Herbert Nkuluzi
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,857
- 3,050
Kufunga bao ukiwa mdogo ndo rekodi inayokufanya uwe GOAT? [emoji23][emoji23][emoji23]Wewe una matatizo makubwa si haba..., Brazil alikuwa kwenye Peak kwa kuchukua vikombe ndio na wale wote ambao alikuwa anacheza nao hawakuwa vibonde, kwa nafasi zao ambao pia alikutana nao kwenye ligi za nyumbani na bado Santos kufanya mambo....
Unasema Pele hakufanya nini ? Kafuatilia 1958 alifanya nini; 62 alicheza game mbili sababu walijua kinara ni nani na katika mbili moja alifunga; kafuatilia 1966 kwanini Brazil hata haikuvuka makundi na Pele alifanywa nini ?, Kafuatilia 1970 alivyorudi alifanya nini hizo ni world cup za kufuatana..., alafu kacheki Messi amecheza World Cup ngapi na amefanya nini na hizo world cup alikuwa na kina nani (yaani benchi la argentina tu ungeweza kuzipa timu za Afrika na hata kuwakopa England strikers kadhaa) na bado chenji ikabaki kina Saviola, Tevez, De Maria; Juan Riqueleme wote ni Wa-Argentina ujue...
Tafuta historia ya Kombe la dunia 1958 na 1970 google tu wala usihofu; Maradona 1986 alifanya mambo sawa ila ilichangiwa na Games kuwa televised world wide hence watu wengi kuangalia na kwa kuwafunga England na Media zao hence more promotion.... bila kusahau Hand of God na kwamba Diego ni a Character (machachari)
Again kabla ya kujibu fanya research ni kwamba 1958 kina Pele kwanza akiwa African, na pili Bwana mdogo game mbili za mwanzo hakucheza Kocha akawa-convinced na kocha mwingine game linalofuata aanze na kina Pele (yaani hatua za makundi) Pele alivyingia game ya tatu / Sio Robo !!! Game ya Tatu akatoa pande la goli, Mechi iliyofuata akafunga only goal yaani in short bila Pele hata makundi wasingetoboa.... kwahio kwa point yako hapo juu inaonyesha hata Data hauna na ungekuwa nazo huenda tusingepotezeana muda mpaka sasa
Aisee againa fanya research alicheza mechi ya kwanza na kufunga bao na kuwa-incenerate Mexico hio ni 1962 baada ya 1958 kufanya mambo na timu walivyoona hivyo kiatu kikatembezwa mechi ya pili akaumizwa sasa asichukue kombe lile goli dhidi ya Mexico ulifunga wewe ? kuna watu wanachukua Kombe hawajafunga game hata moja au utasema De Maria asipewe medali wakati ni kazi yake nzuri ndio ilifanya Argentina mpaka half time wawe mbele ?
Rudia kufuata History 1966 Pele bado alikuwa kwenye Peak na kwa timu kujua hilo Bulgaria na Portugal walimpiga kiatu hadi akashindwa kuendelea game la pili na bila hivyo Brazil wangechukua hii ndoo tena na Pele angekuwa na ndoo nne...
Individual Brilliance ? Fuatilia what happened 1958, 1966 na 1970..., au ni wewe ndio ulikuwa kijana mdogo kuliko wote mpaka sasa kufunga bao Kombe la Dunia ? Yaani Sweden walikuwa kwao na Ubaguzi wao walishindwa hadi kuanza kumshabikia Pele ingawa ni Timu Pinzani..., Yaani hadi King akashuka na kumpa mkono..., kuwa kwake Global Brand hadi Cosmos wakambembeleza aende kutangaza Soccer; Bila yeye huenda Joao Havelenge asingekuwa Fifa President na mpaka leo Europe ingekuwa na Timu zote sisi huku mabara mengine tuna timu za kuokoteleza...
Dogo acha kuleta masihara....
Yani mnazunguka sana washabiki wa ronaldo hadi huruma.Okay kama unataka kuangalia hivyo its your prelogative...
Lakini ukiangalia mechi zote La-Liga alizocheza Messi na Mechi Zote za La-Liga walizocheza wengine wote; Messi ana ratio .91 anafungana na mdau mwingine ila ni watatu yeye na huyo mdau kuna wengine wanampita..., na mmoja kati ya hao wamecheza wote....
Kwahio kama huyu kule mtoni hakufanya vizuri kama huku kwenye swimming pool arguably unaweza kusema mtoni ni pagumu kuogelea (ingawa sisemi hivyo bali ninakuonyesha ukiwa rahisi wa kuchukua stats bila upembuzi yakinifu unaweza ukapata picha ambayo haina uhalisia)
Nadhani kajifunze kusoma kwanza naona nitakesha kama niliyoandika hapo juu hata huelewi.. (ila sichoki taendelea kutoa elimu, kama mimi navyojifunza sababu elimu haina mwisho; ingwa wewe naona hutaki hata kuelewa bali unatumia hoja za nguvu na sio nguvu za hoja )Kufunga bao ukiwa mdogo ndo rekodi inayokufanya uwe GOAT? [emoji23][emoji23][emoji23]
Nimepotezea hoja zako nyingine maana nimeona hakuna hoja zaidi ya ileile ya kiatu wakati hakuna rekodi ya Pele kupigwa kiatu kuliko wengine hata kwenye mechi moja tu maana rekodi ya kupigwa kiatu anayo Maradona sasa huyo pele alichezewa rafu ngapi ndugu yangu!?
