Meya Jacob amkaribisha DC Polepole

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Amwambie anasubiri busara imwongoze kama aende Ubungo ama abaki Kinondoni na akienda ni kwa ajili yake.

MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo katika kikao cha baraza la madiwani,amemkaribisha Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo Humphrey Polepole kuwasalimia madiwani hao kabla ya mgawanyo huo.

Awali kabla ya Polepole kuingia ukumbini, Meya Jacob alisema kwamba taratibu za serikali kugawanya manispaa ya kinondoni kuwa na ya Ubungo zinakamilika na wakati wowote, Wilaya hiyo inaweza kuanza kazi.

"Kama ambavyo tume ya uchaguzi ilianza michakato yake ya kugawa majimbo na hatimaye jimbo la ubungo likagawanywa na kupata kana jimbo la kibamba kulingana na wingi wa watu wake...
Ndiyo serikali kuu (Tamisemi)ili tangazo kuwa Wilaya ubungo na michakato ya kugawa Mali, mapato na watumishi yaliendelea na sasa tayari sehemu kubwa yamekamilika hata jengo la manispaa ....muda wowote watumishi na madiwani watatakiwa kwenda huko" alisema Meya Jacob

Hata hivyo akimkaribisha DC Polepole alisema " karibu sana Wilaya ya Ubungo ...mimi bado sijasema niende au nibaki wapi, nasubiri busara iniongoze hivyo tuko pamoja maana wote ni wamoja ila nikija huko ni kwa ajili yako jiandae"

NAYE DC Polepole akiwasalimia madiwani wa manispaa ya Kinondoni alisema kuwa angetamani Wilaya ya Ubungo iwe ya tofauti katika uongozi wake endapo kila kiongozi na mtumishi atafaa kazi kwa maendeleo ya nchi.

"Mh rais amenichagua nije katika wilaya mpya ya ubungo na nitoke msoma vijijini kwa malengo na kazi ile ile ya wakuu wote wa wilaya ya ulinzi na usalama wa wilaya husika lakini pia kwa ajili ya dhamana ya kusimamia sera na ustawi wa maendeleo hivyo tufanye shughuli zetu kwa amani"

" Kwa wanaonifahamu vizuri mie ni mwanaccm kweli kweli na siyo wa bahati mbaya, lakini naheshimu demokrasia ya ustawi wa vyama vingi na kufanya kazi na watu wengi kwani si mara ya kwanza kufanya kazi na viongozi wa upi nani ....nimefanyanao bila kuvunjiana heshima" alisema Polepole

DC Pole pole alisema kwamba anategemea siasa ya maendeleo katika wilaya hiyo na siyo siasa ya madaraka kwa kuwa msingi mkubwa wa kuwapo viongozi na watumishi ni maendeleo kwa eneo husika.
MBUNGE wa Kinondoni Maulid Mtulia (CUF)alimshukuru DC Polepole kwa elimu hiyo na kumuahidi kwamba kama ataweka mbele maslahi nchi basi watashirikiana naye bila migongano yoyote baina yao na yeye, watumishi na serikali kuu

"Nafikiri tuendelee na kazi ya kutafanya siasa ya maendeleo ili baadae tupate siasa ya madaraka ... ili mkiwa mnaitengeneza Ubungo ya tofauti, siye kinondoni tubaki na kinondoni ya pekee"
 
Attachments

  • IMG-20160712-WA0085.jpg
    IMG-20160712-WA0085.jpg
    65.7 KB · Views: 67
  • IMG-20160712-WA0084.jpg
    IMG-20160712-WA0084.jpg
    84.2 KB · Views: 54
  • IMG-20160712-WA0086.jpg
    IMG-20160712-WA0086.jpg
    63.8 KB · Views: 67
Karibu polepole turudishie shisha, usiwafukuze omba omba kwani ni dhambi mashoga nao watibiwe waache tabia zao.
 
