Meno yananiuma sana, naomba msaada

dokolombwike

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
373
615
Habar ya asubuhi wandugu;

Nina tatizo la meno, meno yangu yananisumbua sana,yaani yanauma kimwendokasi. Kama leo sijalala kabisa.Tatizo ni meno ya mbele yameoza na ndio yanayouma. Wasiwasi wangu nikiyatoa nitakosa reception.

Naomba ushauri wa dawa ya kutumia bila kuyatoa, pia kama kuna sehemu wanatoa huduma ya kuweka ya bandia lakini yawe meupe sio kama yale ya akina Birdman ningependa kufahamishwa.

Natanguliza shukrani
 
Jjaman mbona mnapita kimyakimya.ningeandika jinsi ya kumfikisha mwanamke kileleni ungeona macoment kibao.shikamoo tanzania.
 
Wagonjwa matozi wanashida sana....anyway waswahili wanasema dawa ya jino ni kuling'oa.Kuhusu housing yako usiogope kuna ya bandia na yanapendeza tu kinywani tena weza amua wakupe hata ya dhahabu.Acha uoga nenda kang'oe meno hayo utaendelea kua mcharo tu.
 
Pole sana. Najua maumivu ya meno kwa sababu siku moja ilinibidi nikeshe na kesho yake nikaenda kuling'oa jino. But before hujafikia huko, chukua majivu ya jiko la mkaa changanye na maji kidogo uweke mdomoni. Mengine uwe unapigia mswaki, asubuhi na jioni. Hii itasaidia kupunguza acid kwenye meno yako, na huenda ikayaongezea uhai.
 
Habar ya asubuhi wandugu,nna tatizo la meno,meno yangu yananisumbua sana,yaan yanauma kimwendokasimwendokasi,yaan kama leo cjalala kabisa.tatizo ni meno ya mbele yameoza na ndo yanayouma,waswas wangu nikiyatoa ntakosa reception,naomba ushaur wa dawa ya kutumia bila kuyatoa, pia kama kunasehem wanatoa huduma ya kuweka ya bandia lakin yawe meupe sio kama yale ya akina birdmen.natanguliza shukrani

Tumia dawa ya meno inayoitwa sensodyne itasaidia sana..achana na haya Colgate yaliyojaa sukari yanajaza bakteria tu kwenye meno
 
Back
Top Bottom