Mdahalo: CCM, Serikali Mbili, Azimio La Arusha

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,436
Motion:

Mwananchi atafaidika zaidi kiuchumi na kijamii iwapo Katika KATIBA MPYA CCM itapigania kurudishwa kwa Azimio la Arusha LILILOBORESHWA kuliko kupigania kurudishwa kwa Serikali Mbili ZILIZOBORESHWA.


Tusemezane.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
CCM hawawezi kurudisha azimio la Arusha kwa sababu utakuwa mwiba kwao. Azmio la arusha lilikuwa na misingi mikuu ambayo ni usawa.. demokrasia, umilikaji wa pamoja wa njia kuu za uchumi chini ya mfumo wa ujamaa nk. ni vigumu mambo haya kurejeshwa na ccm kwani ni sawa na kula matapishi yao.
 
CCM hawawezi kurudisha wala kukumbatia mambo yanayo wazuia kutenda maovu na yenye faida kwa wananchi.Wanacho kifanya ni kile ambacho kina manufaa kwao na kwa chama chao kwanza.
 
Ni kweli mtu mwenye kuitakia mema Tanzania angezungumzia Azimio la Arusha lililoboreshwa ingekuwa bora sana kuliko kuzungumzia serikali mbili zilizoboreshwa kwani hazina maslahi ya moja kwa moja kwa Wananchi. Kwa kuwa Azimio la Arusha lilikuwa ni azimio la utu na lililohakikisha njia kuu za uchumi zinamilikiwa na wananchi ni vigumu sana CCM kupigia debe hoja hiyo kwa kuwa ni kweli kuwa Azimio la Arusha linawaweka uchi viongozi wa chama hicho kiasi kwamba hakuna anayeweza kusimama mbele ya misingi hiyo ya utu. Ilikuwa ni marufuku kwa kiongozi wa uma kujilimbikizia mali. Ni mwanaccm yupi atakayeweza kupigia debe hoja ya namna hiyo wakati kila kukicha mwenye mali ndo mtu wengine ni walala hoi? Haiwezekani kulipigia debe azimio la Arusha kwa mazingira yaliyopo sasa.
 
 
Last edited by a moderator:
CCM Inaweza kabisa kurudisha serikali mbili zilizoboreshwa zikawa ndani yake zimeisha boresha Azimio la Arusha. Kwa maana nyingine, CCM inaweza kupiga ndege wawili kwa kutumia jiwe moja.

Kumbuka kuwa Azimio la Arusha liliishi kwa muda mrefu sana ndani ya serikali mbili na kwa maana hiyo, ni serikali hizo hizo mbili zilizoboreshwa zinaweza kulipa nafasi yake tena.

Serikali tatu haziwezi kuishi na Azimio la Arusha kwa sababu ujenzi wake ulikuwa solely katika msingi na nguzo ya serikali mbili.
 

U.JINGA mwingine bwana! Eti Azimio la Arusha msingi na nguzo yake ilikuwa serikali 2? Hivi kweli wewe unaifahamu MISINGI YA AZIMIO LA ARUSHA?
 
U.JINGA mwingine bwana! Eti Azimio la Arusha msingi na nguzo yake ilikuwa serikali 2? Hivi kweli wewe unaifahamu MISINGI YA AZIMIO LA ARUSHA?
Sasa ulichosema hapa ni nini?.

Sasa kama mimi siifahamu hiyo misingi na nguzo zake, wewe usiye m.jinga ungeonekana unaifahamu kama ungeileta hapa badala ya kupiga kelele za debe tupu.
 
Azimio la Arusha ni habari za kufikirika zilizoshindwa kuwa implemented hata kidekteta na Nyerere.

Leo watu wanasonga mbele, sisi tunataka turudi nyuma! ajabu.

Kitacho tusaidia ni kitu kimoja tu. Tuwache roho za kichawi. Ukimwambia mtu "ndio" iwe ndio kweli, na hiyo inaanzia shule, shule zetu haziwatayarishi wanafunzi kuwa wa kweli wa kauli na nafsi zao, iliharibiwa toka enzi za Nyerere, inabidi tubadilike tuzibadilishe njia na namna zetu za kufundisha na nini cha kufundisha. Elimu na mitaala ndiyo inayo mold Taifa.

Hii nchi haiendelei na wala haitoendelea kwa kuwa na watu ambao bado wanafikiri kuwa na fikra za Kinyerere zilishindwa mwenyewe akiwa hai zinaweza zikafaulu sasa kisha kufa. Maawe!

Tukitaka kuendelea tuachane kabisa na fikra za Nyerere.
 

