William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
swali liko palepale je balozi ambazo hazipati waombaji wa visa wa kutosha zinajiendeshaje?Manake Mkuu umetaja hizo nchi giant na naweza kukubali kuwa zinaleta wataalii wengi bongo sasa je zile balozi ambazo ziko kwa 'wachovu' au wasiopenda kufanya utalii tanzania vipi huko nako wanaishi kwa hela ya visa?
- Mkuu nchi nilizozitaja nimewahi kuishi na kama kawa very close na watu wa hizo ofisi, ndio maana ninafahamu vyema jinsi system zetu za balozi financially zinavyofanya kazi, maofisa wanaweza kosa mishahara, lakini sio the locals au bills za ofisi ni lazima zilipwe ontime na wakati mwingi hutegemea hela za viza kunapokosekana hela toka serikalini.
- Pia nimewahi kuishi katika nchi za ki-Africa pia, kama Zambia, Burundi, Rwanda, Kenya na zaire sikuwahi kusikia kwamba ofisi za balozi zina matatizo ya hela hata siku moja, matatizo ya hela mara kwa mara huwa ni kwa balozi zetu za West.
Kaka makusanyo ya visa yanatofautiana nchi na nchi. Siamini kama Brussles kuna flow ya wageni kiasi cha kuweza kuwezesha kukusanya kiasi cha kutosha kwa matumizi kama hayo. Wengi wanaoingia na KLM ni wa connctions kutoka US/CANADA/germany/Nordic/Scandnavian countries ambazo kuna balozi tofauti. Vilevile kama sijakosea mapato yote huwa yanaingizwa kwenye account halafu kupelekwa Hazina. Hazina ndio wanaotoa fedha/idhini za matumizi kufuatana na bajeti.
kuna mtu ananiuma sikio kwamba si kwamba umeishi bali kuna mtu wako ubaloizini hapo ambaye nadhani ni jamaa yako wa karibu sana usibishe tusije mtaja jina hapa maana jf bwana ,ndiyo anakupa hizi habari na namna balozi ziendavyo , maana kama umekaa us miaka kibao ni wazi kwamba walio kuwa katika nchi hizi walisha ondoka labda ubaki kuwasiliana nao na kuuliza lakini kubali na wenzako mwanavyo sema ukweli wa leo hii si wa jana
Mzee ES nimesha shuhudi wageni wengi sana wana chukulia VISA hapa hapa Dar .Kuna shida ya Balozi ama ofisi za balozi kukaa majumbani mwa wa watu.Kwa mgano kule Holland jamaa mzungu ni rafiki yake JK for the last 14yrs wanajuana na hata JK akipita pale lazima wanaitana na wanadanya shopping wote , leo ofisi yake iko porini hjata Public transport ni shida hadi uchukue taxi.Wa Dutch they got no time for that wanachukulia airport Dar wanamaliza fitina .Unasemaje ?
Mkuu Lunyungu,
- Wewe tunaheshimiana kwa hiyo nitakujibu, uliyosema hapa ni kweli 100% na kama unakumbuka hii ishu niliwahi kuisukuma mbele kwa wakuu wakapata kigugumizi kwa sababu ya ushikaji wa huyo mkulu na muungwana, sawa sawa kabisa,
ila tu uliyosema hayana anything to do na ubalozi wetu Brussels kukosa heat, tena wakati huu wa winter, najua for a fact kwamba Brussels tunao ubalozi kamili, maana mimi nilipokuwa pale Karume ndiye alikuwa full balozi.
Masahihisho mkuu .
Kwa data tu nilizo nazo ni kwamba Ubelgiji inaweza kuwa inaleta wageni wengi wa kiserikali na mashirika ya Umma Serikalini lakini kwa Utalii mkuu Ujerumani na Holland ndizo hasa .Wabelgiji hawaijui Tanzania vilivyo na hili ndilo naweza kukupinga bila kuzunguka .Nina data za kutosha .
Again mkuu mimi na wewe tuna heshimiana sana na hata kupingana kwangu mimi na wewe ni kwa hoja mkuu .
Nadhani hili ni suala zaidi la kiutawala wa ndani ya ubalozi wenyewe. Kama wanashindwa ku keep up na bills za gas kazi kweli kweli....
Barafu yamkimbiza ofisini balozi wa Tanzania Ubelgiji
Mwananchi newspaper
Leon Bahati
BALOZI wa Tanzania nchini Ubelgiji, Simon Mlay, amesimamisha shughuli za ubalozi tangu Desemba 5, mwaka huu kutokana na baridi kali katika ofisi za ubalozi huo.
Taarifa iliyopatikana katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeeleza kuwa huduma pekee ambazo zitaendelea kutolewa na ofisi hiyo iliyopo mjini Brussels, ni za viza.
Hali hii imeelezwa kuwa imetokana na mtambo wa kupasha joto kwenye ubalozi huo kuharibika vibaya na sasa serikali imeamua kununua mwingine.
Juhudi za kuuweka mwingine nazo zimeshindikana kutokana na mafundi wengi nchini Ubelgiji kuwa kwenye mapumziko ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
"Hiki ni kipindi cha baridi, ubalozi umelazimika kufunga shughuli zake hadi hapo mtambo huo utakapofungwa na kuanza kufanya kazi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ikibainisha kuwa, uwezekano wa ofisi kurejesha huduma zake kikamilifu ni Januari 20, mwakani.
Ilielezwa kuwa tayari serikali imetuma fedha za manunuzi ya mtambo huo wa kuongeza joto na taratibu za kupata mwingine zimekamilika.
sasa hii si fedheha! hata hivyo ni bora balozi ameamua kusitisha shughuli kuliko kuwalazimisha watendaji wapige mzigo kwenye baridi kali na hivyo kuhatarisha maisha yao.
Taarifa iliyopatikana katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeeleza kuwa huduma pekee ambazo zitaendelea kutolewa na ofisi hiyo iliyopo mjini Brussels, ni za viza.
Es umeona kwamba visa hazitoshi kuendesha ubalozi na kwamba si kweli Ubelgiji wanaongoza kwa watalii ?
Kila siku wako Ulaya na America; inaelekea wakiwa huko hawafiki ubalozini wanaishia mahotelini tu na ndio maana wakina Karamagi wanasign mikataba nje ya ubalozi!! Inaelekea hawa wanamtandao na Seikali yao kila mtu kivyakevyake tu; hawana common vision.Lumbanga si ndio yuko huko Brussels, inakuwaje balozi yupo lakini ubalozi unakosa central heating system? Mrudisheni aje ajibu maswali ya EPA .
Nadhani hii ibadilishwe na itwe "KIMULIKA BALOZI ZETU"
Tanzanianjema