Mchwa waliizidi nguvu awamu ya nne, awamu ya tano kazi mnayo kwenye majipu

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Rais wa awamu ya nne alikuwa mwanamichezo, mpaka kesho ni shabiki mkubwa wa Taifa Stars, anaipenda basketball, nasikia aliwahi kuucheza mchezo huo enzi za ujana wake.

Rais wa awamu ya nne alijaa/amejaa ucheshi na ukarimu, kwenye suala la ubinadamu na ule urahimu kwa kweli nampa alama zote anazopaswa kupewa mtu anayefanya vizuri kwenye mtihani.

Lakini alizungumzia Mchwa kwa maana ya wezi wa kwenye halmashauri, akaongea kwa mkwara mzito alipokutana na watendaji walio karibu na wananchi. Cha ajabu ni kwamba mchwa waliachwa wakaiharibu kabisa nyumba, wakamtafuna mwenye nyumba na matokeo yake kaota majipu mwili mzima!.

Rai yangu kwa uongozi wa awamu ya tano, msije kuhukumiwa vibaya kupitia utumbuaji wa majipu, mmeanzisha vita nzito ambayo ni lazima mpaka mwisho mpambane ili muweze kuibuka washindi.

Kila zinapoibuka tuhuma nzito za wizi mkubwa uliofanywa ndani ya awamu ya nne, naona kama vile ile kauli ya mchwa ilikuwa ni ya kisiasa tu, haikuwa na ufuatiliaji matokeo yake uliibuka wizi juu ya wizi juu ya wizi!!.

Utumbuaji wa majipu ni mtihani kwa wahusika wote wenye mamlaka, kwani wakizidiwa nguvu na mafisadi wenye fedha waliyoipata kwa njia haramu, upo uwezekano wa awamu ya tano kukumbukwa kwa kejeli kama vile awamu ya nne inavyokumbukwa kwa kejeli ya neno "mchwa" lililotumiwa na JK mara kwa mara.

Natumaini walengwa wa ujumbe huu watausoma na kujipima kama kweli wanataka kupambana mpaka mwisho halafu wakakumbukwa kwa heshima au wanataka kuifanya hii kazi nusu nusu halafu waishie njiani baada ya kunaswa kwenye mtego wa wale wanaotumbuliwa.

Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga, nadhani nimeeleweka vizuri.
 
Masikini Bukililo hivi huoni aibu?uzi una zaidi ya saa moja na kitu hakuna mchangiaji hata mmoja ?huoni kuwa hiyo ni sababu ya kuamini kuwa uzi wako hauna mashiko?vijana wa ccm mnatia aibu sana
 
Wapo wengi sana wanatuma like ingawa hawachangii, kitu muhimu kwangu ni kufikisha ujumbe kwa watu husika, mazungumzo yanayoibuka kwa maana ya uchangiaji wakati mwingine sio kusudio la kuanzisha uzi, ukisoma ukaelewa kilichoandikwa unakuwa umeelimika na hicho ndicho muhimu kwangu.
 
Masikini lumumba mnatia huruma
 
Back
Top Bottom