Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
IEBC inasema kuwa mtu huyo alionekana mara ya mwisho siku ya Ijumaa jioni.
Mawasiliano ya mwisho kutoka kwa mtu huyo aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alfajiri kupitia ujumbe wa sms na mmoja wa wafanyakazi wenzake.
Aliyoyaandika kwenye ujumbe huo yalionyesha kuwa alikuwa akijielewa na alikuwa na mipango ya siku.
Ripoti tayari imepelekwa kwa polisi huku IEBC, familia yake na pia polisi wakishirikiana kujaribu kubaini aliko.
Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.
Chanzo: BBC