Meya Arusha kususiwa kama Kikwete bungeni

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
CHAMA cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), kimetanzaga kususia vikao vyote vya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Arusha, hadi hapo uchaguzi wa Meya na naibu wake utakaporudiwa.

Msimamo huo, ulilotolewa juzi usiku na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusu mgogoro uliotokana na uchaguzi wa viongozi hao.

Mbowe ambaye amekuwa Arusha, kwa takriban siku tatu sasa, akikutana na madiwani wa chama hicho na wadau wengine wa siasa katika jitihada za kuzuia vurugu, alisema chama hicho hakijaridhishwa na uchaguzi wa meya na naibu wake.

"Hapa naomba ieleweke kuwa Chadema haigombanii kushinda bali tunataka taratibu,sheria na kanuni zihesimiwe na hii ni kwa mustakabali wa taifa letu,"alisema Mbowe.

Alisema sambamba na kususia uchaguzi, Chadema pia inaitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomii Chang'aa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya Arusha, Zuberi Mwombeji, kwa kusababisha vurugu zisizo za lazima.

"Hawa ni chanzo cha vurugu si tu tangu wakati wa uchaguzi mkuu, lakini pia hadi sasa. Tunaomba hatua zichukuliwe dhidi yao,"alisema Mbowe.

Kwa upande wake, Mbunge wa Arusha, Godless Lema, alisema kama Changaa na mkuu huyo wa polisi wasiopoondolewa ifikapo Januari 5 mwakani, watafanya maandamano makubwa ya kuwapinga.

Lema alisema sambamba na maandamano watalifikisha suala hilo katika kikao kijacho cha Bunge kwa kuwataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Seikali za Mitaa), George Mkuchika kutoa maelezo.

"Viongozi hao kwa kutumia na chama tawala wamekuwa wakivuruga amani ya Arusha na hili tutalifikisha mbali,"alisema Lema.

Awali wakili Abert Msando alisema taratibu za kwenda mahakamani kupinga uchaguzi wa meya na naibu, zinaendelea na zikikamilika watafikisha suala hilo mahakamani.

Uchaguzi wa Meya na Naibu wa jiji la Arusha umekubwa na utata mkubwa baada ya madiwani wa CCM na diwani mmoja wa TLP kushiriki, wakati chadema ikienguliwa kutokana na kupinga mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga, Mary Chatanda kujumuishwa katika madiwani wa CCM.
 
Back
Top Bottom