Member stonetown bado yu mgonjwa

AljuniorTz

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2009
Posts
544
Reaction score
19
Kwenu Nyote

Nawajulisha ya kuwa MwanaJamii mwenzetu anaejulikana kwa jina la Stone Town, yupo Dar es Salaam kwa matibabu zaidi ktk hospital ya kijeshi Lugalo; ule mguu aliofanya upasuaji mdogo wa paja, bado unamfanyia tabu. Uvimbe umerudi tena, na pale aliposhonwa panamletea maumivu makali sana.

Jana niliwasiliana nae akanieleza kuwa amepewa dawa za kutumia kwa muda wa siku 3, then ataenda kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya siku hizo 3.

Anatuomba tumuombee dua ili apone kwa haraka ili arudi katika shughuli zake za kila siku za kujitafutia rizki.

Nimewasilisha.
 
Twamtakia ugua pole
kama atahitaji msaada wa kupungziwa damu nipo tayari kujitolea maana najua upasuaji unaendana na upunguaji wa damu.
NIMEPIMA maana naona mshaanza kutoa macho
 
Twamtakia ugua pole
kama atahitaji msaada wa kupungziwa damu nipo tayari kujitolea maana najua upasuaji unaendana na upunguaji wa damu.
NIMEPIMA maana naona mshaanza kutoa macho

Bado haijathibitishwa na Daktari kwamba atahitajika kuongezewa damu; km patahitajika DONEE ya damu tutajulishwa humu jamvini.
 
Twamuombea apone haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.
 

Naona maombi ya members God kayasikia.......Stone town nimemwona anazunguka zunguka hapa Jamvini for now yup kule kny utambulisho wa Masumbo.....Karibu mkuu!
 
Mkuu Stone...., Mwenyenzi Mungu akujalie upone haraka...... Pole sana na maumivu na duaa zetu zipo nawe na wauguzi wako!!
 
Kama anasimu tupatie wengine twajuana naye yakhe!
 
Ugua Pole StoneTown, M.Mungu akujalie neema upone. Amina!

SteveD.
 
Nilionana naye jana, nimeshampa pole zangu moja kwa moja
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…