Mchungaji wa kilokole kizimbani kwa tuhuma za kubaka mwanaye

Reucherau

JF-Expert Member
Nov 26, 2014
756
1,740
Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (FPCT) Tawi la Gezaulole wilayani Hai, Emanueli Mwikizu (42) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 7.

Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Anold Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha Moleli amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kuzini akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu nyumbani kwake mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo ambapo hakimu anayesikiliza kesi hiyo aliharisha hadi Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa yupo rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

Chanzo: Mwananchi
 
HAWA WACHUNGAJI WA KILOKOLE HAWAISHI VITUKO! KILA SIKU WAO TU! SA KWENDA KUMLAMBA MWANAO KWELI ????
 
kesi iko mahakamani, kwa hiyo kwa mujibu wa sheria za nchi kujadiki hii ni makosa.
"Tii sheria Bila shuruti"
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Wabakaji wao, wanyweshawatu maji ya betri wao, walisha watu nyasi wao, watembea migongoni mwa watu wao, wapiga ramli wao, wachungulia nyeti za watu wao, wabakaji wao duh, hizi dini zingine majanga
 
Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (FPCT) Tawi la Gezaulole wilayani Hai, Emanueli Mwikizu (42) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 7.

Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Anold Kirekiano mwendesha mashtaka wa polisi, Elisha Moleli amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa la kuzini akijua kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu nyumbani kwake mtaa wa Gezaulo majira ya saa 3:30 asubuhi kwa kumwingilia kwa nguvu na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.

Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo ambapo hakimu anayesikiliza kesi hiyo aliharisha hadi Februari 9 mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa yupo rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

Chanzo: Mwananchi

Walokole daima ni watu wa vituko tu. Utawasikia kufanya mapenzi ni dhambi, ila wao ndiyo wanao ongoza kuangalia sinema za ngono na kujichua.
 
Jamaa hariri pale.Umeandika ALIHARISHA mpaka feb....
Yote kwa yote huyo ni mhuni kama wahuni wengine.Sheria ifwatwe kama kweli kafanya hivyo ufungwe bila huruma.Kwa kashfa hiyo tayari uchungaji ndio kajitemesha mwenyewe.
 
Mchungaji wa kanosa la FPTC wilayani HAI , Emannuel Mwikizi aburuzwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 7. Mtuhumiwa alitenda kosa hilo jan 17 mwaka huu majira ya saa 3.30 usiku nyumbani kwake Gezaulo kwa kumuingilia kwa nguvu mtoto wake na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/1597578-3789312-t7584sz/index.html

Mytake: Kama hawa ndio wachungaji wa sasa.....sijui kama dada, wake wa waumini wanasalimika.
 
Back
Top Bottom