Men's Fashion: DOs and DONTs

Roger Sterling

JF-Expert Member
May 10, 2015
13,012
23,613
Drop your expertise, and help another brother get his style and grace together in this fashionable world we live in.

DOs

..Vaa viatu visafi kila mara. Attention unayovipa viatu vyako inaelezea unavyojithamini.

..Vaa nguo zinazokutosha sawia. Sio za kubana sana, wala zisiwe kubwa mno.

..Oga na jali usafi bro. Usafi ni afya.

DONTs

..Usichomekee kamwe kama mkanda haufanani na rangi ya kiatu chako.

..Usivae suti na huna usafiri, hata wa kukodi. Utachoreka tu.

..Usijichubue kamwe.

Karibuni.
 
DON'T...ever think just because you paid a grip, you will look cool in them. Understand your body structure.

cgmhzx6u1jptgtuhnzwp.jpg
 
Drop your expertise, and help another brother get his style and grace together in this fashionable world we live in.

DOs

..Vaa viatu visafi kila mara. Attention unayovipa viatu vyako inaelezea unavyojithamini.

..Vaa nguo zinazokutosha sawia. Sio za kubana sana, wala zisiwe kubwa mno.

..Oga na jali usafi bro. Usafi ni afya.

DONTs

..Usichomekee kamwe kama mkanda haufanani na rangi ya kiatu chako.

..Usivae suti na huna usafiri, hata wa kukodi. Utachoreka tu.

..Usijichubue kamwe.

Karibuni.

Duh, wazee wa kumiliki mkanda mmoja noma.
 
DOs
..Vaa nguo zinazokutosha sawia. Sio za kubana sana, wala zisiwe kubwa mno..
Aisee, kumeibuka tabia siku hizi ya kuvaa nguo za kubana! Sijui imesababishwa na nini?!? Wachezaji wa NBA walikuwa hawana tabia za kuvaa nguo za kubana na matisheti kama ya kike. Lakini siku hizi wakiongozwa na Westbrook ndiyo imekuwa fasheni.
Ni afadhali mwanaume avae loose clothes haswa jeans na pants kuliko kuvaa za kumbana na kumchoresha mwili.

Ndiyo maana mimi nikiwa nanunua jeans uwa napendelea straight au regular. Hizo slim nawaachia wazungu! Nikiona mtu mweusi ndani ya slim, nafsi yangu inasononeka.
 
Ndiyo maana mimi nikiwa nanunua jeans uwa napendelea straight au regular. Hizo slim nawaachia wazungu! Nikiona mtu mweusi ndani ya slim, nafsi yangu inasononeka.

Skinny jeans ndo ziko in vogue sasa hivi....hahahaaa.

Sijawahi kuona, kwa mfano tu, Balmain jeans za kiume zilizo loose fit.
 
Skinny jeans ndo ziko in vogue sasa hivi....hahahaaa.

Sijawahi kuona, kwa mfano tu, Balmain jeans za kiume zilizo loose fit.
Hizo wacha zinipite tu...mimi siyo mtu trendy...bado navaa kama mtu wa late 1990s na early to late 2000s. Nitatupia jeans langu la Levi's, Old Navy ama Wrangler ni yote hayo ni lazima yawe straight or regular na siyo loose sana.

Nikivaa skinny jeans naona kama najichoresha. Yaani mwanaume mzima unabana makalio ili iweje!
 
Back
Top Bottom