jojipoji koromije
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 1,003
- 1,428
Hakuna siri tena, na wala hakuna pa kujificha ili mwanaharamu apite!! Kulingana na projection za IMF uchumi wa Tanzania unaelekea kaburini; Nchi inafilisika; tena wamesema ifikapo july 2017 nchi itakuwa imefilisika rasmi!!!! Ni hatua za dharula tu ambazo ni muhimu zinazoweza kuboost uchumi wa nchi yetu; lakini kwa kuangalia muda uliosalia na ubabe wa utawala huu kukataa ushauri sioni nafasi ya kuchukua hatua za kuboost uchumi huu unao gasp hivi.
Viashiria vya kufilisika kwa nchi ni vingi na kila mtanzania anaviona, mfano: kudorora kwa sekta binafisi- biashara zinafungwa, makampuni yanapunguza wafanyakazi, makampuni yanashindwa kurejesha mikopo bank, mzunguko wa fedha kupungua sana, mfumuko wa bei wa bidhaa mbalmbali hasahasa chakula kama sembe, maharage, mchele, sukari; hakuna ajira, hakuna nyongeza za mishahara kwa watumishi wala promotion, sera mbovu za uchumi (kuzibania pesa zote BOT) , mabenk yanafilisika Na mengine yanajikongoja, fedha za miradi ya maendeleoa tumeishiwa, huduma za jamii kama afya, Maji Na elimu ziko dhofri hali, taaabani!!! Na indicators zingine nyingi tu.
Ni wakati sasa kiongozi wa nchi akachukua hatua stahiki- kujiuzulu, heri tuanze upya kuliko kuingia gharama za kuirudisha nchi kwenye mstari.
Kinachouma zaidi ni kuwa nchi yetu iko kwenye hatua za kufilisika wakati uchumi wa dunia upo stable. Hii ni hatari sana, Na inaonyesha dhahiri uongozi wa Awamu hii una sera mbovu za uchumi.
July Si mbali kutoka sasa, Kiongozi wa nchi lazima achukue hatua za dharula kutunusuru na aibu na fedheha hii, nchi kufilisika wakati tuna kilakitu!!!! Kweli!!!! Nyerere angelikuwepo asingevumilia hali hii, angerudi Ikulu kushika hatam haraka sana.
Na pia kama tukifilisika kama nchi uongozi wote wa awamu hii ukubali kuwajibika Kwa kuachia ngazi, twende kwenye uchaguzi mpya, haitojalisha watashinda CCM au wapinzani, chamsingi tuanze upya, tukiwa na sera Nzuri za uchumi na utawala utakaofuata katiba, kanuni, sheria na taratibu katika kuongoza nchi.
Utawala utakao wajibika kwa wananchi, utawala utakao kuwa na sifa za kuheshimu kilio cha wanachi, kusikiliza, kuvumiliana na kukubali kukosolewa ambazo ndo hulka za watanzania tangu tupate Uhuru.
Mungu Ibariki Tanzania Na Raia Wake.
Amen.