muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
Tumezoea kwenye chaguzi mbalimbali vyama vinatumia mbinu mbinu tofauti kudhoofisha vyama vingine, au kutokea picha flani kama la kihindi ambalo linatoa taharuki kwa wapiga kura wasiwe na msimamo wampigie kura nani.
Uchaguzi mkuu wa 2015, tuliona taharuki kubwa pale ambapo mwanaharakati Slaa ambaye alijijengea jina kwa kipindi kirefu, akiwa anajua ni yeye ndiye atagombea urais kwa tiketi ya ukawa, lakini bila kutarajiwa likaibuka picha la kihindi ambapo Waziri Mkuu mstaafu Lowasa baada ya kukatwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm....alitangaza kuhama chama hicho ambapo alipokelewa kwa bashasha na ukawa na kumpa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Baada ya kutangazwa tu, pakatokea sintofahamu huku ccm ikaanza hamahama ya kumfuata lowasa chadema, lakini na chadema hapakuachwa salama Dk Slaa nae alikasirika kwa nini kachinjiwa baharini dakika za mwisho naye akatafsiri kama kakatwa hivi kugombea urais, na yeye akahamia ccm na baadae baada ya uchaguzi kapewa wadhifa wa kuwa balozi nchini Sweden.
Baada ya uchaguzi kupita Lowasa alivumlia miaka kama miwili na nusu tu, hamu ikamjia ya kurudi nyumbani kwake ki siasa, alirudi CCM, sasa ametulia kama sio yeye vile.
Na sasa kuelekea uchaguzi, jasusi Membe anaonekana ni mtu ambae ana nia ya kuchukua fomu kushindana ndani ya cha cha ccm na Rais wa sasa Dk. Pombe Magufuli, ingawa sio rasmi, kuna kauli mbiu zimeshaanza kusambaa wakati wake utakuwa ni wa "bata na Kazi" na sio "hapa kazi tu", kuna mambo mengi yanayoonesha kuna picha la kihindi linakuja, inawezekana linatayarishwa au limeshaisha bado kuzindua tu.
Sasa hapo vyama ndivyo vitakavyoamua "kuzika au kusafirisha" @ Mwanafa, hapo ndipo tutajua picha linalokuja starring atakufa wakati gani, au atabadirishwa juu kwa juu, uchaguzi uliopita ulikuja msemo wa kubadili gia angani, wakati huu utaibuka msemo gani.........si tuendelee tu kusikilizia ila siasa haikimbiliki.......tusikubali akili ndogo iongoze akili kubwa........Nchi itauzwa yote hii......mi nishawaambia