MECHI ya YANGA, AZAM YAINGIZA MIL 240/-

MECHI ya YANGA, AZAM YAINGIZA MIL 240/-

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803


SUNDAY, FEBRUARY 24, 2013
[h=1][/h]
​


Mechi namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.



Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.


Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.


Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 6,975,669.36.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


SUNDAY, FEBRUARY 24, 2013 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG
 
Team ya Wananchi utaijua tu......mapato yamezidi hata ya yale yaliyopatikana katika mchezo kati ya team ya Taifa ya Tanzania na Cameroun
 
Team ya Wananchi utaijua tu......mapato yamezidi hata ya yale yaliyopatikana katika mchezo kati ya team ya Taifa ya Tanzania na Cameroun
lakini angalia serekali ilivyojichukulia hapo bila jasho ,aise kweli wajua kuzikomba kwa wavuja jasho.
 
Team ya Wananchi utaijua tu......mapato yamezidi hata ya yale yaliyopatikana katika mchezo kati ya team ya Taifa ya Tanzania na Cameroun

Lazima uipende tu siyo hiyo timu ya waarabu/somali pale Msimbazi.
 
Timu zimeingiza mil.240 alafu mgao mnawapunja mil.58 tu kweli??? Huu unyonyaji
 
mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye uwanja huu uliingiza Sh. 500+million, lakini tangia hapo kiwango hicho hakijawahi kufikiwa tena na uwanja unajaa.
Ndio maana TFF wagombea wengine wanakatwa ili mambo mengine yaendelee kuwa siri ila dalili zinaonyesha kuwa umeanza kugeuzwa shamba nao
 
Back
Top Bottom