Meningitis (Uvimbe wa Ubungo) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meningitis (Uvimbe wa Ubungo)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Feb 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Meningitis


  Meningitis ni uvimbi wa bongo.[SUP][1][/SUP] Kuvimba huku kunasababishwa na virusi, au bakteria au hata pia kutumia dawa fulani. Meningitis ni maradhi yanayoweza kuuwa kwa ajili ya kuwa uvimbe huu hufanyika karibu na bongo; kwa hivyo ugonjwa huu ni dharura umwone daktari.Dalili kuu za ugonjwa huu ni kuumwa na kichwa na shingo, pamoja na homa na kuchanganyikiwa kwa akili, kutapika na kutoweza kustahamili mwangaza na kelele.


  Kichwa kuuma sana Dalili

  • Kutokuwa na akili timamu, hii hutokea kwa takriban asilimia 44 ya wagonjwa.[SUP][2][/SUP]
  • Kutoweza kustahamili mwangaza na kelele.
  • Uvimbe juu ya kichwa hufanyika kwa watoto wa umri wa chini ya miezi sita.
  • Dalili zingine zinazopatikana kwa watoto ni kuumwa kwa miguu, kuhisi baridi kali na ngozi kugeuka rangi.[SUP][3][/SUP]
  [​IMG]
  Picha ya Mgonjwa mahututi wa Meningitis


  Sababu

  Kwa watoto wenye umri wa chini ya miezi mitatu, ugonjwa huu husababishwa na group B streptococcus. Wengine ambao hukaa kwenye matumbo ya binadamu ni kama Escherichia coli

  Virusi


  Virusi vinavyosababisha Meningitis ni kama enterovirus, herpes simplex virus type 2, varicella zoster virus, herpes zoster, mumps, HIV, naLymphocytic choriomeningitis.
  Meningitis pia huweza kusababishwa na kuenea kwa saratani hadi kwenye ubongo.[SUP][4][/SUP]


  Kukinga

  Meningitis hukingwa kwa kutumia chanjo. Katika nchi nyingi, watoto wengi hupewa chanjo ya kuzuia Haemophilus influenzae ambayo huondoa bakteria hawa kwa miili ya watoto. Hata hivyo, chanjo hii ni ghali.
  Chanjo ya Bacillus Calmette-Guérin imeonyesha kupunguza kiwango cha ugonjwa huu kuenea.
  Dawa zinazotumika kuzuia ni kama rifampicin, ciprofloxacin au ceftriaxone.

   
 2. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maningitis sio uvimbe wa ubongo. Bali ni ineflamation ya ngozi nyembamba 2 inazozunguka ubongo. Kati ya ngozi hizi panakuweko maji maji ambayo muumba aliweka kama cussion ili unapo pata blow to the head iweze kuwa absorbed hapo. Inflamation hiyo yaweza kuwa bacterial eg Nisseria Maningococus na watoto hata E. Colii, au yaweza kuwa mechanical after a svere blow to the headTiba huwa acording to cause.Diagnosis: Neck stiffness, loss of concentration, fever, reddning of eyes na kwenye lumber puncture utapata cause. Kwa kufanya Grams Stain na proteins na glucoseKwa waathika chief couse ni cripto coccus.
   
Loading...