Royal Warrior
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 1,166
- 2,143
========
LIONEL Messi akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Barcelona katika ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Real Madrid katika mchezo mkali wa ligi ya La Liga uliochezwa usiku huu huko Santiago Bernabeu.
Real Madrid ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya kiungo wako Casemiro kufunga bao akimalizia mpira na Sergio Ramos uliogonga mwamba na kumkuta mfungaji.
Lionel Messi aliisawazishia bao hilo Barcelona dakika chache baadae baada ya kuwalamba chenga walinzi wawili wa Real Madrid na kufyatua mkwaju uliopita chini ya mikono ya kipa,Keylor Navas na kutinga wavuni.
Ivan Rakitic aliifungia Barcelona bao la pili kwa mkwaju wa mbali kabla ya mtokea benchi James Rodriguez kuifungia Real Madrid bao la kusawazisha.
Mchezo ukiwa unaelekea ukingoni Lionel Messi aliifungia Barcelona bao la tatu na la ushindi akiunganisha pasi ya mlinzi Jordi Alba aliyekuwa amegongeana vyema na kiungo Mreno,Andre Gomes.
Ushindi huo umeipeleka Barcelona kileleni baada ya kufikisha pointi 75 sawa na Real Madrid yenye mchezo mmoja.Barcelona ina mabao mengi ya kufunga.
Aidha katika mchezo huo Real Madrid ililazimika kumaliza ikiwa na wachezaji kumi (10) baada ya nahodha wake Sergio Ramos kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kosa la kumkwatua Lionel Messi aliyekuwa mwiba mkali.