Meli ya Vitabu Logos Hope

papiso

JF-Expert Member
Dec 1, 2013
391
230
Yapata wiki kadhaa toka meli kubwa ya vitabu kutia nanga katika bandari ya dar es salaam binafsi nafanya kazi huku bandarini nikapata nafasi ya kuitembelea hii meli,
Kwa kweli kuna mengi ya kujifunza kwenye ile meli kwa watu wote.wana shehena kubwa ya vitabu kuanzia kwa mtoto anayeanza kujifunza hadi kwa anayetafuta PHD wanaruhusu kusoma palepale vilevile vinauzwa kwa bei nafuu kabisa,kitu kingine nilichokikuta pale ni kwamba wale staff ambao wengi ni wazungu ni wakarimu sana unaweza kubadilishana nao mawazo wapo vizuri sana sometimes wanakufata wenyewe mpate kuongea mawili matatu kuhusu kazi zao na kadhalika kiingilio ni bure fanya uende utafaidi sana wapo mpaka tarehe 18 ya mwezi huu
 
Nadhani kuna kiingilio 1000 getini bandarini.
Vitabu ni vya aina gani? Nikiangalia kwenye mitandao naona vingi ni vya kikristu/biblia nadhani ni shirika na kikristu linaendesha hii kitu, kuna vitabu vya technical/non-fiction umeviona?
 
Nilipita kila kona sjaona vitabu vya mapenzi ila vingine vipo vya kila aina
 
Nilipita kila kona sjaona vitabu vya mapenzi ila vingine vipo vya kila aina
Duh, kwamba Shigongo akipeleka nakala zake za vitabu vya malavi lavi hawatapokea. Niliwahi enda miaka ile ilipokuja mara ya kwanza, sikuona cha maana zaidi ya maiskrimu na con, kipindi hicho azam hajaanza kutengeneza.
 
Basi we huna shauku ya elimu, mi ilivyokuja mara ya kwanza ambayo ni MV Doulous nilivutiwa na vingi na nilikuwa na wakati mgumu wa kuchagua kipi cha kununua maana nilipenda vitu vingi sana, kuanzia vitabu, CDs na michezo mbali mbali. Hizo koni hata sikuzitilia maanani
 
Back
Top Bottom