R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
Mdororo wa uchumi umeaanza kuikumba tanzania baada ya meli kutopiga nanga kwa wiki zaidi 4, baada ya kufanya utafiti na kuulizia ,
meli nyingi zinazofika ni za kijeshi na nyingine zinafika kuchukua au kunywa maji.
Ikizingatiwa msimu wa meli ndo huu baada ya x-mass.
Hii imeiladhimu mamlaka ya bandari kufuta vibarua zaidi ya 700.
Baada ya kufanya utafiti kwenye icd, pia nao wanalalamika hakuna mizigo wanayopokea kutoka bandarini.
Kkoo, wafanya biashara wameshindwa kupata mizigo kwa ajili ya pasaka na kulazimu kuuza old stock.
Pia ata meli za mafuta zimepotea , kutokana na mita kuwa mbovu kama ilivyolipotiwa na gazeti la tanzania daima na kamati ya miundo mbinu iliyokuta mita moja ndo inafanya kazi , nyingine zote mbovu.
Usahuri wangu , faida ya bandari ni kushusha mizigo na kupakia mizigo.
Kama kwa kipindi hiki tunashindwa kupakia na kushusha mizigo ; je kodi itakusanya vipi?????? Kama sio kodi ya kukamua ngombe.
Kwa maana hiyo kenya inapata faida sana kushusha na kupakia mizigo ya tanzania , na mizigo hiyo inaingia kama transit toka mombasa . Kitu ambacho kinatukosesha pesa za kigeni.
Na kama mizigo haingii sokoni ; je kodi inayokusanywa ni hipi.
Ushauri:
1. Serikali ifanye umafia kama awamu ya 4 , ya kuingiza meli za mizigo na mafuta za iran na north korea kwa kuzibadili rangi na kupeperusha bendera yetu . Ingawa usa atakuwa mbongo; lakini ata akiwa mbogo mbona kina jk waliweza.
Nchi hizi zina vikwazo na bidhaa zao ni cheap .
2. Kuongea na wafanya biashara wakubwa waliokuwa wanaleta meli nzima kama azam,mo, nyati, steel, wafanyabiashara wa kichina, gsm, bin sulum na kupata muafaka kwa kutengeneza kamati ya ushuruishi wa pamoja, na kuzika ya awamu ya nne na kufungua awamu ya 5.
3. Kuweka ulinganifu katika kusafirisha mizigo sawa kwa train na barabara; tatizo nalo linaoma matajiri wanataka wakileta mizigo yao wasafirishe kwa magari yao mapaka congo na rwanda , na si reli,
serikali , mizigo ya serikali za congo na rwana , zambia - ndo isafirishwe kwa reli , lakini wafanya biashara waruhusiwe kuchagua njia ya kusafirisha.
Wasiwasi wangu , matajiri wengi wamesajiri magari yao kwa nchi walizowekeza kama kenya , rwanda, congo azam na gsm , wasije kuwa wanatumia hiyo kufuata mizigo mombasa kwa magari yao kwenye inchi walizowekeza na kutukomoa kwenye mapato; ikizingatiwa kenya rushwa hiko juu sana. Wa ki corrupt serikali ya kenya ni rahisi kupitisha mizigo yao.
4. Serikali ikubali kufanya ubia na wafanya biashara watanzania -
mfano ; zile bilioni 900 alizokamata bot jpm, awape wafanya biashara wafungue viwanda 20% wafanyabiashara 80% ni serikali .
Party 2.........Inaendelea
==================
Kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya serikali yanayotokana na kodi mbalimbali kimeshuka kati ya Desemba mwaka jana na mwezi huu.
Itakumbukwa kuwa Novemba mwaka jana, makusanyo ya Mamlaka ya Mapato (TRA) yalipanda kutoka wastani wa Sh. bilioni 800-900 kwa mwezi mpaka Sh. trilioni 1.3.
Kiwango hicho kiliongezeka na kuwa Sh.trilioni 1.4 kwa Desemba kabla ya TRA kukusanya jumla ya Sh. trilioni 1.06 Januari na Sh. trilioni 1.04 mwezi uliopita.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka hiyo, Diana Masalla, aliiambia Nipashe katika mahojiano wiki iliyopita kuwa, TRA imejiwekea lengo la kukusanya Sh. trilioni 1.3 kwa mwezi huu.
“Kwa mwezi wa Machi lengo ni kukusanya Sh.trilioni 1.3, kiasi hiki ni lengo lakini tunaweza kuvuka na kufikia zaidi ya hapo,” alisema Massala.
Wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma Novemba 20, mwaka jana, Rais John Magufuli alisema kwa zaidi ya miaka mitatu ukusanyaji wa mapato ulikuwa chini kwa sababu mbalimbali.
Alisema Serikali ya awamu ya Tano itaongeza nguvu katika upanuzi wa wigo wa kodi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
“Tutahakikisha kwamba kila mtu anayestahili kulipa kodi analipa kodi stahiki. Hatutasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakaye kwepa kulipa kodi," alisema.
"Tunawaomba wananchi mhakikishe mnapewa risiti kila mnaponunua bidhaa au huduma. Kodi ni kitu muhimu lazima kila mtu anayestahili kulipa kodi alipe."
Rais Magufuli pia alieza kuwa, serikali yake itahakikisha kwamba kila senti inayoongezeka katika mapato ya Serikali inaelekezwa katika kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi kwa kuziba mianya ya upotevu wa fedha za Serikali ambayo inaipunguzia Serikali uwezo wake wa kuwahudumia wananchi.
Lakini tangu iweke rekodi ya makusanyo Desemba mwaka jana, TRA imeshindwa kurudi katika kiwango cha makusanyo ya Sh. trilioni 1.4.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema kila mwezi TRA hujiwekea malengo ya kukusanya kodi kiasi fulani, na kwa miezi mitatu iliyopita wameweza kuvuka lengo.
“Kila mwezi una malengo tuliyojiwekea na miezi yote mitatu tumevuka malengo tuliyojiwekea,” alisema Kayombo.
WATAALAM WA UCHUMI WAELEZA SABABU
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dk. Bill Kiwia alieleza sababu zinazoweza kusababisha makusanyo ya kodi kupanda na kushuka kwa serikali au halmashauri.
Alisema serikali inaweza kuwa na makusanyo mengi katika mwezi fulani kutokana na malimbikizo ya kodi kuwa mengi kutoka kwa wafanyabiashara.
Alisema kwa mfano mwezi Desemba, serikali ilikusanya Sh.trilioni 1.4 kwa sababu wafanyabiashara wengi walikuwa wanalipa kodi tofauti na udanganyifu walioufanya miaka ya nyuma.
Alisema makusanyo yanaweza kupungua kutokana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabishara, akitolea mfano, mfanyabiashara anakua na namba mbili hadi tatu za utambulisho wa biashara (TIN).
Alisema endapo serikali inahitaji kukusanya mapato mengi zaidi inapaswa kutoa elimu kwa wananchi ya umuhimu wa kulipa kodi.
“Sera ya ukusanyaji kodi iendane na aina ya biashara, tusije tukawa tunahamasisha ukusanyaji wa kodi huku tukawa tunaua sekta binafsi,” alisema Dk. Kiwia.
Naye Mkuu wa Idara ya Uchumi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Jehovaness Aikaeli alisema kinachosababisha mapato kuongezeka ama kushuka inategemea nguvu au juhudi ya ukusanyaji wa mapato iliyojiwekea serikali kwa mwaka.
Alisema nguvu hiyo ni pamoja na kuziba mianya ya rushwa.
Alisema utofauti wa shughuli za kiuchumi au kibiashara kwa mwezi husika nayo inaweza kusababisha makusanyo ya kodi kupanda au kushuka.
“Kwa mfano mwezi wa kumi na mbili (Desemba), shughuli nyingi za kibiashara zinafanyika, watu wanafunga biashara zao, hivyo lazima makusanyo kwa serikali yatakuwa makubwa,” alisema Dk. Aikaeli.
Aidha, Dk. Aikaeli alisema miezi mingine kama vile Januari, wafanyabishara wengi wanakuwa na shughuli zingine za kiuchumi mbali na kulipa kodi hivyo hata mapato kwa serikali hupungua.
Chanzo: Nipashe