Underdog
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 364
- 483
Amani iwe nanyi!
Nina shahada ya kwanza ya uhandisi wa mitambo toka UDSM na nina uzoefu wa mwaka mmoj katika usimamizi na ukarabati wa engine na mitambo mingine midogo kama generator.Nimekuwa nikijitole katika taasisi moja kwa muda wa mwaka mmoja sasa nikihudumu kama Trainee Maintennce Engineer.
Kama kijana mwingine mwenye ndoto, imefikia wakati ambapo nahitaji kuona taaluma yangu inaniingizia kipato. Hivyo nimeamua kuanza kuzungusha CV nikiamini ya kwamba huu uzoefu wa mwaka mmoja utanisaidia kukabiliana na changamoto zozote za kazi nitakayoipata na mwishowe kuzishinda changamoto zenyewe na kuwa msaada kwa taasisi nitakayokuwa naitumikia. Ningeendelea kujitolea hapa nilipo nikisubiri labda nafasi iitajitokeza lakini kmpuni niliyopo haikui (kulingana na misingi na kazi zake) hivyo ni ngumu kwa nafasi mpya kujitokeza.
Kwa kuamini mipaka ya fikra zangu, upeo wa kuona na idadi ya watu niwajuao, nimeona ni vyema nikaomba msaada wenu utakaoniwezesha kupata kazi ya taaluma yangu. Nipo tayari kutumika sehemu yeyote ille ya dunia hii. Kwa sasa nipo Dar es Salaam.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa msaada wenu.