Mechi za CC na NEC, Kikwete ajipigia pasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mechi za CC na NEC, Kikwete ajipigia pasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Nov 24, 2011.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Akiwa ameshindwa kuiwakilisha hoja ya kujivua gamba katika vikao vya Kamati Kuu na ile Kamati ya Nidhamu ya CCM,Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameamua kuisogeza,pasipo maandishi, hoja hiyo kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayokutana hapa Dodoma.Rais Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa vikao vyote vya kitaifa vya CCM,amejikuta akigeukwa na wasaidizi na washauri wake wakuu na wa karibu kuhusu hoja ya kujivua gamba.Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Wilson Mukama alinukuliwa jana akimnong'oneza Kikwete kuwa kuwatosa magamba ni gharama kubwa kuliko kuwa nao.Alimshauri akae mbali na hoja hiyo kwa kuiacha mikononi mwa wajumbe wa NEC.Wachambuzi wa mambo hapa Dodoma wanatabiri kuwa hoja ya gamba italetwa kama AoB(Mengineyo) na si kama hoja rasmi.Makongoro Nyerere,Mwenyekiti wa CCM Mara,maarufu kama Mzee wa site ameapa kuweka hoja hiyo mezani.Kikao cha NEC kilichoanza jana,kimegawanyika katika makundi mawili:wachukia gamba na wapenda gamba huku wapenda gamba wakiwa na nguvu zaidi.Nilipomdodosa Bashe juu ya gamba,alinijibu kwa kujiamini kuwa Lowassa na Chenge hawagusiki.Mimi ni Vuta-Nkuvute kwa niaba ya JamiiForums-Dodoma.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Kuwavua gamba Lowassa na Chenge tu haiwezekani kwa kuwa chama kimejaa magamba. Ndani ya chama hakuna aliye msafi
   
 3. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  nilishasema humu jk ni mtu muoga sana......hiyo ndiyo imetoka hivyo hawezi kuchukua maamuzi magumu huyu....hana lolote
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  na tena kimeoza mbaya sana..
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Uoga wake kwa kiasi kikubwa unatokana na ukweli kwamba naye ni sehemu ya mfumo uliopelekea kuwapo magamba, au kwa maana nyingine naye ni gamba. Hivyo hawezi kuwanyooshea kidole magamba wenzake kwa kuogopa kuumbuka.
   
 6. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Tuvute subira kikao kiishe tusikie kitakachojili
   
 7. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kuweza kuvua gamba CCM inahitaji timu ya viongozi wa juu walio wasafi kwa maneno na vitendo, wenye ushawishi kwa wanachama na wananchi wa kawaida, na ambao bila ya shaka yeyote hawajaingia madarakani kwa ufedhuli, rushwa au zawadi. Hao wakisema watasikilizwa na wanachama na hata wananchi tulio nje ya CCM tutakubaliana nao. Nachelea kusema, sijaona angalao watu watano wenye sifa hizo. EL ni kama linesman kwenye mechi ya mpira wa miguu, refa haweza kumpa red card mshika kibendera, kitakachotokea kuna mchezaji atatolewa kafara ya red card kwa kumtukana linesman eti hana busara.
   
 8. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  The chairman of 'magamba's' party has no audacity of making hard and prompt decision that'd salvage the situation in his party. He has a syndrome of listening to back-bitter (back-bitters will never enter into a paradise).

  So, his action has always been like someone trying to scr...himself. this is too disgusting.
   
Loading...