Happy nation
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 679
- 597
mimi namuunga mkono membe hajakosea mnyonge mnyongeni haki yake mpeni dada zetu na kaka zetu wamekwama ulaya wanashindwa kuja kujenga nchi huku
Umeanza vizuri lakini hapo mwisho umeharibu, hamna sababu ya kukashifu. wewe eleza faida ambazo taifa litapata kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili ambazo haziwezi kupatikana kwenye mazingira ya sasa.Namuunga mkono. Sioni hasara walizopata mataifa yaliyokubali uraia wa nchi mbili kwa muda mrefu tu sasa, na wale wote mnaopinga hamtoi mifano halisi ya jinsi nchi hizo zimeingia matatizoni kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili, pamoja na nchi jirani kama Kenya na Uganda.
Unajua kila nikisoma sababu za watu wanaopinga uraia pacha nashikwa na hasira unayopata unapomsikiliza mlevi akiongea pumba. Tatizo letu Watanzania tunapenda kubisha bila kuwa na facts, tunaishia ku-speculate tu. Hivi mnafikiri kutorosha mali kwenda nje ya za nchi ni rahisi kiasi hicho, kama watu wanavyofanya madawa ya kulevya?
Mnatoa hadithi za vijiweni huko mnataka ndio uwe msimamo wa serikali. Sijui kukosa uzalendo, sijui tukipigana vita watakuwa upande gani, ooh sijui watatorosha mali na siri za nchi. Hamna lolote la maana mnaongea, pumba tupu kama vile tu ni mjadala unafanyika kwenye shule ya chekechea. au klabu ya ulanzi, kayoga, mbeke, kangara, wanzuki, pyuwa, mataptap, nk. Kama ligi ni kubwa kukuzidi kaa kando acha wenye kelewa mambo waicheze kuliko kuleta hadithi za vijiweni kuhusu uraia pacha.
Mantiki ya bwana Membe haieleweki, ikiwa anpita humu naomba anijibu, wawekezaji hata wasio na asili ya Tanzania wanapewa kipaumbele sasa hawa wenye asili ya Tanzania wanashindwa nini kuja kuwekeza? Sio lazima wapewe uraia ndipo wa nchi 2 ndipo waje, tumewakaribisha watu tofauti hatutashindwa kuwakaribisha hawa waliokua raia wa Tanzania kuwekeza, ikizingatiwa kuwa wana hata familia zao huku. SIO LAZIMA WAPATE URAIA WA NCHI 2 NDIPO WAWEKEZE, NINAVYOFAHAU NI KUWA MAREKANI HAIKUBALI URAIA WA NCHI 2, URAIA WA NCHI 2 UNAONDOA UZALENDO, MNAMKUMBUKA ALBERTO FUJIMORI ALIKUA RAIS WA PERU LAKINI PIA ANA URAIA WA JAPAN? ALIPOHARIBU PERU ALIKIMBILIA KWAO JAPAN, TAFAKARI.
Umeanza vizuri lakini hapo mwisho umeharibu, hamna sababu ya kukashifu. wewe eleza faida ambazo taifa litapata kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili ambazo haziwezi kupatikana kwenye mazingira ya sasa.