Mechi 3 bora za wakati wote!

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,409
6,555
1. Man Utd 4-3 Man City (mwaka 2009.)
_46410778_owen_new_credit.jpg

Wakati Craig Bellamy akiisawazishia Man City dakika ya 90 na kufanya ubao usomeke 3-3 wengi waliamini mechi hiyo ingeisha kwa sare, zikaongezwa dakika 4, City wakarudi nyuma kupaki basi.
Ghafla Michael Owen akaibuka shujaa baada ya kufunga goli la ushindi dk ya 96 nje ya zile 4 za nyongeza. Kocha wa Man City alilalamika sana baada ya Refa kushindwa kumaliza mpira kwa muda sahihi.

2. Liverpool 3-3 Ac Milan (Fainali ya Uefa 2005)
0505250137b.jpg

Fainali hii iliyofanyika Instanbul, Liverpool walikuwa nyuma kwa magoli 3-0 wakati wa mapumziko, kipindi cha pili kinaanza kwa kocha Benitez kumuingiza Dietmar Hamann ambaye alienda kumzuia Pirlo asicheze na kuwafanya Liverpool warudi mchezoni, dk 90 mechi inaisha 3-3 na Liverpool wanaenda kubeba ndoo kwa penati baada ya extra time.
final.jpg

ucl+2005+LFC+vs+Milan.jpg


3. Derpotivo La Coruna 4-0 Ac Milan ( Robo Fainali ya Uefa, April 7, 2004)
270271.jpg

Mabingwa watetezi wa Ulaya, AC Milan wakiwa na advantage ya ushindi wa 4-1 walioupata nyumbani San Siro, walienda kuwafata Derpotivo wakiwa vifua mbele lakini wakakutana na dhahama nzito ya kipigo cha 4-0 toka kwa Derpotivo. Walter pandiani kaibuka staa wa mchezo kwa kutakata na kuwapoteza mastaa wa Milan kama Kaka, Pirlo, Inzaghi na Shevchenko.
Ac Milan wakatolewa kwa jumla ya Magoli 5-4.

Karibu mdau ututajie na wewe mechi zako 3 unazozikubali.
 
Mechi ya AC na Liverpool nikiwa nashabikia AC nikaenda kulala after first half, kwamba kazi imeisha, na kuanza kejeli (as if nina maslahi kama Berlusconi) Nilipoamka asubuhi kupata matokeo, mijicho ilinitoka kwa kutoamini.
 
Germany vs Italy semi final world cup 2006.....
Germany anakufa goli 2 kwa 0 ndani ya dk ya 118 na 120....

Fabio Grosso anafunga bonge la bao baada ya kupokea pande maridhawa kwa el maestro pirlo anangalia kushota anapiga kulia.

Alesandro del piero ana wamalizia wajerumani kwa goli safi baada ya counter attack iliyoanzia kwa canavaro, luca toni, gilardino na kumkuta del piero na kumgalagaza jens lehman. Hapo ndipo ndoto za wajerumani zilipoishia.


Natamani kuwawekea clip yake ila jf apps ni jipu linapokuja suala la ku-upload video
 
Newcastle 4 Arsenal 4 febr 5 2011 Arsenal anatangulia kufunga goli zote 4 akiwapo Van parsie then newcastle wanarudisha yote Tiote akisawazisha
Ungejua ulivyokitonesha kidonda changu kilichokwisha kupona?
Basi tu.
Hata hivyo mechi zilizowahi kuniuma maishani,nililia zaidi ya msiba;zipo 2 tu.
1.France vs Italy 2006 (World Cup Final)Nilikuwa upande wa France
2.Arsenal vs Barcelona (UEFA Final)
Nimesahau mwaka ila nakumbuka Jens Lehman alipewa red card kwa madai ya kumfanyia Samuel Eto'o madhambi.
Kama sio ile red card kombe lilikuwa letu kabisa .
Mechi ile ilinifanya nikamchukia Eto'o na Barcelona hadi leo.
cc BAK
 
Back
Top Bottom