Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi amesema Serikali imegharamia na kuisadia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kusaini mkataba na Mkandarasi ambaye ni kampuni ya China Harbour Engineering ( CHEC) kwa ajili ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao kwa thamani ya shilingi bilioni 434.5.
Nyathi ameeleza hayo leo Aprili 04, 2025 wakati wa kongamano maalumu la miaka minne ya uongozi Rais Samia Suluhu Hassan, lililofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu mkoani Mtwara.
Amesema ujenzi wa bandari hiyo tayari umeanza kutekelezwa na mkandarasi yupo saiti, pia mradi huo utakapokamilika unatatajiwa kuwa kichecheo kikubwa cha uchumi wa ushoroba wa kusini hususani katika usafirishaji wa madini.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Bandari ya Kisiwa Mgao inajengwa Mtwara Vijijini na ni maalumu kwa ajili ya kusafirishia mizigo michafu kama makaa ya mawe, sulphur na saruji.
Aidha, Nyathi amesema Serikali imefanya upanuzi wa Bandari ya Mtwara kwenye maeneo ya gati, miundombinu ya barabara, mizani pamoja na mifumo ya TEHAMA
Pia Serikali ya awamu ya sita imegharamia ujenzi wa gati jipya kwa shilingi bilioni 157.8 ambalo lipo Bandari ya Mtwara, vifaa vya zaidi ya shilingi bilioni 100 na ununuzi wa boti ya kisasa kwa zaidi ya shilingi bilioni 20.