George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 148
Kwa watanzania wote,
Jumuiya ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), imeandaa mdahalo wa wazi utakaowapa wananchi fursa ya kuutafakari Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwa kuangalia tulikotoka, tulipo na tunakoelekea.
Mdahalo utafanyika katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kampasi ya Mlimani, mnamo tarehe 26.04.2016, siku ya jumatano, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni. Tutakuwa na wachokoza mada wakuu wanne (wawili wanataaluma na wawili wananchi).
Wananchi wote mnakaribishwa. Hakuna kiingilio.
Aidha, kwa wasioweza kuhudhuria kwa sababu mbalimbali, tunapenda kuwataarifu kuwa wanaweza kuufuatilia mdahalo huu mubashara kupitia ITV.
Karibuni sana.
George Kahangwa
Mwenyekiti wa UDASA