AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Haya ni maswali na majibu ambayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Mrisho Gambo aliyatoa leo Jumatatu 22/5/2017 wakati anafanya mdahalo huru na marafiki zake katika mtandao wa Whatssap.
Twende kazi:
Swali langu: Tatizo lilikuwa ni nini mpaka MEYA wa akazuiwa kutoa rambirambi kule LUCKY VINCENT????
Jibu: Meya hakuzuiwa. Serikali ilipata taarifa za kiinteligensia kuhusu mkusanyiko ule na ikachukua hatua stahiki. Mchakato wa kuwapeleka wahusika mahakamani utakamilika baada ya upelelezi kikamilika. Pia ni busara kuacha kufanya siasa kupitia misiba. Watoto wa Lucky Vincent wanahitaji treatment ya kisaikolojia na si purukushani. Mkusanyiko ule ulikuwa kipindi ambacho Serikali ilikuwa inatoa tiba ya kisaikolojia kwa watoto wetu waliobaki.
Swali langu
Napenda kujua mchakato wa kuifanya Arusha kuwa Satellite city,umefikia wapi
JIBU
SASA hivi tunakamilisha Master Plan. Mengine yatafuata baada ya Master Plan kukamilika.
SWALI.
A)Mheshimiwa Gambo hongera sana kwa kazi nzuri unayoifanya. Mimi binafsi nafuatilia tangu ulipokuwa DC koronge. SWALI 1. Unawasaidiaje vijana wewe kama wewe binafsi maana ukiangalia maswala ya vijana sehem nyingi yapo nyuma sana hata ule uwezeshaji wa Vikundi vya vijana aufwati maana watendaji wenye mamlaka ya kutekeleza hilo hawafanyi kama ilivyo elekezwa kuna ukiritimba mnoo na mwisho vijana hawawezeshwi na vijana wengine wanakata tamaa, kumbuka vijana wengi sana waliomaliza vyuo tangu 2008 mpaka sasa hawana ajira rasmi wangependa wasaidiwe. Unalizungumziaje hili sawala?
2. Arusha ni inavivutio vingi sana Mheshiwa na wewe unalijua hilo maana inatoa mchango mkubwa kwa pato la taifa ila watumishi wako wa utaliii hawapo serious maana hawahangaiki na swala la utalii wa ndani ,Je unampango wa kuboresha au kuajiri watu wenye weredi kulingana na jinsi soko linavotaka??
B)
Pia mkuu tunaomba utuongoze jinsi ya vijana kupata mikopo yenye riba nafuu, tunauhitaji mkubwa sana mheshimiwa.
JIBU.
Utaratibu uko wazi kwa vijana kuwezeshwa. Kuna 5% ya mapato yote ya Halimashauri nchini, pia Kuna pesa ya uwezeshaji wa vijana Wizara ya vijana. Tatizo vijana tunalalamika badala ya kuchangamkia fursa. Jiji la Arusha Kuna zaidi ya 1B kwa vijana na kina Mama.
SWALI.
Ndugu mkuu wa Mkoa baada ya ile ajali ya wanafunzi ukiwa kiongozi wa serikali wa ngazi ya juu Kimkoa, ile ajali ya wanafunzi iliyotokea kuna mkakati gani wa kujaribu kuzuia majanga kama yale, pili. Kuna utaratibu gani wa kuwahamisha wanafunzi kutoka wilaya moja kwenda nyingine kwa ajili ya kujifunza jef serikali ya Mkoa inahabarishwa yaani regional education officer? Au mtu mwenye shule akijisikia kuwasafirisha wanafunzi anasafirisha tu?
JIBU.
Kwanza tumeongeza ukaguzi kwenye magari yanayobeba wanafunzi wetu. Pili tumeshauri shule zinazotaka kufanya mitihani ya ujirani mwema ni vema wakatunga mitihani pamoja na Walimu wa kusimamia ndio wakasafiri na si wanafunzi. Walimu wa shule A wakaenda kusimamia shule B na wa shule wakaenda shule
A.
SWALI.
Mh. Mkuu wa Mkoa naomba kuuliza maswali mawili
1.Baada ya msiba kutokea wa Wanafunzi. Wa Lucky Vincent wadau ikiwemo serikali ilichangia rambirambi katika kufanikisha shughuli mbalimbali za msiba ule mzito. Pamoja na taarifa ya mapato na matumizi kusomwa bado kuna mining'ono katika mitandao ya kijamii na hata makundi mbalimbali ya kijamii kuwa pesa zimeliwa. Kubwa zaidi ni kwamba kiasi kilichobaki kitatumika kujengea hospitali ya Mount Meru. Nini kauli yako moja juu ya pesa za rambi rambi kuwa zimeliwa, na pili uamzi wa pesa iliyobaki kuwa itajengea hospitali ni uamzi wako au ni wa kamati kwa kukubaliana na wazazi?
