Membe,ulifikiri kabla ya kusema?

Membe,ulifikiri kabla ya kusema?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Sijui viongozi wa CCM na Serikali kimewapata kitu gani.Kuna kauli zisizo na nauli.Kauli zimejaa kiburi na jeuri. Kauli zisizojaa hata kwenye bakuli. Hazieleweki.Hakibebeki.Haziambiliki. Mimi sijadili kauli ya Mwenyekiti wetu aliyoitoa Dodoma.Najadili kauli ya mmoja wa Mawaziri wa nchi hii na aliyehojiwa Dodoma kama mmoja wa 'waharibu chama. Waziri Benard Camilius Membe.

Unataka kujua kauli yenyewe? Utaiamini? Utaamini kama ameisema Waziri Membe? Ni kwamba, Waziri Membe alikitaka chama tawala-CCM kimteue mgombea wa Urais wake hadi ifikikapo Disemba mwaka huu. Yaani,uteuzi wa mgombea ufanyike kabla ya kuisha mwaka huu. Aisee!? Kauli hii kaitoa yeye.Imeripotiwa na baadhi ya magazeti leo hii (kama sikosei Mwananchi).

CCM sasa inataka kuvuka mipaka.Mipaka hadi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jaji Damian Lubuva. Tume ya Uchaguzi ndiyo yenye dhamana ya kutangaza tarehe za kuanza mchakazo wa kiuchaguzi: kuchukua fomu,kuteuliwa na kadhalika. Si mwingine. Waziri Membe halijui jambo hili? Kauli yake inaonesha kujisahau au dharau. Si kauli nzuri.

Sasa chama kinayumba. Wanaohojiwa ndio wanaotoa kauli zilizo kinyume na Sheria na Taratibu za Uchaguzi. Nani aaminike chamani? Shime viongozi wangu,muwe na uchaguzi wa maneno kabla ya uchaguzi wa viongozi kichama na kiserikali!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
He is just another nut.case!

Kumjadili ni kujilisha upepo tu.
Kama uliwahi sikiliza mahojiano yake ITV yale ya dk 45 utanielewa.
 
nimefurahishwa na hoja ya bkm iko poa lazima ccm ijitofautishe na socalled wahafidhina wa chadema kulinda hadhi ya chama na urais,urais sio jambo la kushtukiza wawaruhusu kuweka mambo peupe
 
Le mutuz at ahojiwe lini? Lukosi naye ametangaza kugombea Urais lini ataitwa ?
 
Viongoz wa ccm ni majanga, yaan kaul wanazotoa viongoz wate wa ccm ukiizitafakar kwa umakin hata mtoto wa chekechea hawez kuongea utumbo,
Watanzania wenzangu sasa tufike mwisho tuseme ccm bac tena,

Hili lichama limetufanya tuwe maskin wa kutupwa, viongez wa ccm ndo wakubwa kwa kuhubir udin na uvunjivu wa aman huku wakisingizia wapinzan,

Nemeshanga sn kama kaul ya amir jesh, yy kaangalia upande mmoja tu mbona bomu la arusha hakutoa kauli yeyote?

Nafikir hapo ukiitafakar kwa umakin kaul za viongiz wetu kila mtanzania anatakiwa ajilinde mwenye, na huko tunapoelekea nchi hii itaingia kwenyr machafuko, mpaka ikifika 2015 tutaona matendo mengi sn kwa kauli hz za viongoz!!
 
Huyu membe hana lolote atuambie zile hela za simbo ziko wapi ndo tutamuelewa.hii mijitu ni mijizi tuuu
 
vuta nikuvute huna jipya. umebaki msukule usio na mbele wala nyuma
 
wahafidhina vs wapenda demokrasia

cc.
zitto,kitila,slaa,mbowe.
 
Mzee Tupa Tupa,ndani ya CCM wenye busara na akili hamna wakapinga upuuzi na kauli za hovyo za wakubwa wenu??!! Hata kushauri pia ngumu??!!

