MCT, LHRC, THRDC Watinga Mahakama ya EACJ kupinga sheria ya huduma za vyombo vya habari

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Sheria-ya-Vyombo-vya-Habari-750x375.jpg

Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Haki za Binadamu Tanzania ( THRDC) leo Jumatano ya Januari 11, 2017 wamefungua kesi ya kuipinga Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya mwaka 2016 katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kesi hiyo, Katibu Mtendaji MCT, Kajubi Mukajanga amesema washirika waliofungua kesi hiyo wanataka baadhi ya vifungu vya sheria vinavyokandamiza uhuru wa habari na kujieleza vifutwe kwakuwa vinakiuka matakwa ya mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Na kwamba mahakama ya EACJ imepewa mamlaka ya kutafsiri mkataba huo na kuhakikisha nchi wanachama wanaufuata na kuusimamia.

“Vifungu hivyo vya sheria vinakandamiza uhuru wa habari na wa kujieleza, vifutwe kwani vinakiuka matakwa ya mkataba wa EAC ambao unataka nchi mwanachama kuzingatia na kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba huo kwenye ibara ya 6(d) na 7(2),” amesema.

Amesema kuwa, Ibara ya 6(d) ya mkataba wa EAC inahimiza umuhimu wa kufuata kanuni za utawala bora, wa kidemokrasia, sheria, uwajibikaji, uwazi na haki kwa wote ikiwa pamoja na usawa wa kijinsia, kulinda na kuheshimu haki za binadamu.

“Kama ilivyo kwenye kifungu cha 8(1) (c), Tanzania inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha haki zote zinazotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Helen Kijo-Bisimba amesema baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vinakiuka haki za binadamu na kwamba wameshiriki kufungua kesi hiyo ili kuipinga sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari.

“Sheria imekaa sivyo, tumeona tuungane na wenzetu ili kuipinga sheria hii,” amesema.

Mkurugenzi wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema sheria inabidi ibadilishwe hasa katika vifungu kandamizi kabla ya kuanza kutumika.

“Kuna mazingira yatakayowaweka katika mazingira magumu waandishi wa habari, ni vyema kuipinga sheria hii isitumike hadi ibadilishwe.”

Chanzo: Dewji Blog
 
Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Haki za Binadamu Tanzania ( THRDC) leo Jumatano ya Januari 11, 2017 wamefungua kesi ya kuipinga Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya mwaka 2016 katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunguliwa kesi hiyo, Katibu Mtendaji MCT, Kajubi Mukajanga amesema washirika waliofungua kesi hiyo wanataka baadhi ya vifungu vya sheria vinavyokandamiza uhuru wa habari na kujieleza vifutwe kwakuwa vinakiuka matakwa ya mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Na kwamba mahakama ya EACJ imepewa mamlaka ya kutafsiri mkataba huo na kuhakikisha nchi wanachama wanaufuata na kuusimamia.

“Vifungu hivyo vya sheria vinakandamiza uhuru wa habari na wa kujieleza, vifutwe kwani vinakiuka matakwa ya mkataba wa EAC ambao unataka nchi mwanachama kuzingatia na kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba huo kwenye ibara ya 6(d) na 7(2),”
amesema.

Afrika Mashariki? Tunaweza tusitekeleze hiyo hukumu!!
 
Baraza la Habari nchini Tanzania limewasilisha kesi mahakamani kupinga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo Novemba mwaka jana.

Baraza hilo limewasilisha kesi hiyo katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) likishirikiana na mashirika mawili ya kutetea haki za kibinadamu; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.

Baraza hilo linaaka baadhi ya vifungu vya sheria, ambavyo wanasema vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza vifutwe.

Wanasema vinakiuka matakwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zinataka nchi wanachama kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba wa kuundwa kwa jumuiya hiyo.

"Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unahimiza umuhimu wa kufuata kanuni za utawala bora, utawala wa kidemokrasia, utawala wa sheria, uwajibikaji, uwazi, haki kwa wote, usawa wa kijinsia na kuheshimu haki za binadamu," baraza hilo linasema kupitia taarifa iliyotiwa saini na katibu mtendaji Kajudi Mukajanga.

"Tanzania inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha haki zote zilizotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa."

Source: BBC
 
Sasa awamu hii ataomba mizimi ya kwao ije ifunge mitandao naona malaika wamekataa maombi yake, hii inadhihirisha malaika huwa wanasimama upande wa haki, na alichokiomna hakikuwa ni haki.

Mungu simama mwenyewe ktk hii kesi.

Amen!
 
Haki za binadamu kwenye masuala yasiyokuwa na tija utawaona pua mbele mbele, lakini Serikali ikitimiza wajibu kwa Wananchi wake, ikiondoa kero, ikisimamia na kudhibiti rushwa, Haki za binadamu kimya kama hawapo, Watu wamepigwa huko Tarime, haki za binadamu huwaoni, maafa ya mtoni watu kufungwa kwenye mifuko, haki za bindamu kimyaa, wakulima na wafugaji kuuwana haki za binadamu kimya? Sasa nauliza Hakiza za Bindamu mnafanyakazi kwa maslahi ya Upinzani hususan Chadema aunachagua binadamu wa kutetea? Kuweni wazi tu ili msajiri wa vyama awatambue.
 
Sasa awamu hii ataomba mizimi ya kwao ije ifunge mitandao naona malaika wamekataa maombi yake, hii inadhihirisha malaika huwa wanasimama upande wa haki, na alichokiomna hakikuwa ni haki.

Mungu simama mwenyewe ktk hii kesi.

Amen!
yeye anaomba malaika waje wafunge mitandao halafu anataka sisi tumuombee!!!?
Muda tulionao sasa hivi ni kuwaombea wenye mapepo na mkuu wetu sio miongoni mwao
 
Back
Top Bottom