Mkuu! Kwanini CCM na si Wajumbe wa Bunge wote? Lakini huo ndio Ukweli, japo unauma! Ni wazi kuwa kupata Katiba bora tunategemea KUDRA na MSALIE MTUME za CCM! Ndio MTEGO wetu na tumenaswa!
MAENDELEO NI HESABU! Na Mustakabali wa Taifa si wa kuuchezea Mchezo wa Bahati Nasibu au Kufanyia Majaribio"! TUNATAKA HAKIKA YA USTAWI WETU NA SI KUBAHATISHA! Tuchukue hatua nyuma, HAKUNA KUCHELEWA kwani watoto wetu bado matumboni mwa mama zao! BOTTOM-UP APPROACH! Hakuna wa kusikiliza, haina maana hatutoi sauti, ni wakati wa kujisikiliza!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Haya shosti ni kitu gani kibaya katika AZIMIO LA ARUSHA. Kushindwa ku-implement ni tatizo la fikra za Mwalimu au watu? Jibu straight to the point usianze kupaparika.
 
Mengi ya yaliyokuwemo kwenye Azimio la Arusha lililoboroshwa tayari yako katika Rasimu ya Pili ya Katiba.
 
Wadau,

Katika nukuu hapo chini:
*Yepi bado yanatufaa katika nyakati hizi bila ya kuyabadilisha.
*Yepi yanatufaa lakini baada ya maboresho au marekebisho.
*Yepi hayatufai, hivyo tuachana nayo?

Tujadiliane kwa hoja.

On the Policy of Self-Reliance in Tanzania, February 5, 1967.

Source:
From Africa Report, March 1967 issue of pp. 11-13


Haya yote CCM iliamua kuachana nayo mwaka 1992 na kuleta azimio la zanzibar. Kuanzia hapo, CCM ikaachana na wanyonge na kuanza kuwa karibu zaidi na wenye nguvu - kwa nchini mafisadi, kwa walio nje - wawekezaji. Mwananchi akabaki kuwa ni mtu wa kuokoteza okoteza tu maisha ndani ya mfumo wa uliberali HOLELA.

Kwa wale wanaohitaji tafsiri ya kiswahili, nitajitahidi kuileta.

Tusemezane.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 


Asante kwa kutukumbusha, lakini nitumie nafasi hii kukukumbusha pia kuwa Azimio la Arusha lilikuwa kwa Tanzania Bara tu na kamwe Hayati Mzee Karume hakukubali litekelezwe Zanzibar. Mwenyewe alisema mwisho wa Azimio hilo ni kisiwa cha Chumbi- (ukitokea bara kabla ya kufika Zenji). Kwa hiyo sio sahihi kusema kuwa lilipata hifadhi kwenye serikali mbili kwani utekelezaji wake ulikuwa wa upande mmoja wa Muungano.
 
Mara nyingi kama sio zote CCM huwa inamkumbuka na kumuhitaji mwananchi wa kawaida wakati wa kupiga kura, baada ya zoezi la kupiga kura hali ugeuka na mwananchi wa kawaida uanza kupigwa kula na Viongozi aliowachagua kwa matumaini makubwa!
 
Faiza,

You are negatively critical of Mwl. in all your postings. which takes away any creative thinking on your part. You are making massive attempt (and poorly at that) to reduce his stature to that of the likes of Mobutu, Gadafi, et al.
You may dislike Mwl and you are entitled to your feelings, by the way, but you are unreasonable to challenge the ideologies he propounded without due regard to the times he lived and the resources (people, etc,) around him and the global challenges to that matter.
He was a human being, just like you and I. If patriotism is a yardstick to use, how would the likes of you compare to him?? What have you done for your country? He, on the other hand, will remain in history books as one of the greatest Africans to have graced this continent, love it or hate it, my dear sister!

PP
 
AZIMIO LA ARUSHA ilipitishwa na almashauri kuu ya TANU mwezi januari 1967 na kuthubitishwa na mkutano mkuu wa TANU mwezi marchi 1967 na kutolewa mwaezi februari 1967. IMANI YA TANU siasa ya TANU ni kujenga nchi ya ujamaa. misingi ya ujamaa imetajwa katika katiba ya TANU nayo ni:-

  • kwamba binadamu wote ni sawa
  • kwamba kila mtu anastahili heshima
  • kwamba kila raia ni sehemu ya taifa na anayo haki ya kushiriki sawa na wengine katika serikali kuanzia ya mtaa mkoa hadi serikali kuu
  • kwamba kila raia ana haki na uhuru wa kutoa mawazo yake,kwenda anakotaka .kuamini dini anayitakana kukutana na watu mradi havunji sheria
  • kila mtu ana haki ya kupata kutoka kwenye jamii ifadhi ya maisha yake na mali yake aliyonayo kwa muhujibu wa sheria.
  • kwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo ya haki kutokana na kazi yake.
  • kwamba raia wote kwa pamoja wanamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana kwa kizazi chao.
  • kwamba ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakwenda sawa serikali lazima iwe na mamlaka kamili juu ya njia za muhimu kukuza uchumi.
  • kwamba ni wajibu wa serikali ambayo ni watu wenye kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya taifa ili kuhakikisha ustawi wa raia wote na kuzuia mtu kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa
MADHUMUNI YA TANU:

  • kwa hivyo basi ,makusudi na madhumuni ya TANU yalikuwa kama ifuatavyo...
  • kudumisha uhuru wa nchi yetu na raia wake
  • kuweka heshima ya mwanadamu kwa kufuata barabara kanuni za tangazo la ulimwengu la haki za binadamu
  • kuhakikisha kwamba nchi yetu inatawaliwa na serikali ya watu wa kidemokrasia na ya kisoshalist
  • kushirikaiana na vyama vyote vya siasa katika Afrika vinavyipigania uhuru wa bara lote la Afrika
  • kuona kwamba serikali inatumia mali yote ya nchi kuondosha ujinga maradhi na umasikini
  • kuona kwamba serikali inasaidia kwa vitendo kuunda na kudumisha vyama vya ushirika.
  • kuona kwamba kila iwezekanapo serikali inashiriki katika hasa katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu
  • kuona kwamba serikali inatoa nafasi sawa kwa wote wake na waume bila kujali rangi kabila wala dini
  • kuona kwamba serikali inaondoa kila aina ya dhuluma vitisho ubaguzi rushwa na upotofu
  • kuona kwamba serikali ya nchi yetu inasimamia barabara njia kuu za kuzalisha mali na inafuata barabar a siaisa ambayo inarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali ya nchi yetu
  • kuona kwamba serikali inashirikiana na dola nyingine katka Afrika kuleta umoja wa Afrika.
  • kuona kwamba serikali inajitahidi kuleta amani na salama ulimenguni kwa njia ya chama cha umoja wa mataifa
  • SIASA YA UJAMAA.>HAKUNA UNYONYAJI...nchi yenye ujamaa kamili ni nchi ya wafanya kazi,haina ubepari wala ukabila haina tabaka mbili za watu, tabaka la chini la watu wanaoishi kwa kufanya kazi,na tabaka la juu la watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi, na katika nchi ya ujamaa kamili mtu hanyonyi mtu bali hawezaye kufanya kazi hufanya kazi.nchi yetu ni ya wakulima na wafanyakazi lakini si nchi ya ujamaa kamili ina misingi ya ebepari na ukabaila wa vishawishi vyake.misingi hii ya ukabaila na upeapri yaweza ikapanuka na kuenea
NJIA KUU ZA UCHUMI NI YA WAKULIMA NA WAFANYA KAZI.namna ya ya kujenga na kudumisha ujamaa ni kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu zinatawaliwa na wakulima na wafanya kazi wenyewe kwa kutumia vyombo vya serikali yao na ya vyama vyao vya ushirika, pia kuthibitisha kuwa chama kinachotawala ni cha wakulima na wafanyakzi. Njia kuu za uchumi ni kama ardhi,misitu,madini,maji,mafuta na nguvu za umeme. Njia za habari,njia za usafirishaji,mabenki na bima,biashara za nchi za kigeni na biashara za jumla.... I wish CCM irejee misingi ya TANU kama itawezekana nyakati hizi...
[h=4][/h]
 

Shukran RockSpider,

Msingi wa mada yangu ni je - what makes sense zaidi linapokuja suala la kuinua wananchi kiuchumi na kijamii - je turudi katika serikali mbili zilizoboreshwa chini ya katiba mpya au azimio la arusha liliboreshwa?

Kwa maana nyingine - ccm ingeeleweka zaidi kulinda maslahi ya umma kwa kupigania azimio lililoboreshwa au serikali mbili zilizoboroshwa?




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hoja yako iko crystal clear! Azimio la Arusha lililoboreshwa ndiyo suluhisho la matatizo yetu kama nchi! Hili wananitambua sana lakini Sera za Uwekezwaji according to Prof Chachage zinatuandaa kuwekezwa kama nchi! IMF, WB na Nchi wahisani hawezi kukubali Azimio la Arusha lirejee hata likiwa na maboresho yatakayowanufaisha! Mpaka sasa hivi wanadai eti mazingira ya uwekezaji Tanzania siyo rafiki sana !!! Back kwenye mada, CCM wangetutendea haki wananchi kwa kurejesha Azimio la arusha kwani hofu ya kutengwa na western imekwisha baada ya Wachina kuja juu! Sera za wachina ziko wazi sana wao ni 50/50 hawana unafiki wa kuangalia masuala ya ndani ya nchi nyingine! Sasa hivi nchi za magharibi zinatuhitaji kuliko tunavyowahitaji! Wakenya wamejitambua wakakataa misaada katakata na sasa wanapaa kiuchumu...Once again Azimio la Arusha ndo suluhu la matatizo yetu kwa chama chochote kitakacho shika dola coming 2015...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…