Nini maoni na tathimini yako ya Kauli ya Raisi rahisi na Mwenyekiti wenu wa Chama kinachojinadigi kuhubiri amani,umathubutu na utaifa??!!
 
Kwani chama kikimtangaza mtu wake wanayetegemea atagombania uraisi kabla ya muda wa uchaguzi ambao utatangazwa na Tume kuna kosa gani hapo? Chama kumtangaza mtu wake kuna taratibu zake ambazo sidhani kama zinaingiliana na taratibu za tume ya uchaguzi ambazo zinazuia tu mtu kuanza kampeni kabla ya tarehe rasmi waliyoipanga!
 
Hujui ulisemalo.Kisheria haitakuwa halali

Mzee Tupatupa
 
Mzee Tupa Tupa,ndani ya CCM wenye busara na akili hamna wakapinga upuuzi na kauli za hovyo za wakubwa wenu??!! Hata kushauri pia ngumu??!!

Nini maoni na tathimini yako ya Kauli ya Raisi rahisi na Mwenyekiti wenu wa Chama kinachojinadigi kuhubiri amani,umathubutu na utaifa??!!
Mwenyekiti amenukuliwa vibaya.Hata mkuu Mungi anajua. Hakusema hivyo

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Ni kwamba, Waziri Membe alikitaka chama tawala-CCM kimteue mgombea wa Urais wake hadi ifikikapo Disemba mwaka huu. Yaani,uteuzi wa mgombea ufanyike kabla ya kuisha mwaka huu. Aisee!? Kauli hii kaitoa yeye.Imeripotiwa na baadhi ya magazeti leo hii (kama sikosei Mwananchi).

Mkuu, kitendo cha Membe kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu ya CCM kimemchanganya sana. Anatapatapa ovyo sasa hivi. Anachofanya Membe ni kujaribu kupunguza uelewevu wa watu kuelewa sababu zao za kuhojiwa, kutaka kuonyehsa hawajaitwa kwa kuwa wana makosa. Membe anataka kuonyesha kwamba waliitwa na Kamati ya Nidhamu si kwa ajili ya masuala ya nidhamu bali kwa ajili ya kutoa ushauri kwa Kamati ya Nidhamu! Hata anadiriki kusema "eti wameomba ushauri wa jinsi ya kumaliza makundi ndani ya CCM!!!!"

Ha, ha ha! Budesi budesi budesi! Yaani kamati ya Nidhamu imemwita kumhoji Membe ili aishauri juu ya kumaliza Makundi ndani ya CCM!!!

Membe, kuna watu tuna akili tupo tu tunabangaiza maisha, japo sisi sio Mawaziri kama wewe.

In fact, kwa kauli hizi za Membe mojawapo kati ya haya mawili ni kweli; CCM imefilisika kimawazo au Membe kafilisika kimawazo.
 
CCM wameshajikubali kushindwa lakini sasa wanakuja na slogans mpya, wanasema "ccm imechoka lakini upinzani hauko tayari". Na wanajikubali kuwa wao ni 'zimwi' kitu ambacho ni kweli lakini wanatumia kinyume chake kuwa bora zimwi likujualo.
Kinachonisikitisha ni uchaguzi uliopita wa madiwani, sijui hao waliowapa kura wanawaza nini maana inaonyesha kutokuwa wazi kwa walio wengi huku shida zikiongezeka.
 
CCM bado ina nguvu vijijini. Mjini hawana chao, CCM imechokwa kiasi kwamba watu wanapigiana kura Chama na sio Mtu. Membe atachanganyikiwa akiukosa uRais
 
Kweli urais umekua kama ubalozi wa nyumba kumi,hadi membe nae anautaka kirahisirahisi hivyo.rais ajae ni lowasa yeye asipoteze muda wake.
 
Back
Top Bottom