PostGE2025 Mchungaji Wanjohi wa Kenya: Mmeona Ripoti ya Madowo jinsi watu walivyouawa Tanzania? Kama ni kweli, naomba ICC iingilie

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Sehemu ya mahubiri ya Mchungaji Dr.John Chege Wanjohi (PhD), kutoka nchini Kenya ambaye pia ni Balozi wa Amani wa Umoja wa Mataifa. Nimeweka tafsiri isiyo rasmi;

"Mmeona ripoti ya Larry Madowo na jinsi watu walivyouawa Tanzania? Kama tulichoona ni kweli, serikali imeua watu wengi kiasi kile naomba ICC iingilie kati. Nililia jana usiku nilipoona ile ripoti. Ngoja nikueleze ni jinsi gani unaweza kujua mtu ana roho mbaya. Ni yule atakayeona hayo mauaji na aseme "hizo ni propaganda".

Unawezaje kusema kitu cha aina hiyo ni propaganda, wakati tumeshuhudia miili mingi imelala mtaani? Kama si kweli natoa rai kwa serikali ya Tanzania kuishtaki CNN. Washtakini sasa maana wamechafua jina lenu. Natoa rai kwa Suluhu kuishtaki CNN. Roho yangu inaniuma sana. Mimi siyo kama nyie. Nikiona jambo lisilo la utu roho yangu inaniuma sana.

Kwanini watu wafe kisa eti nataka madaraka? Kama watu hawakutaki pumzika kwa amani. Kwa nini unataka kujilazimisha kwa watu wasiokutaka. Kama umefanya kazi nzuri acha watu wenyewe waamue.

Mimi sina muda wa kukuambia tangu niingie madarakani nimejenga barabara, kwani hamzioni? Maandiko yanasema tutawajua kwa matendo yao, kama kweli nimefanya kazi matendo yangu yatasema kwa niaba yangu. Sina sababu ya kupayuka kila saa nilichofanya. Nilichofanya kitajisema chenyewe.

Kilichotokea Tanzania ni aibu kubwa kwa Afrika. Naishauri serikali ya Kenya isijaribu kujiingiza kwenye hiyo laana. Nimemuona Waziri wetu Mudavadi akiulizwa kwa nini alipongeza ushindi wa Samia, hakuweza kujibu zaidi ya kujiumauma. Eti nakupongeza kwa ushindi. Ushindi gani? Hapakuwa na ushindi wowote katika ule uchaguzi. Ni serikali gani uliwahi kuisikia ikipata 98%? Hata Trump?

Kuna watu watasema hubiri injili mambo ya siasa acha. Sijui huwa wanajionaje? Mmewahi kutazama hata midomo yao wanavyoongea?? Huwa wanajiona kama wana hekima sana. Subiri uitiwe mwili wa mama yako ndiyo utajua kama una hekima. We subiri. Sasa hivi si unaona tunaongea ujinga? We subiri mama yako apigwe risasi uambiwe ukaokote mwili wake, ndiyo utatuelewa."

Your browser is not able to display this video.
 
Samuya lazima aburuzwe kortini ICC, ushahidi upo wa kutosha...ni suala la muda tuu akajibu huko imekuwaje raia waliompigia kura 98% amewaua namna ile!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…