Mdahalo: Nani aliyekwamisha Katiba mpya?

Mdahalo: Nani aliyekwamisha Katiba mpya?

Mfumo wetu huu ambao Rais anasikiliza zaidi chama chake kuliko watanzania kwa ujumla wao ni hatari sana. Tukiendelea hivi maendeleo ya kweli na kujikwamua kabisa kutoka makucha ya mabepari wa kimataifa HAIWEZEKANI. Lazima tubadilike haraka sana.
 
Sidhani kama Kikwete ndio chanzo,utakumbuka yeye ndio Rais pekee aliyethubutu na kukubali mchakato wa kupata katiba mpya,sio Nyerere,sio Mwinyi wala Mkapa. Alifungua historia ya kukumbukwa vizazi na vizazi ingawa baada ya kuunda bunge la katiba aliyumbishwa na mitazamo ya mtangulizi wake Mkapa,kilichonishangaza zaidi ni pale alipowahi kusema akili za kuambiwa changanya na za kwako. Yeye alishindwa kabisa kuchukua usahauri aliopewa na Mkapa na kuupima kabla ya kwenda bungeni kufungua rasmi bunge la katiba badala yake akaenda kuzungumzia msimamo wa chama chake cha kuwa na serikali moja bila hata kutamka kuwa amefungua rasmi bunge hilo la katiba.
Sasa aibu imemrudia,mchakato wa kupata katiba mpya uko njia panda. Nia yake ilikuwa njema lakini alishindwa kusimamia mawazo yake mazuri ambayo yangebaki katika historia vizazi na vizazi.
Kiongozi makini hatakiwi kufanya kama alivyofanya JK. Ni dalili ya kutojua ufanyalo na udhaifu mkubwa. Wanasema ni bora kunyamaza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom