Membe, Lowassa na Sitta wanaigawa CCM

Membe, Lowassa na Sitta wanaigawa CCM

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
408
Salamu wanajamvi.

Membe,sitta na Lowasa wamekuwa wakitumia misikiti na makanisa kutoa harambee ili uchaguzi wa 2015 waje kuungwa mkono maana kila mmoja anania ya kugombea nafasi ya juu kabisa ya taifa hili.

Nasema wataligawa taifa kwa misingi ya kidini,iwapo kati ya mmoja atashinda kiti cha urais japo sina uhakika na imani na yeyote.Kuna kundi fulani litaibuka na kuhoji mwenendo wa mgombea kabla ya kuwa rais,huu ni mwendelezo wa yaleyale ya mwaka 2010 kwa Jk kutoa ahadi ya kuruhusu mahakama ya kadhi wakati katiba ya nchi hairuhusu matokeo yake ndio haya ya udini nk.

Hawa watu wataligawa taifa kwa misingi ya dini,kuna kundi litaibuka na kunena juu ya mshindi mmojawapo kati ya hawa either of the two between muslims or christians. Ni mwendelezo ule ule wa makundi katika chama katika misingi ya dini,kibaya zaidi haya ni makundi yanayokinzana..najua kila moja litamtupia mwenzake lawama au kashifa yoyote ili kummaliza kisiasa.

Taifa hili,limekuwa ni familia/kupeana vyeo kwa misingi ya urafiki,kila mtu anafanya analotaka as if hakuna katiba ya nchi.Iwapo kati ya Membe/ Lowasa/Sitta atakuwa rais taifa hili hakika linaingia katika hali mbaya zaidi ya hali ilivyo sasa.

Nawaomba watz wenzangu wenye mapenzi mema na taifa hili watu hawa ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu,japo hadi sasa amani hakuna ila kuna utulivu na uoga,tusiwaunge mkono kwenye mkono hata kidogo.
 
Kama Membe amewasaliti wamakonde wenzake, Je atatuthamini sisi watanganyika? Sitta ni mroho wa madaraka tena mwenye siasa za chuki. Nakumbuka Mke wake alipokamatwa anatoa rushwa, badala ya kuachia mahakama itoe hukumu, alitamka maneno ya jeuri wa vyombo vya sheria.

Sitta hana mapenzi na Tanzania, baada ya kuporwa Uspika wa Bunge lililokuwa na msisimko, uroho wake wa madaraka aliamua kubaki kuwa waziri wa EA. Mh Lowasa ni jemedari aliyeweka maslahi ya nchi mbele, kwa kujiuzuru kuinusuru serikali ya CCM. Kama serikali ingekwenda chini, Tanzania tungeingia gharama kubwa kusimamisha uchaguzi mwingine, pesa ambazo zinasaidia kuleta maendeleo
 
Na hakuna tatizo kwa CCM kugawanyika why not? CCM lazima igawanyike sana. katika hao kuna ambao ni typical magaidi wa kupandikiza mabomu makanisani na kwenye mihadhara. katika hao kuna ambao ni mafisadi wa ktupwa.

Katika hao kuna wenye ka chembe ka CCM the coservative ile ya kina nyerere. wee huoni chimbuko la mgawanyko wa nguvu hapo? CCM MAGAIDI, CCM MAFISADI NA CCM UTU. Lazima mnykano hadi kieleweke.
 
Sijui kama wote wanatoa michango misikitini, ila kanisani!... Najua "Luwasa" analaumiwa kuwa alitoa msikitini kidogo wk hiyo hiyo akatoa kingi msingi.
 
Hawa CCM MAJANGILI/MAFISADI wanaweza kuungana na CCM MAGAIDI kuwa kitu kimoja CCM OVU. Hawa watapambana na CCM ADILIFU na uwezekano ni kusambaratisha chama.

Hii CCM ADILIFU ndiyo kwa mbali inaweza kupambana na CDM na kubwagwa maana ni wachache sana. Ni bora ikajiengua na kuridhiana na MAKAMANDA. Jambo ambalo nawaapia likoJIKONI.
 
hawa ccm majangili/mafisadi wanaweza kuungana na ccm magaidi kuwa kitu kimoja ccm ovu. Hawa watapambana na ccm adilifu na uwezekano ni kusambaratisha chama.