Msimamo wa Polepole ni hivi vyeo vya ukuu wa wilaya kufutwa baada ya kuwasikiliza watz na yy akakubaliana na hilo... kwa nini asiige ya Cameron waziri mkuu wa UK aliye amua jiuzuru japo muda wake bado sbb waingereza wameamu jitoa EU wakati yeye haamini kuwa ni uamuzi mzuri? Kwa nn usiishi kwa matendo kwa kile unacho kiamini?
 
wakuu hivi kwa wilaya ya ubungo ni chama gani kina wabunge wengi? je kwa mgawanyo huu je kinondoni itaendelea kuongozwa na UKAWA?
 
UKAWA wanajiamini sana! Makonda anakimbilia PoLi CCM kutawala hana jipya! Sasa ile mikurupuko yake imekosa rhythm any more! Anatafuta singeli ingine akurupuke nayooo!! Awamu ya mwendokasi na kukurupuka style! ....ni zamu yetu kanda ireeee!!!
 
Amwambie anasubiri busara imwongoze kama aende Ubungo ama abaki Kinondoni na akienda ni kwa ajili yake.

MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo katika kikao cha baraza la madiwani,amemkaribisha Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo Humphrey Polepole kuwasalimia madiwani hao kabla ya mgawanyo huo.

Awali kabla ya Polepole kuingia ukumbini, Meya Jacob alisema kwamba taratibu za serikali kugawanya manispaa ya kinondoni kuwa na ya Ubungo zinakamilika na wakati wowote, Wilaya hiyo inaweza kuanza kazi.

"Kama ambavyo tume ya uchaguzi ilianza michakato yake ya kugawa majimbo na hatimaye jimbo la ubungo likagawanywa na kupata kana jimbo la kibamba kulingana na wingi wa watu wake...
Ndiyo serikali kuu (Tamisemi)ili tangazo kuwa Wilaya ubungo na michakato ya kugawa Mali, mapato na watumishi yaliendelea na sasa tayari sehemu kubwa yamekamilika hata jengo la manispaa ....muda wowote watumishi na madiwani watatakiwa kwenda huko" alisema Meya Jacob

Hata hivyo akimkaribisha DC Polepole alisema " karibu sana Wilaya ya Ubungo ...mimi bado sijasema niende au nibaki wapi, nasubiri busara iniongoze hivyo tuko pamoja maana wote ni wamoja ila nikija huko ni kwa ajili yako jiandae"

NAYE DC Polepole akiwasalimia madiwani wa manispaa ya Kinondoni alisema kuwa angetamani Wilaya ya Ubungo iwe ya tofauti katika uongozi wake endapo kila kiongozi na mtumishi atafaa kazi kwa maendeleo ya nchi.

"Mh rais amenichagua nije katika wilaya mpya ya ubungo na nitoke msoma vijijini kwa malengo na kazi ile ile ya wakuu wote wa wilaya ya ulinzi na usalama wa wilaya husika lakini pia kwa ajili ya dhamana ya kusimamia sera na ustawi wa maendeleo hivyo tufanye shughuli zetu kwa amani"

" Kwa wanaonifahamu vizuri mie ni mwanaccm kweli kweli na siyo wa bahati mbaya, lakini naheshimu demokrasia ya ustawi wa vyama vingi na kufanya kazi na watu wengi kwani si mara ya kwanza kufanya kazi na viongozi wa upi nani ....nimefanyanao bila kuvunjiana heshima" alisema Polepole

DC Pole pole alisema kwamba anategemea siasa ya maendeleo katika wilaya hiyo na siyo siasa ya madaraka kwa kuwa msingi mkubwa wa kuwapo viongozi na watumishi ni maendeleo kwa eneo husika.
MBUNGE wa Kinondoni Maulid Mtulia (CUF)alimshukuru DC Polepole kwa elimu hiyo na kumuahidi kwamba kama ataweka mbele maslahi nchi basi watashirikiana naye bila migongano yoyote baina yao na yeye, watumishi na serikali kuu

"Nafikiri tuendelee na kazi ya kutafanya siasa ya maendeleo ili baadae tupate siasa ya madaraka ... ili mkiwa mnaitengeneza Ubungo ya tofauti, siye kinondoni tubaki na kinondoni ya pekee"
Safi sana Mh. Meya pamoja na Mh. Polepole kwa kuonyesha mfano wa siasa bora.
 
Back
Top Bottom