MEI MOSI SHEREHE ZA TISHETI, MAANDAMANO NA MABANGO.
Sherehe za Tshirt husherekewa Duniani kote Tarehe Moja ya Mwezi wa Tano. Pamoja na mambo mengine yawezekana hazijatumika vizuri kuenzi wafanyakazi waliopigania haki na kusababisha kuhasisiwa kwa maadhimisho haya. Kwetu Tanzania maziona kama sherehe za Tshirt, Maandamano na Mabango Yenye Ujumbe Mbalimbali lakini hazijawa na maana yoyote hasa kadiri ya siku zinavyosogea mbele.
Wafanyakazi wa Tanzania wanayo matatizo mengi ukiachilia uwepo wa maslahi duni, mazingira duni, na ukosefu wa haki. MIMI BINAFSI NILITAMANI TU TAREHE 1 MEI kwa HAPA KWETU INGEENDELEA KUWA SIKU YA KAZI, watu tukapiga kazi na kuendeleza kauli mbiu yetu ya "Hapa Kazi Tu". Wafanyakazi tumegeuka mabango ya matishirt na ujumbe mbalimbali usioleta tija na kuondoa matatizo, zaidi ya kutuanika juani na mabango yetu.
Hii yote inatokana na kuwa na viongozi ambao mimi naona kwa mtazamo wangu wamekosa ubunifu na uwezo wa kuwaongoza wenzao katika kupigania maslahi bora. Haiwezekani ikihitajika haki mpaka wafanyakazi wafikia kugoma wakati Vyama vipo na watu wanalipa ada kila mwezi ziweze kuendesha vyama hivi. TUCTA pamoja na vyama vingine vyote vilivyo chini yake, I am sorry to say vimejenga tu jina Vyama Vya Wafanyakazi. Lakini Sijaona kama vinayo matendo ya kazi inayofanana na Trade Unionism.
Naorodhesha changamoto chache tu na ndogo ambazo Trade Unionism sidhani hata kama wanazijua au kama wanazijua basi hawajui hata kuzitatua au basi wamefungwa macho na fikra zao ili wasione.
1. Tunalo tatizo la kodi kubwa kwa wafanyakazi. Hivi TUCTA au vyama vingine mmewahi kuangalia au kufanya ulinganifu na kuona Mtu mwenye mshahara kiasi fulani na mfanyabiashara ambaye anaingiza kipata kinacholingana na mfanyakazi wanatofautiana vipi katika kodi. Kwanini kusiwepo na ulinganifu wa Kodi. Chukua kodi ya Biashara inayoingiza milioni moja kwa mwezi ilinganishe na mfanyakazi anayeingiza milioni moja kwa mwezi. (PAYEE ni Mzigo Mkubwa.
2. Sasa hivi limkuja swala la makato ya marejesho ya fedha za Bodi ya Mikopo. Hatukatai au kuzuia watu kurejesha. Lakini je lina uhalali wa kupandisha makato form 8% to 15% na kubadilisha makato kwa watu ambao mikataba yao ya ukopeshaji walikubaliana kurejesha asilimia nane.
3. Ukitoka kwenye PAYEE kuna utitiri mwingine wa kodi na makato. Hela iliyokatwa kodi ya PAYEE inaenda tena kulipa VAT kwenye withdraw charges, Hiyo hiyo inaenda kwenye VAT katika manunuzi na huduma zingine.
4. Kuna swala la FAO la kujitoa halieleweki bado lina wasiwasi, nina haja gani ya kuvaa mabango na kubeba mabango na kupigwa jua ati ni MEI MOSI wakati in reality ni MWE MOSHI. Moshi unafuka baada ya wafanyakazi kuunguzwa na matatizo na changamoto lukuki.
BORA NIVAE TISHIRT YANGU YA SIMBA, NIMETOKEA KUZICHUKIA TRADE UNION KWANI ZIPO KUKUSANYA MAKATO KWA WAFANYAKAZI