Hii ccm adilifu ndiyo kwa mbali inaweza kupambana na cdm na kubwagwa maana ni wachache sana. Ni bora ikajiengua na kuridhiana na makamanda. Jambo ambalo nawaapia likojikoni.

hakuna uadilifu uliopata kutawala mahali popote duniani, na Wala kesho haijapata kuwa heri kuliko leo. NI kufukuzia upepo tuuu ambao haukamatiki
 
Kama Membe amewasaliti wamakonde wenzake, Je atatuthamini sisi watanganyika? Sitta ni mroho wa madaraka tena mwenye siasa za chuki. Nakumbuka Mke wake alipokamatwa anatoa rushwa, badala ya kuachia mahakama itoe hukumu, alitamka maneno ya jeuri wa vyombo vya sheria.

Sitta hana mapenzi na Tanzania, baada ya kuporwa Uspika wa Bunge lililokuwa na msisimko, uroho wake wa madaraka aliamua kubaki kuwa waziri wa EA. Mh Lowasa ni jemedari aliyeweka maslahi ya nchi mbele, kwa kujiuzuru kuinusuru serikali ya CCM. Kama serikali ingekwenda chini, Tanzania tungeingia gharama kubwa kusimamisha uchaguzi mwingine, pesa ambazo zinasaidia kuleta maendeleo.WEWE NI MCHOCHEZI SOMA MADA UELEWE
 
Duh kuna mtu kasema 15% ya 46 tanzanians arw Ccm.
Kama hivyo ndivyo basi ccm itatawala kwa miaka mingine 50 ijayo. Kidumu chama cha mapinduzi
 
Kwanza hapo sioni udini wowote ambao unauongelea.

Pili mi sioni wataligawaje taifa kwa wao kutaka nafasi ya urais.!

Tatu kuutaka urais ni haki ya kila mtanzania. Hata wewe unayo hiyo haki kama ukiamua

Kama hawafai sema kwa nini hawafai
 
Duh kuna mtu kasema 15% ya 46 tanzanians arw Ccm.
Kama hivyo ndivyo basi ccm itatawala kwa miaka mingine 50 ijayo. Kidumu chama cha mapinduzi

Kidumu mpaka kipasuke ili vilivyojificha ndani tuvione wote.
 
Ni kweli hawa wote ni watu wa chuki na visasi, havifai!
 
We ndugu, hujui kuwa vita ya panzi ni furaha ya kunguru. Acha wanyukane ili sisi tupate napasi. Kwani inchi lazima itawaliwe na CCM?
 
Salamu wanajamvi.

Membe,sitta na Lowasa wamekuwa wakitumia misikiti na makanisa kutoa harambee ili uchaguzi wa 2015 waje kuungwa mkono maana kila mmoja anania ya kugombea nafasi ya juu kabisa ya taifa hili.

Nasema wataligawa taifa kwa misingi ya kidini,iwapo kati ya mmoja atashinda kiti cha urais japo sina uhakika na imani na yeyote.Kuna kundi fulani litaibuka na kuhoji mwenendo wa mgombea kabla ya kuwa rais,huu ni mwendelezo wa yaleyale ya mwaka 2010 kwa Jk kutoa ahadi ya kuruhusu mahakama ya kadhi wakati katiba ya nchi hairuhusu matokeo yake ndio haya ya udini nk.

Hawa watu wataligawa taifa kwa misingi ya dini,kuna kundi litaibuka na kunena juu ya mshindi mmojawapo kati ya hawa either of the two between muslims or christians. Ni mwendelezo ule ule wa makundi katika chama katika misingi ya dini,kibaya zaidi haya ni makundi yanayokinzana..najua kila moja litamtupia mwenzake lawama au kashifa yoyote ili kummaliza kisiasa.

Taifa hili,limekuwa ni familia/kupeana vyeo kwa misingi ya urafiki,kila mtu anafanya analotaka as if hakuna katiba ya nchi.Iwapo kati ya Membe/ Lowasa/Sitta atakuwa rais taifa hili hakika linaingia katika hali mbaya zaidi ya hali ilivyo sasa.

Nawaomba watz wenzangu wenye mapenzi mema na taifa hili watu hawa ni hatari sana kwa amani ya nchi yetu,japo hadi sasa amani hakuna ila kuna utulivu na uoga,tusiwaunge mkono kwenye mkono hata kidogo.

hawaligawi taifa, kwani ccm imeshakufa siku nyingi mazishi 2015, au unapokea cheki wilayani kama mwalimu fulani kumbe upo kitaa!!! Usiogope kutafuta shughuli halali kisa ccm imekufa...au hujapata mtaji kwa pesa unazozitoa bank kwa jina la kapuni?
 
Kati ya hao lowassa ndo jemedari wa kweli hao wengine sijui membe akaongoze familia ya kikwete msata atakapostafu au ya mama salma tena uzuri wote wanatoka lindi akawe kiongozi wa familia ya mama salma
 
Back
Top Bottom