natoa rai kwa watu wote ambao hawajalipa kodi walipe Mara moja kwa hiari kabla kikosi kazi hakijawafikia. Kikosi kazi kimeanza kazi tangu tarehe 01/06/2016.

Aidha, mhe. Kuyeko ameikosoa serikali kuu kuacha kuchelewesha fedha za ruzuku kwenda kwenye Halmashauri hiyo. Kuyeko amesema fedha za ruzuku hazifiki kwa wakati na zinapopatikana huwa ni chini ya kiwango kilichopangwa. Mfano katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 fedha za ruzuku za serikali kuu kwa Ilala ni Tshs. 108,230,807,338.33 lakini mpaka sasa tumepokea bilioni 66.8 sawa na 41% kitendo hicho kinatufanya tuwe na mazingira magumu ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wetu.

Manispaa ya Ilala inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitendea kazi hususani magari ya ufuatiliaji mapato, mwingiliano katika baadhi ya vyanzo vya mapato kati ya Halmashauri ya jiji na Manispaa ya Ilala.

Kadhalika tuna changamoto ya wafanyabiashara wa mahotel kutolipa Kodi kwa Manispaa yetu kutokana na waraka kutoka wizara maliasili na utalii. Kuyeko amesema wafanyabiashara wa mahoteli wanawaraka kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii unaowaelekeza wasilipe kodi ya huduma ya Jiji (City Service Levy) ingawa wanapata huduma zinazotolewa na Manispaa ya Ilala. Hivyo ni lazima tuzungumze na wizara ili utaratibu ufanywe kwa Manispaa kupata kodi toka kwa wafanyabiashara wa mahotel walioko Manispaa yetu.

Makadirio ya Bajeti 2016/2017 kwa mapato ya ndani ni Tshs. 85,200,000,000/ ili kufikikia malengo Halmashauri ya Ilala imeandaa mikakati ya ukusanyaji wa mapato. Mikakati hiyo ni pamoja na kununua magari mapya 20 ili kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato, kufanya utambuzi wa walipa kodi wapya pamoja na kutambua majengo ambayo bado hayajafikiwa katika ulipaji wa kodi, kuongeza machine 150 za kielectronic (pos) kwenye mitaa na Kata zote, kushirikisha jamii yote katika kuwatambua walipa kodi wapya ndani ya Manispaa yetu.

Katika kile ambacho kinaonyesha dhamira ya kweli katika kutekeleza mikakati hiyo Leo mhe. Kuyeko amefanya kikao cha kazi. Kika hicho cha kazi juu ya kukusanya mapato kiliwahusu wataalamu na wakuu wa Idara na vitengo vyote vinavyohusika na ukusanyaji mapato, wajumbe wa kamati ya fedha ya Madiwani, maafisa watendaji wa kata na mitaa, maafisa tarafa, na wenyeviti wa mitaa katika Manispaa ya Ilala.

Manispaa ya Ilala inafanya utaratibu wa kupeleka mashine za kielektroni kwa kila Kata, hakuna malipo yatakayofanywa kwa risti (receipt) za kuandikwa kwa mkono. Wafanyabiashara wajihadhari na matapeli wa aina hiyo.

Meya amewataka viongozi wa Kata na mitaa kushirikiana na kikosi kazi kilichoundwa kufuatilia na kukusanya mapato kwa Manispaa yetu. Lakini pia amewataka wajiepushe na rushwa wakati wa kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ndugu Isaya Mngurumi ametoa rai kwa wafanyabiashara na wamiliki wa majengo kulipa kodi kwa hiari kabla ya tarehe 30/06/2016. Mkurugenzi pia ametahadhali wale wote waliomba vibali vya ujenzi wa parking za magari katikati ya jiji hasa kariakoo lakini walienda kinyume nivibali vyao wajue wamevunja sheria hivyo nivyema wakajisalimisha kulipa faini na kisha wakabomoe majengo hayo na kisha wajenge kwa kufuata vibali vyao.

Imetolewa Leo 03/06/2016
Na Alex Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala.
0656-568256
 

Attachments

  • IMG-20160603-WA0097.jpg
    IMG-20160603-WA0097.jpg
    42.3 KB · Views: 38
Ushauri - msitumie mabavu kama watu wa ccm , mimi nina maduka makubwa matatu kariakoo , nawaahidi ushirikiano , nitalipa kodi na ama nitaweka na ziada kidogo , sina wasiwasi na serikali ya UKAWA , tunatakiwa kuonyesha mfano na ni lazima tutofautiane na ile mikwepa kodi ambayo ni mifadhili ya ccm .
 
Ushauri - msitumie mabavu kama watu wa ccm , mimi nina maduka makubwa matatu kariakoo , nawaahidi ushirikiano , nitalipa kodi na ama nitaweka na ziada kidogo , sina wasiwasi na serikali ya UKAWA , tunatakiwa kuonyesha mfano na ni lazima tutofautiane na ile mikwepa kodi ambayo ni mifadhili ya ccm .
Tushirikiane kuijenga ukawa imara Tanzania Nzima Mkuu
 
Ushauri - msitumie mabavu kama watu wa ccm , mimi nina maduka makubwa matatu kariakoo , nawaahidi ushirikiano , nitalipa kodi na ama nitaweka na ziada kidogo , sina wasiwasi na serikali ya UKAWA , tunatakiwa kuonyesha mfano na ni lazima tutofautiane na ile mikwepa kodi ambayo ni mifadhili ya ccm .
Kwahiyo sasa unaanza kulipa kodi sababu ni vibaka wenzako? Kwanini unataka kulipa zaidi? We kibaka tu aisee, hakuna namna
 
Kwahiyo sasa unaanza kulipa kodi sababu ni vibaka wenzako? Kwanini unataka kulipa zaidi? We kibaka tu aisee, hakuna namna
Ni uzalendo na kuguswa tu mkuu , mimi siyo kibaka kabisa , tangu nizaliwe sijawahi kudokoa hata sukari .
 
Back
Top Bottom