rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,412
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ametangaza upya vita dhidi ya majangili wa nyara za taifa na rasilimali nyingine nchini, huku akiwema wazi mpango wa kufanya doria 100,000 na kukunua ndege mbili katika mwaka ujao wa fedha kwa lengo la kuwakabili maadui hao wa maendeleo.
Waziri Kagasheki amesema licha ya changamoto kubwa ya kusimamia rasilimali za nchi hususan wanyamapori, wizara yake itaimarisha usimamizi na udhibiti kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola pamoja na wananchi.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake bungeni jana Jumanne mjini Dodoma, Waziri huyo alisema suala la doria na udhibiti wa ujangili limekuwa changamoto kubwa na kwamba serikali kupitia wizara yake haitashindwa kuwadhibiti.
"Wizara itaendelea kuimarisha usimamizi wa rasilimali za wanyamapori kwa kuendelea kufanya doria ndani na nje ya mapori ya akiba kwa kuendesha doria - siku 100,000. Miundombinu, vitendea kazi na huduma vitaboreshwa kwa watumishi katika vituo 27 kwenye mapori ya akiba na kanda nane za vikosi dhidi ya ujangili," alisema Waziri Kagasheki.
Alisema biashara ya uvunaji haramu wa mazao ya misitu na nyuki itadhibitiwa zaidi kwa kuongeza doria 20,700 katika maeneo ya nchi kavu na majini pamoja na kudhibiti viwango vya ubora wa mazao ya misitu na nyuki ili kuongeza thamani yake na kuongeza mapato ya nchi.
Kuhusu maboresho ya maeneo ya kufikia watalii alisema wizara yake kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) itajenga nyumba 29 katika hifadhi tisa za Arusha, Katavi, Kilimanjaro, Mikumi, Mkomazi, Ruaha, Rubondo, Serengeti na Udzungwa pamoja na kujenga barabara mpya zenye urefu wa kilomita 115 katika mwaka ujao wa fedha 2013/2014.
"Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itajenga jengo moja la familia sita za wafanyakazi, jengo la mapokezi uwanja wa ndege wa Ndutu, jiko kwenye kambi ya kulala wageni ya Simba A pamoja na nyumba moja ya Askari eneo la Lositete. Mamlaka itaendelea na ujenzi wa jengo la kitega uchumi (kwa ubia) lenye gorofa 10 mjini Arusha,"alisema Waziri Kagasheki ambaye hotuba yake ya bajeti kwa Wizara ya Maliasili na Utalii imechapishwa katika gazeti hili.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Mali Asili na Mazingira, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. James Lembeli, alisema kamati yake imesikitishwa na tatizo kubwa la ujangili wa tembo unaozidi kukua badala ya kupungua.
"Kwa sasa ujangili wa tembo umekuwa ni janga la kitaifa, ni ukweli usiofichika kwamba leo hii si tu tembo wanauawa bali wanateketezwa, kwa mujibu wa tafiti zilizokwishafanywa na taasisi za utafiti wa wanyamapori nchini takwimu zinazoshabihiana na za taarifa za utafiti wa kimataifa zinaonesha kwamba tembo wasiopungua 30 wanauawa kwa siku, 850 kwa mwezi na tembo 10,000 kila mwaka,"alisema Bw. Lembeli.
Wakati huo huo, Siasa zenye dalili za kuchafuana kwa malengo ya kisiasa zimeibuka bungeni na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana, akijikuta katikati ya siasa hizo, kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kusimama na kulitaka Bunge kuepuka kuhusishwa na uongo.
Ni kama vile ulikuwa mpambano kati ya wabunge wa CHADEMA wakiongozwa na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa na wabunge wa CCM, wakiongozwa na Waziri Dk. Nchimbi ambako mivutano ya hoja zilizomhusisha Kinana bungeni huku Spika wa Bunge, Anne Makinda aliamua kuweka kuachia kwa muda kila upande ukamilishe mashambulizi dhidi ya upande mwingine na kisha upande ulioshambuliwa ujibu mapigo.
Katika kuacha mashambulizi na kujibu mapigo kuchukue nafasi yake, Spika alisikika akisema; "Nyingi (wapinzani) mlivyokuwa mkizungumza (kuporomosha mashambulizi) wenzenu walinyamaza wakiwasilikiza."
Katika hoja zake, Msigwa alidai Kinana anahusika katika biashara haramu ya pembe za ndovu akigusia tukio la mwaka 2009 ambako shehena ya pembe za ndovu zenye uzito wa tani 4 kutoka Tanzania na Kenya ziliripotiwa kukamatwa na vyombo vya usalama vya Vietnam akiitaja kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf Shipping Co. Ltd inayomilikiwa na familia ya Kinana.
Waziri Nchimbi alianza kwa kueleza namna Wizara ya Maliasili na Utalii inavyofanya jitihada kutimiza majukumu yake na kwa sababu Waziri kivuli, Mchungaji Peter Msigwa alidai hakuna cha maana kilichofanyika, Nchimbi alisema anaamini mtu wa namna hiyo (aina ya Msigwa) upeo wake wa uelewa una utata mkubwa na baadae kufafanua tuhuma dhidi ya Kinana.
Nchimbi alisema wahusika walikwisha kufikishwa mahakamani na kwamba Msigwa na viongozi wenzake wa upinzani wanafahamu tofauti kati ya kampuni ya Uwakala wa Meli (Shipping Argent) na Kampuni ya Kupeleka na Kuingiza Mizigo (Clearing and Forwading Co. Ltd).
Pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu kutaka kumzuia Nchimbi kujibu tuhuma, Spika Anne Makinda alipuuza na kumtaka Nchimbi kuendelea kuzungumza akisema; "wakati Msigwa anatoa tuhuma dhidi ya Kinana na makada wengine wa CCM, aliachwa ahitimishe tuhuma zake bila kuingiliwa."
Nchimbi aliwataja waliokamatwa na kufunguliwa kesi ni pamoja na Ladislaus Tesha, Gabriel Chambo, Shaaban Yasin, Erick Leo (anayedaiwa kuwa Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato eneo la Bandari ya Dar es Salaam), Issa Ahmed, Norbert Kiwale na Aboubakar Omar Hassan.
Nchimbi alilieleza Bunge ya kuwa kesi dhidi ya watuhumiwa hao ilifunguliwa katika Mahakama ya Kisutu lakini ilisimamishwa kwa muda ili kupata ushahidi kutoka nchi ya Vietnam na kwamba Vietnam ilikataa kutoa ushahidi kwa maelezo kuwa haina mkataba na Tanzania katika ushirikiano dhidi ya makosa ya jinai lakini kumekuwa na jitihada za kupata kibali cha mpito cha mkataba huo kutoka China ili kupata ushahidi na kesi hiyo iweze kuendelea katika Mahakama ya Kisutu