2.Kuna vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoendelea huko Pwani na Lindi vinavyohusisha mauaji kwa viongozi na askari wetu na mpaka sasa chanzo hakijafahamika. Arusha sio kisiwa, Je wewe ukiwa ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa mmejipanga vipi kuzuia na kuhakikisha hayo hayatokei tena hapa Arusha???
Asante
JIBU.
1.Zoezi la kukusanya michango ya Ajali ya basi ya Lucky Vincent liliendeshwa kwa uwazi wa hali ya juu. Kika mzazi aliyefiwa alipewa 3,857,000 pamoja na gharama zote za mazishi. Ilitolewakwa Umma ya mapato na matumizi. Baada ya mazishi wazazi walikuja na wazo la kujenga mnara wa kumbukumbu, tukajadiliana na kupendekeza yapatikane mawazo mbalimbali kuhusu namna Bora ya kuweka kumbukumbu kwenye jambo hili, ikaundwa timu ya wazazi 4 na Serikali kwa jambo hilo ambapo hadi Sasa halijapatikana wazo lililokubalika kutekelezwa. Kwa ujumla nguvu kubwa imepelekwa kwenye kuhudumia majeruhi ambayo ndio faraja pekee iliyobakia. Wapendwa wetu waliofariki hata utoe kiasi gani kwa wazazi hawawezi kufufuka.Hadi Sasa hakuna mradi wowote wa Mount Meru Hospital unaotakana na michango ya Ajali hii.
2. Mkakati wetu Kama mkoa ni kupambamba na wahalifu toka wakiwa vibaka na kabla hawajawa majambazi, maana tukiwamaliza toka wakiwa vibaka hatutatumia nguvu kubwa mbeleni. Tumedhamilia kupambana na dalili za uvunjifu wa amani kwa gharama yoyote. Usalama ni agenda yetu namba moja.
SWALI.
Mh mkuu wa mkoa wa arusha umewezaje kuongoza mkoa wenye changamoto nyingi kama arusha ukizingatia umri wako bado mdogo sana.
JIBU.
Mkuu wa Mkoa ni Taaasisi. Rc ana vyombo vinavyomshauri kwenye kila sekta. Ana instrument zinazomuongoza Kama sheria, kanuni na taratibu. Umri sio kigezo.
SWALI.
Ndugu Mkuu wa Mkoa, Mkoa wetu ni Mkoa wa kitalii na umebeba ajira nyingi, najua kuna taasisi zinazoshughulika na sekta hiyo, lakini tunashuhudia wageni wengi wakifika hapa kwetu hawapati huduma walizotarajia, wanaibiwa kwa nguvu barabarani, wakati mwingine wanapotea mitaani hakuna wa kuwaelekeza, hili linapelekea wageni watuone tuko nyuma sana, huoni haja ya kulisimamia hili pamoja na taasisi zake ile Tija ipatikane zaidi.
JIBU.
Pale polisi tumeteua Askari maalum kwa ajili ya masuala ya utalii. Pili kwa kushirikiana na TATO tumetoa eneo pale polisi ili tujenge kituo cha kushughulika na masuala ya utalii
Tunaendelea pia kutoa Elimu kwa umma.
SWALI.
Mh RC ofisi yako imeathiriwaje na zoezi la wafanyakazi wenye vyeti Feki?
JIBU
Zaidi ya watu 500 wameathirika mkoa mzima.
SWALI.
Ndugu Mkuu wa Mkoa, je hauoni kuna haja ya kukutana na wadau wenye shule binafsi, kujaribu kuona njia ya kuwasaidia wapate mikopo nafuu na ya muda mrefu kwa ajili ya magari mapya ya kubeba wanafunzi,
JIBU.
Wazo zuri, tutalifanyia kazi.
SWALI.
Mimi naomba kuuliza juu ya habari kwenye gazeti la mtazania juu ya mzazi wa marehemu anayesema ameombwa wakubali fedha za rambirambi zitumike kukarabati hospitali.
Nimeona taarifa yako na wala siwaamini, ila naomba kauli yako pia juu ya hilo. Nashukuru na samahani kama limeshaulizwa.
JIBU.
Tanzania Daima na Mtanzania yanajulikana. Leo ukiwauliza mambo ya hela ya Rambirambi kujenga Mount Meru wameyatoa wapi watashangaa. Ukiwataka wathibitishe watasema unabana Uhuru wa vyombo vya habari. Busara ni kuwapuuuza.
HOJA.
Hongera sana mkuu, ila upate muda utembelee halmashauri ya arusha vijijini, barabara ni kero sana huko. Pia nenda kawakague kuna ufisadi mwingi sana wa ardhi.
JIBU.
Naanza ziara huko karibuni.
HOJA.
Mhs.Mimi nina kituo kinachosaidia watu walioathirika na dawa za kulevya Bagamoyo.Ninapenda kuja kufungua kituo Arusha naomba ushirikiano wa ofisi yako ili tusaidie vijana nguvu kazi ya kesho.
JIBU.
Karibu , hiyo ni vita ya kudumu.
MWISHO
UONGOZI UNAOACHA ALAMA