Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Habari nyingi zimetapakaa Mkoani Arusha juu ya ujio wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mkoani Arusha . Agenda kubwa iliyoko mitaani na katika Mkoa huu ni yeye kukutana na Wanafunzi wa Vyuo Vikuu bila kujulika sababu hasa ya kukutana nao na malengo yake ni yapi kwa Wanafunzi hao.
Mikakati hii inasemekana kuwa inaratibiwa kwa ukaribu mno na anayesemekana kuwa ni Katibu wa Vyuo Vikuu Ndg. NGUBIAGAI pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha na watu wengine wenye mrengo huo. Hata hivyo vijana Mkoani hapa wamechachamaa hasa juu ya mkakati huo na hasa ikizingatiwa kuwa imekuwa ikifanywa kwa siri mno bila kushirikisha watu wengine Mkoani hapa juu ya ama nia na malengo ya ujio wa mtu huyo.
Huko Mavyuoni nako pamoja na wengi kukiri kutokufahamu ujio huo wamesema hata akija hawadhani kama watakuwa na muda wa kukutana naye na wala hawana utayari huo kwa kuwa hakuna jipya ambalo yeye anaweza kuwaambia. Hata hivyo wengi wamekiri kuwa kutokana na hali ilivyo Membe ajiandae kukutana na zomea zomea katika ziara yake hiyo iliyojaaa usiri wa hali ya juu.Habari zilizoko Mjini ni kwamba Ndg. Lema amezipata habari za ujio wa Waziri huyu na ameanza kuzunguka Vyuoni kwa siri sana akiwashawishi wanafunzi kumwandalia Membe zogo.
Inasemekana kuwa Lema anawaambia Wanafunzi kuwa anashangazwa na utaratibu unaotumika kwa kuwa kama Membe kweli anakuja kuzungumza nao na kama ziara yake ni ya Kiserikali basi hakuna haja ya usiri huo na taratibu za Kiserikali zingefuatwa.
Na kama Membe vile vile ziara yake ni ya Kichama basi hana budi vile vile kufuata taratibu za kichama kuliko njia zinazotumika sasa ambapo imeonekana kuwa anayetumika sana na huyo Ngubiagai hivyo lazma kutakuwa na kitu nyuma ya pazia ambacho kimejificha.
Makamanda komaeni makamanda huyu hakuna chochote kinachomleta zaidi ya kujinadi na kujiandalia mazingira msimpe nafasi kabisa makamanda. Mi niko nyuma yenu formula ya Uhasibu itumike na kwenu pia manake Makamanda msipokomaa hawa jamaa si wenyewe kabisa.
Alisikika akisema Bwana Lema.Pamoja na kuwa siku, tarehe, na wala muda bado haujajulikana ama kuwekwa wazi ila macho na masikio sasa yameanza kugeuziwa huko na watu wamekaa wakisubiri kwa hamu sana kujua hatma ya yote hayo ..