beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Habari zisizo na shaka zinaeleza kuwa Meneja Ardhi wa Mgodi wa Acacia North Mara, Bwana Peter Enger amekamatwa tangu juzi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime kufuatia kampuni hiyo kushindwa kuwalipa wananchi fidia kwa miaka mitatu.
Inaelezwa kuwa uamuzi wa kutaka meneja huyo akamatwe ni suluhisho la kujua hatma ya fidia ya wananchi.
Zaidi ya wakazi 1,000 kutoka katika vitongoji Nyamichele, Muryambai na vijiji vya Kewanja, Matongo, Kerende, Nyakunguru, na nyamwaga wanadai fidia za mali zao yakiwamo mazao na nyuma ambapo juzi waliandamana mpaka kwenye mgodi huo wakishinikiza kusikilizwa kwa malalamiko yao.
Luoga alisema kuwa aliagiza meneja huyo akamatwe na kupelekwa Kituo cha Polisi Musoma baada ya kufika mgodini hapo kutuliza ghasia hizo.
Awali malipo ya fidia za wananchi yalichelewa kwa kudaiwa kuwapo majina hewa ya wananchi ambapo serikali iliingilia kati lakini bado hadi leo hawajalipwa. Mkuu huyo wa Wilaya aliuagiza uongozi wa mgodi kuwalipa fidia wale wote ambao majina yao hayana utata.
Wananchi hao walisema mbele ya kiongozi wa wilaya kuwa mgodi huo umewafanya washindwe kulima mashamba yao yaliyochukuliwa na kufanyiwa tathmini kwa ajili ya malipo tangu miaka mitatu iliyopita.