Mwaka 1970 CUBILLA alichezewa rafu nyingi zaidi ya mchezaji yeyote huyo Pele rekodi yake iko wapi kama yeye ndo unajifichia eti alipigwa viatu vingi zaidi?
Kama mambo ya Stats ngoja nikupe chache ambazo mimi wala sitaki kuzitumia kama nilivyosema Football is a Game of Opinions (wala sitaki kwenda huko) ninaongelea facts:- ; Yaani mkuu hata kutokujua achievements za Pele na Alichoweza kusaidia Football kuwa a Global Most Loved Game nachelea kupata wasiwasi na ufuatiliaji wako wa Soka...Mimi nahitaji unioneshe kipi ambacho Pele anamzidi Messi la sivyo tutabaki na MESSI as a GOAT
La Liga Pure League timu zote sawa, ligi sio kuongezea ligi za mbuzi n.k.
Naam na ungesoma Post ya mwanzo ndio maana nimeleta hii Post; Hii Post ni ya kuchuja Pumba na Mchele; yaani kupunguza kuondoa achievements za mwingine ili ku-justify mambo mengine kwahio kama mchambuzi wa Mpira uangalie vitu kwa jicho la kichambuzi
Na sio kushinda tu world cup bali umefanya nini katika hio world cup Pele was a Piooneer, Yaani Pele was among the People who Made Football the Beautiful Game Pele identified na watu masikini wa Brazil na watu Weusi dunia nzima..., What Pele achieved kwa kijana wa leo kuja kusema ligi ilikuwa ya wavuta sigara na mijamaa ambayo haina talent kwakweli ni kuleta masihara na kudharau achievements za watu....
Kwamba ligi Bora Duniani zipo Ulaya huenda hii ni kwa sasa lakini kipindi vinara wote / wengi wanacheza ligi za nyumbani logically timu bora ya kipindi hicho means zilikuwepo huko ambapo timu ya taifa ilikuwa more talented....
Na kwa ku-confirm hilo ni kwamba Santos ilishinda Kombe la Timu za Ulaya na South America mara mbili (Intercontinental Cup) pamoja na Intercontinental Supercup ambayo ilijumuisha washindi wote wa nyuma wa Intercontinental Cup na Brazil akamfunga Inter Milan nyumbani kwao Italy San Siro
Wanaosema Pele alibebwa ni kweli alibebwa na wenzake baada ya kuona mchango wake; kuanzia kijana mdogo makaka zake wali-appreciate mchango wake, yaani pamoja kuwa na ma-born leaders kwenye timu ila wali-appreciate mchango wa Pele kwenye timu....
Tofauti na Messi ingawa ni mchezaji mzuri lakini kumfanya yeye kuwa Leader ni kosa kubwa..., Messi sio kina Roy Keane, Messi sio Grafter Messi sio Vocal huenda Argentina ingekuwa na kiongozi ambae ni vocal na kumuacha Messi acheze tu bila kumbebesha mzigo ambao hauwezi ingeshinda Kombe la dunia zaidi hata lile la 2014
Natural Born Leader kwenye Timu wasingefungwa na Saudi Arabia wala kupoteza lead mara kadhaa wakiwa wameshinda bao mbili bila... When things are falling apart you need a leader (Both in and out of pitch)
Mashabiki wa Ronaldo wamekimbilia kwa Pele[emoji23][emoji23].
Kitu pekee ambacho Messi alikua anakwama kwa Pele ni Worldcup tu ila kila kitu Pele kazidiwa na Messi mbali sana.
Messi ndo GOAT kwa sasa uyo pele hata Ronaldo kamkalisha
Naunga mkono hojaMjadala ufungwe, Messi ndio the G.O.A.T akifuatiwa na Maradona.. Moderator futeni huu uzi..
REST IN PEACE the Eternal KING....
The Man who helped in Promoting the Beautiful Game
Has been the Living Legend..., We Shall Never See his Like Again..., Now his Walk Has Ended....
Acha ujinga wewe kimafanikio tu mesi hamkuti Pele jamaa kaiwezesha Brazil kuchukua kombe la Dunia mara 3 Tena kombe la kwanza amechukua akiwa na umri mdogo Zaid miaka 17 tu pale Sweden 1958 afu unasema huyo mesi wako ni Bora acha ujingaMessi ni mchezaji bora kuliko wote hata pele mwenyewe
Pele alikuwa bora kwenye ufungaji tu tena mpira wa zamani haukuwa na offside
Messi anavyo vyote
Mkuu nakubaliana nawe umeongea kisoka zaidPele anabaki kushindana na Maradona japo Pele anabaki kuwa mkali wa muda wote.
Mess anabaki kushindana na CR7 wao Wana daraja lao ila Zidane na Gaucho awa nawaweka kwenye daraja lao peke Yao,
Wao Si tu walikua wakicheza mpira ila waliufanya mpira kuwa Sanaa ya ajabu kabisa.