MENGELENI KWETU
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 9,557
- 24,180
Kiuhalisia, watu wengi wamekuwa wanamkubali Lowassa kutokana na Nchi ilipofikishwa sasa, na kwamba ili basi tuweze ku-move toka hapana twende mbele tulipo tunahitaji kweli kiongozi ambae ni IMARA na MADHUBUTI. Nilikuwa nasoma mahojiano ya Tibaigana former Dar RPC na gazeti la Mwananchi, anakwambia TZ ya sasa tunahitaji Rais dikteta kidogo ingawa katika ufafanuzi wake akasema hamaanishi dikteta kwa maana ya dikteta bali Rais ambae ni mkali kidogo ili tuweze kutoka hapa tulipo.
Sasa ukitazama wote wanaojitangaza na wanaotajwa-tajwa hakuna ambae anamfikia Lowassa hata kwa ukaribu. Lowassa sio mtu wa kuyumbishwa katika jambo lolote lile, pia ni mtu ambae ni mwepesi kwenye kuchukua maamuzi. Watz tumefikishwa hapa kutokana na mambo mengine kukosa tu kuchukua uamuzi wa mara moja, Lowassa sio mwoga na Lowassa ni mfuatiliaji wa jambo lolote lile analoliagiza au kulitolea uamuzi.
Tuwe wakweli, katika wote waliojitangaza mtu pekee ambae angeweza kuubadili upepo ni Magufuli ambae kwake Urais hana habari nao. Lakini kwa hawa ambao tumewasikia hakuna kama kama Lowassa na ndio maana basi kila team za wagombea wengine wanatapatapa.